Pendekezo: SLAA amrithi SUMARI Arumeru!

Pendekezo: SLAA amrithi SUMARI Arumeru!

Owk owk...ametumia akili na busara sana kufanya huo uamuzi. Kwa sasa Tanzania hatuitaji kuwa na viongozi wazee kama yeye. Tunataka vijana watakaoleta mabadiliko na mbinu mpya za kumkomboa mtanzania.

Kwani katibu mkuu wa ccm mliyemtoa kwenye retirement ni kijana? Busara za wazee zinahitajika pale mustakabali wa Taifa unapozungumziwa ama sivyo hao unaowaita vijana ni rahisi kurubuniwa na vijisenti vidogo kama walivyofanya DOWANS kwa zito!! Wakamuhonga na HAMMER; hawezi kubisha hata siku moja kwani huko alikotoka kunajulikana wazi na kila mtu!!
 
Nilitaka kukukumbusha tu kwamba aliweza kuwa mbunge na katibu pia na alikiimarisha chama ndio mpaka leo wewe unajivunia watu kama zitto kabwe ni matunda yake licha ya kuwa mbunge,na slaa anaweza kuwa mbunge na akaimarisha chama,upo hapo!leo ni hoja juu ya hoja tu hapa
Kwanini usishauri kuwa Wilson Mukama agombee kwa ticket ya ccm?
 
Binafsi napendekeza CHADEMA imsimamishe Dr.SLAA kwenye kinyang'anyiro cha ubunge huko Arumeru. Hii itaipa chadema kwanza nafasi kubwa ya kukinyakua kiti hicho kwa kuwa Slaa kwa sasa ni heavy weight politician na pia watanzania wenye uchungu na nchi hii tumekuwa tukiukosa mchango wa Dr pale bungeni.

Wengi tunaukumbuka ujasiri wake akiwa anga zile, kiukweli Mboe anapwaya kwenye nafasi ya kiongozi wa upinzani pale bungeni,waziri mkuu Pinda na serikali yake wanahitaji kuchangamshwa na mtu machachari wa aina ya Slaa,Lema au Tundu!....

Mboe amekua na huruma huruma hivi,sasa slaa kama atafanikiwa kushinda ubunge(nina uhakika atashinda)basi mh.mboe awe muungwana kwa kumpisha bwana Slaa kiti cha kiongozi wa upinzani!hii imekaaje wadau,yote ni katika kuimarisha makali ya bunge.
Mie siungi mkono hoja yako. kwanza sioni kama Mbowe amepwaya badala yake naona amefanya mambo makubwa sana bungeni i.e ameufanya upinzani uwachangamshe ccm kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea nchini. Namuona mbowe kama ni kiongozi bora na thabiti kuwahi kutokea ktk siasa za upinzani. Pili naona performance ya wabunge wa chadema bungeni imeongezeka sana kuliko bunge lililopita hivyo sioni kama kuna uhitaji mkubwa wa Slaa kwa sasa bungeni. Tatu Slaa kwa sasa yuko next level ktk siasa za TZ anatakiwa kuwa Rais ajaye japo kama isingekuwa NEC ya ccm angekuwa ametangazwa kama Rais. Mwisho kwa sasa Slaa ni productive zaidi ktk chama kuliko alivyokuwa mbunge, tofauti na huko nyuma majukumu ya katibu wa chadema yameongezeka kwa kasi kiasi kwamba anahitajika mtu asiyekuwa na majukumu mazito kama ya ubunge. Anachotakiwa kufanya slaa ni kuzidi kuhamasisha chama kiendelee kusambaa mijini na vijijini.
 
Hakuna tatizo. Anzisha Thread tutajadili.

ANGALIZO: Najua kuna makundi katika CDM ambayo yanapingana, wakati mwingine kwa hoja dhaifu sana. Sina hakika wewe uko kwenye kundi gani kati ya hayo. Bahati mbaya mimi sipendelei mfumo wa makundi maslahi kwani yanaonyesha udhaifu wetu wa kufikiri. Hata wewe hapo nimeona ni pro- Zitto kwa namna unavyotaka suala la posho lionekane ni la mtu binafsi.
Huyo sio chadema ni ccm au kikundi cha watu ambacho kwa maslahi ya taifa hatupendi kukitajataja.
 
Owk owk...ametumia akili na busara sana kufanya huo uamuzi. Kwa sasa Tanzania hatuitaji kuwa na viongozi wazee kama yeye. Tunataka vijana watakaoleta mabadiliko na mbinu mpya za kumkomboa mtanzania.
Masha, Ngeleja na Maige wamewaletea mabadiliko gani?
 
Hakuna tatizo. Anzisha Thread tutajadili.

ANGALIZO: Najua kuna makundi katika CDM ambayo yanapingana, wakati mwingine kwa hoja dhaifu sana. Sina hakika wewe uko kwenye kundi gani kati ya hayo. Bahati mbaya mimi sipendelei mfumo wa makundi maslahi kwani yanaonyesha udhaifu wetu wa kufikiri. Hata wewe hapo nimeona ni pro- Zitto kwa namna unavyotaka suala la posho lionekane ni la mtu binafsi.

Hivi kwanini watz siku hizi hawawezi kutofautiana mawazo bila kuwa makundi tofauti au bila mmoja kuhusishwa na u pro fulani?kwanini tumefikia hapo yani tunatakiwa wote kuwa na fikra na mitazamo inayofanana?sidhani kama hii kitu inaonyesha dalili njema,nadhani tukubali kutofautiana kimawazo na mitazamo itatujenga zaidi,we have to accept different opinion for the same issue bila kuhusisha u pro ama u anti,mfano tunasema zitto kuna watu wanataka suala la posho lionekana la mtu binafsi(zitto)lakini hatusemi kivipi?maana zitto ni kweli amepinga posho tena sio kwa maneno bali kwa vitendo,je hastahili credit hasa toka kwetu ma anti-posho?

Nikuhakikishie tu kwamba mimi sina kundi lolote huko chadema na wala siamini kama chama makini na cha kidemokrasia kama chadema kinaweza kuwa na u.p.u.u.z.i huo wa magenge ndani yake naomba hapa uniruhusu nisikubaliane na wewe kwa hilo,sanasana kundi langu ni la tax payers ambao ni ma anti-posho kwenye kundi hilo ndipo tumo na kina zitto ambae ni kama kiongozi wetu kundini humo
 
Kwanini usishauri kuwa Wilson Mukama agombee kwa ticket ya ccm?

kumbuka nilichosema lengo langu la kupendekeza hili la slaa kugombea is nothing than kuimarisha makali ya bunge,haiyumkiniki kutaka kuimiarisha makali ya bunge kwa kuongeza bungeni wabunge kutoka kwenye chama chenye wabunge wengi,hapo tutakua hatuliimarishi bunge letu na kulipa makali yanayostahili ya kuisimamia serikali.

Naongeza ushauri mwingine ambao nimeshawahi kuutoa huko nyuma kwa wapinzani hasa chadema,acheni mawazo ya urais,badala yake mconcetrate kwenye kujiimarisha bungeni,mnaweza kuunda serikali bila kutoa rais,amkeni usingizini nyie watu,nani kawaroga vibaya kiasi hicho
 
Dr Slaa akikubali na akashindwa umaarufu wake utazidi kupotea kwani ni mwaka mmoja na miezi nne tu iliyopita alishindwa Uras. Angetulia kwanza kupima upepo
Sema umaarufu wake utapotea sio utazidi kupotea aliyekwambia kwamba umaarufu wa Dr. slaa umeanza kushuka nani? kwani kitu kinachozidi kushuka lazima kiwe tayari kilishaanza kusuka!!
 
Wala sijasoma sana comments lakini assumptions za kawaida you don't need any stochastic processes to prove this, Slaa akigombea amemalizika kisiasa na upinzani utakuwa
kwenye hail Ngumu! No way! Huyu bwana ni Rais siyo mbunge mbowe is more than enough na mkubwa lissu. No loss should hit you hard that you will avoid with constant care! So long as you know the risks, only four alternatives, accept, reject, transfer and lastly mitigate, Kama kuna mtu ana nyingine aseme, na Slaa get away of this for the future of the country you simply reject!
 
Ni wazi dr slaa usiende kugombea kule arumeru CCM itashinda na utahaibika bure kama uamini nenda!
 
Mbowe: Dr Slaa ruksa kuwania ubunge Arumeru
ALIYEPEPERUSHA BENDERA CHADEMA 2010 AREJEA KUTOKA MAREKANI, AUNGA MKONO
Musa Juma na Moses Mashalla, Arusha

WAKATI Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa akianza kugusa hisia za watu wanaomtaka agombee ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki, mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amesema iwapo mtendaji mkuu huyo wa chama ataamua kuwania kiti hicho, wataheshimu uamuzi wake.

Wakati Mbowe akitoa kauli hiyo, aliyepeperusha bendera ya Chadema katika uchaguzi wa mwaka 2010, Joshua Nasari na kutoa upinzani mkali kwa mgombea wa CCM, marehemu Jeremiah Sumari, naye amesema kama katibu mkuu wake ataamua kuwania kiti hicho, hatakuwa na pingamizi ikiwa chama kitaamua kwani lengo ni kutwaa jimbo hilo.

Akizungumza na Mwananchi jana baada ya kuibuka mjadala kuhusu uwezekano wa Dk Slaa kuwania jimbo hilo, Mbowe alisema, "Katika suala la kugombea, utashi binafsi ni jambo la msingi...,kama Dk Slaa ataamua kugombea ubunge Arumeru Mashariki, tutaheshimu uamuzi wake."

Mbowe alisema katika uteuzi wa chama, kuna vigezo vinavyoangaliwa ikiwa ni pamoja na jinsi mtu anavyokubalika kwa wananchi anakogombea, sifa zake na utashi wake binafsi na kuongeza, "Hatuna uteule katika chama."

Hata hivyo, Mbowe alisema Chadema hakiwezi kumlazimisha Dk Slaa akagombee jimbo hilo kama mwenyewe utashi haumtumi kufanya hivyo, na kwamba hana shaka na kukubalika kwa katibu mkuu huyo kutokana na imani aliyojijengea kwa umma wa Watanzania.

Mbowe alisema Dk Slaa amekuwa akiombwa kugombea ubunge katika maeneo mengi likiwamo Jimbo la Igunga, lakini chama kisingeweza kumlazimisha kwani jambo la kwanza ilibidi mwenyewe aonyeshe utashi binafsi wa kutaka kuwania kiti hicho.

"Dk Slaa aliwahi kuombwa akagombee Igunga, lakini hakwenda. Hii ni kwasababu anakubalika nchini karibu kote, hivyo kama atakuwa na utashi binafsi kwanza, nadhani taratibu za chama zitatumika tu kufikia uamuzi," alifafanua.

Mwenyekiti huyo wa Chadema pia alitoa angalizo kwamba, wakati mwingine uamuzi wa chama kupata mgombea unaangalia jinsi mgombea alivyo na mtandao katika jimbo analotaka kugombea ili hata kama akichaguliwa aonekane ni mbunge wa eneo hilo.

"Ndiyo maana nasema kuna vigezo vingi tu, kwa mfano mtu anaweza kuwa mbunge mzuri bungeni, lakini je, ana connectivity (kinachomuunganisha) jimboni, kuangalia kama ana makazi na mtandao mwingine kwani asije akawa mbunge mzuri bungeni, lakini jimboni akiwa kama mgeni hivyo watu wakaona kama kimewapelekea pandikizi tu,"alifafanua Mbowe.

Tangu juzi kumekuwa na mjadala katika mitandao ya kijamii huku baadhi wakimtaka Dk Slaa akagombee ubunge Arumeru Mashariki kuziba pengo la aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Marehebu Sumari, lakini wengine wanapinga na kumtaka aendelee kubaki na nafasi yake ya katibu mkuu wa chama kwa lengo la kukijenga.

Hata hivyo, Dk Slaa ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 alishika nafasi ya pili akiwa nyuma ya Rais ya Jakaya Kikwete, juzi alinukuliwa na gazeti moja la kila siku (siyo Mwananchi) akisema, "Siwezi kulizungumzia jambo hilo, maana nilikwisha kusema muda mrefu kuwa sitaki tena ubunge na isitoshe mimi si mwenyeji wa Arumeru,"
Joshua Nasari

Kwa upande wake Nasari (26) ambaye ana mtaji mkubwa wa kura kufuatia matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2010 alitoa msimamo wake akisema yupo tayari kufanya mazungumzo na viongozi wa juu ya chama chake juu ya kumpisha Dk Slaa kuwania ubunge katika jimbo hilo kama akihitaji.

Nasari ambaye amerejea hivi karibuni mjini Arusha akitokea nchini Marekani, leo anatarajiwa kuchukua fomu rasmi ili kuwania nafasi hiyo kupitia Chadema.

"Nimesikia maoni kupitia mitandao na wadau wakimuomba Dk Slaa kugombea, hili ni jambo jema kwetu kwani wananchi wanajua jimbo hili tunashinda Chadema na kama Dk (Slaa) akitaka kugombea dekomrasia ya chama chetu itafanya kazi, kwani kikubwa tunataka ushindi,"alisema Nasari.

Nasari aliyewahi kuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso) kati ya 2008 na 2009 alipohitimu shahada ya Sayansi ya Jamii katika masuala ya utengenezaji Sera na Utawala, alisema ana imani Chadema kitashinda Arumeru.

"Nilikuwa Marekani kikazi na sasa nimerejea kama ulivyoshuhudia watu wengi wananiunga mkono na tayari wamenichangia Sh 11milioni za kampeni na magari manane," alisema Nasari.

Mgombea huyo ambaye tayari ametangaza kuacha kazi katika shirika la Kimarekani la Foundation For Tomorrow ili kujikita kwenye uchaguzi huo, alisema wakazi wa Arumeru Mashariki wanahitaji mwakilishi sahihi ambaye anaweza kuwatetea katika kuinua uchumi wao.

Hata hivyo, alisema tayari amepata taarifa za Dk Slaa kutoa tamko kuwa hawezi kushiriki katika uchaguzi huo, kwa kuzingatia kuwa sio mkazi wa Meru na pia hana nia ya kugombea kiti hicho.

"Nategemea Dk Slaa na viongozi wengine wa kitaifa, wakiwapo wabunge, marafiki zangu wa vyuo vikuu na wengine wengi tutakuwa nao Arumeru kuhakikisha Chadema inashinda,"alisema Nasari.

Hadi kufikia jana, kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema Mkoa wa Arusha (Bavicha), Ephata Nanyaro, wanachama waliokuwa wamechukua fomu ni Yohane Kimuto, Samweli Chami na Rebecca Mwingisha na leo Nasari atakuwa mwanachama wa tatu.

"Tunatarajia wanachadema wengi zaidi watajitokeza katika siku hizi zilizobaki ili kuchukuwa fomu na kurejesha mapema,"alisema Nanyaro.

Mgombea CCM alalamikia rushwa
Katika hatua nyingine, Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM katika Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Elirehema Kaaya ambaye pia ni afisa wa mifugo mkoani Mwanza, amekitaka chama hicho kukemea kampeni za fedha ndani ya chama katika uchaguzi huo.

Kaaya ambaye pia aligombea jimbo hilo katika uchaguzi uliopita na kushindwa katika kura za maoni ndani ya CCM, alisema wakazi wa Arumeru hawahitaji mgombea wa CCM ambaye anapata nafasi hiyo kwa kutumia fedha.

"Arumeru wanataka mtu wa kuwasemea matatizo yao mjengoni (bungeni) na sio mtu anayetumia fedha kupata ubunge na mimi naomba chama kikemee na kukomesha matumizi ya fedha,"alisema Kaaya.

Akizungumzia maombi hayo, Katibu wa CCM Wilaya ya Arumeru Edson Lihweuli alionya mgombea yoyote ambaye atabainika kujihusisha na vitendo vya rushwa au kukiuka taratibu atachukuliwa hatua.

Lihweuli alisema wagombea wote ambao wamechukua fomu, wamekuwa wakipewa taratibu hizo ili kuhakikisha uchaguzi ndani ya chama hicho unakwenda vizuri.

Wakati huohuo, Mkuu wa shule ya Sekondari ya Leguruki inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Mwalimu Athony Msami jana alijitokeza kuchukua fomu na kufanya wagombea wa chama hicho wanaomba ridhaa ya chama kufikia sita.Wengine waliokuwa wamechukuwa fomu ni Sioi Sumari, mtoto wa aliyekuwa mbunge Jeremiah Sumari, William Ndeoya Sarakikya, Elipokea Urio, Elishiria Kaaya na Elirehema Kaaya.

Wakati kada huyo wa CCM akichukua fomu, juzi jioni Mkurugenzi wa kituo cha Mikutano cha Arusha(AICC), Elishiria Kaaya alirejesha fomu na kueleza kuwa anagombea ili kutekeleza ilani kwa kushughulikia matatizo ya wananchi wa Meru.

Kaaya ambaye pia aligombea uchaguzi uliopita na kuangushwa katika kura za maoni na Marehemu Sumari, alisema miongoni mwa mambo ambayo atayasimamia ni kuhakikisha anashirikiana na wananchi kukabiliana na matatizo ya upatikanaji maji, barabara, huduma za afya na masuala ya elimu.

Takukuru yaanza kazi
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Arusha imekutana na wagombea waliojitokeza kuchukua fomu katika uchaguzi huo na kuwaonya kutojihusisha na rushwa pia kuwataka waheshimu sheria za gharama za uchaguzi.

Takukuru pia imetamka kwamba tayari imeshashaanza kupokea malalamiko mbalimbali ya makada wa vyama tofauti vya siasa wilayani humo, kujihusisha na vitendo vya kutoa na kupokea rushwa na kwamba madai hayo yameanza kufanyiwa kazi.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Takukuru mkoani Arusha, Mbengwa Kasumambuto imesema katika kujipanga kukabiliana na rushwa katika uchaguzi huo taasisi hiyo imekutana na wagombea wote wa vyama hivyo kwa lengo la kuwatahadharisha.

“Katika kujipanga na uchaguzi wa Arumeru kwanza tumewaita wagombea ambao wameshajitokeza hadi sasa pamoja na viongozi wa vyama vyao, lengo ni kuwatahadharisha na kuwataka waheshimu sheria ya uchaguzi,”alisema

Source. Mwananchi la leo Febr 17, 2012

MY TAKE: Dr Slaa endelea kuimarisha chama ili 2015 CDM iwe na wabunge wengi zaidi na ikiwezekana kuchukua IKULU> Nasari ana mtaji wa kutosha kulitwaa jimbo hivi sasa kutokana na kura 27,000 za 2010 na pia uimara wa chadema kwa sasa ikilinganishwa na 2010.
 
CDM sasa ni taasisi kubwa, kutaka Dr.Slaa agombee Arumeru ni kuonenyesha kutojiamini kwa ushindani wa Arumeru Mashariki na pia ni dalili mbaya ya kutowaamini wanachama wengine kwamba nao wanaweza kuwa wabunge.
Pili Dr. Slaa tayari ni Presidential and MP material inayoeleweka kwa kazi mzuri, ili kuongeza number ya MP material na future leaders ndani ya chama, iyo nafasi wagombee wananchama wengine na sio yeye. Dr. Slaa abakie na nafasi yake ya sasa ya katibu wa chama na kuwa kama kiranja wa kuwapa experience yake ya mjengoni wabunge wote. Maendeleo ya taasisi yoyote yanakua mazuri iwapo kuna kuwa na mgawanyo mzuri wa madaraka na kuamininia. CDM awana budi kuonesha chama ni zaidi ya Dr.Slaa, vinginevyo CDM itarudi nyuma na kuwa chama cha mtu mmoja kama TLP na Mrema or UDP na John Cheyo.
 
mwaka 2010 tofauti ya sumari na Nasari ilikuwa kura 5,000 tu, kutokana na kutambulika sana kwa chadema kwa sasa, ni wazi itakuwa ushindi wa dhahiri kama jinsi ilivyotoka kwenye 0 hadi 23,000 kule Igunga
 
Duh haya magazeti sasa balaa, mbona wanahangaika na hii kitu?
 
bado naamini wana Arumeru wana mtu wao anayeweza kuwawakilisha, haihitaji mtu kutoka karatu kwenda kuwawakilisha.... slaa needs to help nasari kushinda

slaa kugombea arumeru ni sawa na kusema chadema arumeru haina uwezo wa kushindana na ccm, au kama vile kuletewa mkenya kuombea tanzania kwenye bunge east africa kwamba tulio nao ni weak

i definitely oppose slaa kugombea arumeru, he is bigger than that...
 
katika kosa ambolo limaweza kupoteza sura ya mwanamapinduzi dr slaa ni pamoja na hilo la kugombea arumeru. CCM watakuwa tayari kuhonga kuanzia wapigakura mpaka tume yote ya uchaguzi kudhohofisha heshima ya dr. Slaa na kama hili likitokea basi litakuwa ni kosa kubwa toka Chadema ianzishwe.


sidhani kuna sababu ya dr.slaa kugombea ubunge na kujiongezea majukumu mengi badala ya kujenga chama kama anavyofanya sasa hivi.

Dr.slaa kuwa katibu mkuu na jinsi unavyojenga Chadema ni zaidi ya kuomba ubunge.
 
Back
Top Bottom