Hili bila shaka ni wazo la ccm,wanataka kumpeleka njia waliyompitisha Mzee mrema.kwa mfano akishinda watafanya mbinu na kumfungulia kesi mahakamani na huko basi,kesi inacheleweshwa hadi karibu na uchaguzi mkuu 2015 halafu inaanza kusikilizwa mfululizo,wakiwa wamelikataa ombi lake la kusitisha na kumruhusu ahudhurie katika kampeni za urais.
Jambo amhalo litampotezea muda mwingi na kumdhoofisha kisiasa kwani anakuwa busy na utetezi mahakamani,kama tunavyoona sasa hivi kule arusha kwa mh Godbless lema.
Ambako wanafanya mchezo kama huo,na pale wanaweza chakachua hukumu ikawa ni pamoja na kumzuia kushiriki uchaguzi kwa kipindi fulani mathalani miaka mitano,na hapo lengo lao linakuwa limetimia,
Kumbukeni walijaribu mchezo huu kwa mh slaa katika uchaguzi uliopita kwa kumletea yule mume mtalakiwa wa mama mshumbuzi. Jaribio lililoshindwa lakini likamuathiri kwa kiasi fulani kisaikolojia na pia kitaswira kwa wapiga kura ambao hawakuujua mchezo ule ulivyokuwa.
Cha msingi mzee slaa atumie mvuto alionao kwa sasa kwa kutembelea matawi ya chama na kufanya uhamasishaji na uhai wa chama katika kila kona ya nchi,,badala ya kukaa na kuongelea kutoka dar es salaam tu.
Atumie nafasi hii huku akiwa anafanya utambulisho wa timu ya vijana wabunge wa sasa na hata wale wasiokuwa bungeni,manufaa ya hii inakuwa ni kuwapa nafasi kutambulika na kusikika katika sehemu zote nchini na itamfanya asilazimike kusafiri nchi nzima wakati wa kampeni.kwani anakuwa na kikosi cha kutosha kuifanya kazi hiyo,na yeye ana kwenda sehemu zile zenye kuhitaji nguvu za ziada ambazo ni kambi kongwe za ccm.
Kumbukeni anapambana kumn'goa baba mwenye nyumba na familia yake yote na wakwe,mashemeji,binamu,washenga,makuwadi wa ufisadi na kila aina ya watu waliojikita pale kutuangamiza watanzania kiuchumi.