Pendekezo: SLAA amrithi SUMARI Arumeru!

Pendekezo: SLAA amrithi SUMARI Arumeru!

JF ndiyo desa kuu kwa kipindi hiki,hakuna source kama hii ila mpunguze udaku
 
Kwa lugha uliyoitumia "desa" inaashiria wewe ni mtu wa aina gani " mvaa mlegezo"na sijui nani kakuleta humu na kama ndivyo unasubiri nini kuchapa mwendo kwenu facebook ukauze sura huko labda utalikuta limama lililo kwisha msafirisha mume kwa mungu likuchukuwe mmalizie mabaki.
 
Akigombea itathibitisha dhana ile ile tunayoikataa kuwa hakuna watu wengine wa kuongoza. Moja ya mafanikio ya kiongozi ni kuweza kuandaa watu wengi zaidi kuchukua nafasi yake, hivyo ni bora kuandaa wakazi wa Arumeru kuchukua uongozi wao. Tusijenge mazoea kuwa fulani ndio anaweza. Ni mantiki inaowafanya baadhi ya viongozi wetu wawepo kwenye utawala tangu uhuru hadi leo. Kuna namna nyingi tu za kulitumikia taifa nje ya bunge
Ninakubaliana na wewe kwa 100% mkuu,huo ndio ukweli halisi.
 
Hataki tena ubunge..inamaana bado ana ndoto za urais?
Vipi minjino, unauliza Tigo ya mbwa na mkia umeuona? Tena I forgot, I heard Mama Nagu was contemplating applying for arumeru too, she thinks she can handle two constituencies
 
'danganya toto kula indi bichi' teh teh, usikubali DR. wanajua wewe ni tishio urais 2015

Ntakubaliana na ww akiwa ni rais wa familia yenu na si watanzania , na isitoshe cdm kushika dola nchi hii ndoto, usijidanganye dola inashikwa kwa ww kutumbukiza vikaratasi kwenye saduku

Tanzania daima wapuuzi kweli.
Jana wame ichongea JF kwamba ina mdhalilisha raisi,..kumbe wao wenyewe ndo
wanao pita humu na kutafuta habari za kuweka kwenye gazeti lao.

Huku kung'ata kote kote sijui mnataka nini.
Dr.Slaa alishasema humu humu kwamba hata gombea,...leo mna changanya wasio ingia JF
eti ana shinikizwa agombee,...fanyeni kazi yenu vizuri naona mmesha nunuliwa.
 
Binafsi napendekeza CHADEMA imsimamishe Dr.SLAA kwenye kinyang'anyiro cha ubunge huko Arumeru. Hii itaipa chadema kwanza nafasi kubwa ya kukinyakua kiti hicho kwa kuwa Slaa kwa sasa ni heavy weight politician na pia watanzania wenye uchungu na nchi hii tumekuwa tukiukosa mchango wa Dr pale bungeni.

Wengi tunaukumbuka ujasiri wake akiwa anga zile, kiukweli Mboe anapwaya kwenye nafasi ya kiongozi wa upinzani pale bungeni,waziri mkuu Pinda na serikali yake wanahitaji kuchangamshwa na mtu machachari wa aina ya Slaa,Lema au Tundu!....

Mboe amekua na huruma huruma hivi,sasa slaa kama atafanikiwa kushinda ubunge(nina uhakika atashinda)basi mh.mboe awe muungwana kwa kumpisha bwana Slaa kiti cha kiongozi wa upinzani!hii imekaaje wadau,yote ni katika kuimarisha makali ya bunge.

Salaam Ndugu.

Nimeshawishika kujibu asubuhi hii kwa sababu ya kupenda tu kuonyesha kuwa nina mtazamo tofauti. Mpaka sasa CDM bungeni hawana matatizo yanayoweza kutafsiriwa kwamba kiongozi wao Mh. Mbowe anapwaya. Sidhani kama unawatendea haki watanzania wengine ambao hatuamini hivyo. Ukitaka kujua kwamba wanaenda vizuri chunguzi waliyoyafanikisha kwa mwaka mmoja tangu waingie bungeni CDM kama chama kikuu cha upinzani.

Jingine ni kwamba Dr. Slaa ni kiongozi. Hahitajiki kuingia bungeni ili kuwaongoza wenzake katika kuisimamia serikali. Na hili unaweza kuliona namna ambavyo CDM kimebadilika toka Dr. Slaa awe nje ya Bunge. Kwa kuwa nje ya bunge, Dr. Slaa amepata nafasi nzuri ya kukisimamia chama chake akiwa katibu mkuu mtendaji. Hajaenda likizo kusubiri uchaguzi wa mwaka 2015. Dr, Slaa yuko kazini hata kipindi hiki tunapoandika kwenye huu mtandao. Serikali nayo imeendelea kuwajibika kwa kutazama zaidi yanayosemwa na viongozi wa CDM (tazama taarifa ya Mnyika ya jana kwenye mtandao huu).

Kitu kingine ni kwamba CDM wana hazina kubwa ya vipaji. Mwaka 2010 nilibahatika kutazama mdahalo wa wagombea wa jimbo lililoachwa wazi la Arumeru. Mgombea wa CDM alionyesha uwezo mkubwa wa kujenga hoja; bado tunakumbuka namna wenzake (marehemu sumari hakushiriki) walivyopwaya. Kwa umri ule, kukosa kwake uzoefu, na tofauti ya kura alizopata yeye na marehemu Sumari inaonyesha kijana huyu ni hazina ya CDM. Naomba apewe nafasi japo mimi si mpiga kura wa jimbo hilo. Ninamuombea kwa CDM wamteue na kumuunga mkono.

Kitu kingine naomba tuige kwa mwalimu J.K. Nyerere. Aliacha madaraka ya serikali akaamua kuimarisha Chama. CDM ya sasa inahitaji kuimarishwa kwa haraka sana kabla ya uchaguzi wa 2015. 2015 si mbali. CDM waendelee kujipanga kwa kumtumia vizuri katibu wake mkuu Dr. Slaa. Nafasi iliyokubalika ni sasa.

Kingine naomba mtoa hoja utafakari namna michango ya wabunge wa CDM ilisaidia kunyosha mijadala mingi bungeni. Hoja zao zimekuwa zikibeba watanzania wa kawaida, hali inayowafanya wabunge wa CCM waonekane kama kwamba wao ndiyo wapinzani., kwa kuamua kupinga kila kitu kinachotetewa na wabunge wa CDM. Tuna mfano wa karibu kabisa wa sheria ya mchakato wa katiba mpya. Tumeona namna wabunge wa CCM walivyoamua kuwa wapinzani wa hoja za msingi na kututelekeza sisi wapiga kura wao. Kama si msimamo wa wabunge wa CDM, nchi yote ingekuwa ya wapinzani hivi sasa tunavyoandika humu. Tuendelee kuwapa nafasi basi wabunge hawa wachache tukiamini kwamba Dr. Slaa naye yuko pamoja nasi, hata kama anapigana akiwa nje ya Bunge.
 
Habari yote hii ya ili gazeti ni copy and paste za hoja za hapa hapa jukwaani....
 
uraisi nakumbuka alisema atagombea awamu moja tu,sasa sijui atasema nini tena

watanzania hawakukosea kumchagua Rais Jakaya Kikwete...walijua ana busara...' -Tundu Lissu.......................kumbe hana hizo busara tehetehetehetehhhh
 
uraisi nakumbuka alisema atagombea awamu moja tu,sasa sijui atasema nini tena

Gwandalized! Nikukumbushe system ya CHADEMA ya kumpata mgombea urais sio kama yenu wakina-MAGAMBA! Ninyi Magamba mnaomba kuteuliwa kugombea, CHADEMA mgombea anaombwa. Najua wajua lakini inabidi nikujulishe zaidi! Anayeomba huwa anapenyeza rushwa ili ateuliwe! Anayeombwa huwa hana nafasi ya kutoa rushwa!.....................
 
Dr Slaa akikubali na akashindwa umaarufu wake utazidi kupotea kwani ni mwaka mmoja na miezi nne tu iliyopita alishindwa Uras. Angetulia kwanza kupima upepo
 
Binafsi napendekeza CHADEMA imsimamishe Dr.SLAA kwenye kinyang'anyiro cha ubunge huko Arumeru. Hii itaipa chadema kwanza nafasi kubwa ya kukinyakua kiti hicho kwa kuwa Slaa kwa sasa ni heavy weight politician na pia watanzania wenye uchungu na nchi hii tumekuwa tukiukosa mchango wa Dr pale bungeni.

Wengi tunaukumbuka ujasiri wake akiwa anga zile, kiukweli Mboe anapwaya kwenye nafasi ya kiongozi wa upinzani pale bungeni,waziri mkuu Pinda na serikali yake wanahitaji kuchangamshwa na mtu machachari wa aina ya Slaa,Lema au Tundu!....

Mboe amekua na huruma huruma hivi,sasa slaa kama atafanikiwa kushinda ubunge(nina uhakika atashinda)basi mh.mboe awe muungwana kwa kumpisha bwana Slaa kiti cha kiongozi wa upinzani!hii imekaaje wadau,yote ni katika kuimarisha makali ya bunge.

Salaam Ndugu.

Nimeshawishika kujibu asubuhi hii kwa sababu ya kupenda tu kuonyesha kuwa nina mtazamo tofauti. Mpaka sasa CDM bungeni hawana matatizo yanayoweza kutafsiriwa kwamba kiongozi wao Mh. Mbowe anapwaya. Sidhani kama unawatendea haki watanzania wengine ambao hatuamini hivyo. Ukitaka kujua kwamba wanaenda vizuri chunguzi waliyoyafanikisha kwa mwaka mmoja tangu waingie bungeni CDM kama chama kikuu cha upinzani.

Jingine ni kwamba Dr. Slaa ni kiongozi. Hahitajiki kuingia bungeni ili kuwaongoza wenzake katika kuisimamia serikali. Na hili unaweza kuliona namna ambavyo CDM kimebadilika toka Dr. Slaa awe nje ya Bunge. Kwa kuwa nje ya bunge, Dr. Slaa amepata nafasi nzuri ya kukisimamia chama chake akiwa katibu mkuu mtendaji. Hajaenda likizo kusubiri uchaguzi wa mwaka 2015. Dr, Slaa yuko kazini hata kipindi hiki tunapoandika kwenye huu mtandao. Serikali nayo imeendelea kuwajibika kwa kutazama zaidi yanayosemwa na viongozi wa CDM (tazama taarifa ya Mnyika ya jana kwenye mtandao huu).

Kitu kingine ni kwamba CDM wana hazina kubwa ya vipaji. Mwaka 2010 nilibahatika kutazama mdahalo wa wagombea wa jimbo lililoachwa wazi la Arumeru. Mgombea wa CDM alionyesha uwezo mkubwa wa kujenga hoja; bado tunakumbuka namna wenzake (marehemu sumari hakushiriki) walivyopwaya. Kwa umri ule, kukosa kwake uzoefu, na tofauti ya kura alizopata yeye na marehemu Sumari inaonyesha kijana huyu ni hazina ya CDM. Naomba apewe nafasi japo mimi si mpiga kura wa jimbo hilo. Ninamuombea kwa CDM wamteue na kumuunga mkono.

Kitu kingine naomba tuige kwa mwalimu J.K. Nyerere. Aliacha madaraka ya serikali akaamua kuimarisha Chama. CDM ya sasa inahitaji kuimarishwa kwa haraka sana kabla ya uchaguzi wa 2015. 2015 si mbali. CDM waendelee kujipanga kwa kumtumia vizuri katibu wake mkuu Dr. Slaa. Nafasi iliyokubalika ni sasa.

Kingine naomba mtoa hoja utafakari namna michango ya wabunge wa CDM ilisaidia kunyosha mijadala mingi bungeni. Hoja zao zimekuwa zikibeba watanzania wa kawaida, hali inayowafanya wabunge wa CCM waonekane kama kwamba wao ndiyo wapinzani., kwa kuamua kupinga kila kitu kinachotetewa na wabunge wa CDM. Tuna mfano wa karibu kabisa wa sheria ya mchakato wa katiba mpya. Tumeona namna wabunge wa CCM walivyoamua kuwa wapinzani wa hoja za msingi na kututelekeza sisi wapiga kura wao. Kama si msimamo wa wabunge CDM nchi yote ingekuwa ya wapinzani hivi sasa tunavyoandika humu. Tuendelee kuwapa nafasi basi wabunge hawa wachache tukiamini kwamba Dr. Slaa naye yuko pamoja nasi, hata kama anapigana akiwa nje ya Bunge.
 
Dr Slaa kwa sasa ni jembe la kuimarisha chama wakati huu makamanda wa chadema wenye nguvu wako bungeni muda mwingi. Dr Slaa aendelee kuzunguka nchi nzima.
 
Kumbe hawa Tanzania Daima wanacopy huku JF halafu wanaenda kuuza gazeti lao...hapa inabidi haki miliki izingatiwe!!
Mbona na nyie mnacopy habari toka kwenye magazeti na mnazileta huku!i
 
Tunajadili nini wakati Dr Slaa amekataa kugombea Arumeru? Vyombo vya habari vimemnukuu akisema "hataki tena ubunge isitoshe sio mwenyeji wa Arumeru"
 
Salaam Ndugu.

Nimeshawishika kujibu asubuhi hii kwa sababu ya kupenda tu kuonyesha kuwa nina mtazamo tofauti. Mpaka sasa CDM bungeni hawana matatizo yanayoweza kutafsiriwa kwamba kiongozi wao Mh. Mbowe anapwaya. Sidhani kama unawatendea haki watanzania wengine ambao hatuamini hivyo. Ukitaka kujua kwamba wanaenda vizuri chunguzi waliyoyafanikisha kwa mwaka mmoja tangu waingie bungeni CDM kama chama kikuu cha upinzani.

Jingine ni kwamba Dr. Slaa ni kiongozi. Hahitajiki kuingia bungeni ili kuwaongoza wenzake katika kuisimamia serikali. Na hili unaweza kuliona namna ambavyo CDM kimebadilika toka Dr. Slaa awe nje ya Bunge. Kwa kuwa nje ya bunge, Dr. Slaa amepata nafasi nzuri ya kukisimamia chama chake akiwa katibu mkuu mtendaji. Hajaenda likizo kusubiri uchaguzi wa mwaka 2015. Dr, Slaa yuko kazini hata kipindi hiki tunapoandika kwenye huu mtandao. Serikali nayo imeendelea kuwajibika kwa kutazama zaidi yanayosemwa na viongozi wa CDM (tazama taarifa ya Mnyika ya jana kwenye mtandao huu).

Kitu kingine ni kwamba CDM wana hazina kubwa ya vipaji. Mwaka 2010 nilibahatika kutazama mdahalo wa wagombea wa jimbo lililoachwa wazi la Arumeru. Mgombea wa CDM alionyesha uwezo mkubwa wa kujenga hoja; bado tunakumbuka namna wenzake (marehemu sumari hakushiriki) walivyopwaya. Kwa umri ule, kukosa kwake uzoefu, na tofauti ya kura alizopata yeye na marehemu Sumari inaonyesha kijana huyu ni hazina ya CDM. Naomba apewe nafasi japo mimi si mpiga kura wa jimbo hilo. Ninamuombea kwa CDM wamteue na kumuunga mkono.

Kitu kingine naomba tuige kwa mwalimu J.K. Nyerere. Aliacha madaraka ya serikali akaamua kuimarisha Chama. CDM ya sasa inahitaji kuimarishwa kwa haraka sana kabla ya uchaguzi wa 2015. 2015 si mbali. CDM waendelee kujipanga kwa kumtumia vizuri katibu wake mkuu Dr. Slaa. Nafasi iliyokubalika ni sasa.

Kingine naomba mtoa hoja utafakari namna michango ya wabunge wa CDM ilisaidia kunyosha mijadala mingi bungeni. Hoja zao zimekuwa zikibeba watanzania wa kawaida, hali inayowafanya wabunge wa CCM waonekane kama kwamba wao ndiyo wapinzani., kwa kuamua kupinga kila kitu kinachotetewa na wabunge wa CDM. Tuna mfano wa karibu kabisa wa sheria ya mchakato wa katiba mpya. Tumeona namna wabunge wa CCM walivyoamua kuwa wapinzani wa hoja za msingi na kututelekeza sisi wapiga kura wao. Kama si msimamo wa wabunge CDM nchi yote ingekuwa ya wapinzani hivi sasa tunavyoandika humu. Tuendelee kuwapa nafasi basi wabunge hawa wachache tukiamini kwamba Dr. Slaa naye yuko pamoja nasi, hata kama anapigana akiwa nje ya Bunge.

Ok nimekuelewa,lakini nina swali kidogo tu,unakizungumziaje kitendo cha kiongozi wa upinzani bungeni pamoja na wabunge wake kumuachia zitto pekee suala la kupinga na kususia posho ya kukaa kitako bungeni ambao ni mzigo kwetu sisi tax payers?unaona kiongozi wa upinzani bungeni yuko sahihi kupanga foleni ya kugombea posho hiyo haramu?
 
Back
Top Bottom