Pendekezo: SLAA amrithi SUMARI Arumeru!

Pendekezo: SLAA amrithi SUMARI Arumeru!

Dr for Arumeru?hapana,imarisha chama Dr kwa ajili ya kuchukua dola 2015,ubunge si hadhi yake tena!kijana Nasari anatosha kutwaa jimbo ilo,hiyo haina shaka!viva cdm
 
hatuhitaji kuua mende kwa nyundo maana tutaumia sisi.....dk endelea na majukumu ya kichama
 

Chadema inaelekea kumeza hii ndoano waliyotegewa na CCM.
 
mwaka 2010 tofauti ya sumari na Nasari ilikuwa kura 5,000 tu, kutokana na kutambulika sana kwa chadema kwa sasa, ni wazi itakuwa ushindi wa dhahiri kama jinsi ilivyotoka kwenye 0 hadi 23,000 kule Igunga
msisahau kuwa cuf nao walikua na mtaji igunga kilichowapata hawatakaa waahau na nyie cdm lazima mtambue ya kwamba uchaguzi huu wa arumeru unaweza kuwaletea matokeo kama ya cuf Igunga
 
Dr Slaa anaakili kuliko hao waandishi wote wa hayo magazeti pamoja na wanaowatuma so i believe hawezi kugombea.
 
dr slaa jenga chama .arumeru sio saizi yako ,wewe ni raisi wetu mtarajiwa .mungu ibariki chadema mungu ibariki tanzania
 
Nasari aliyewahi kuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso) kati ya 2008 na 2009 alipohitimu shahada ya Sayansi ya Jamii katika masuala ya utengenezaji Sera na Utawala, alisema ana imani Chadema kitashinda Arumeru.

.

kuna upotoshaji hapo. Nassari Joshua, alikuwa mwanaharakati makini lakini hakuwa kuwa waziri mkuu wa DARUSO. Ninachokumbuka, kuna kipindi hali ilikuwa tete sana UDSM baada ya wanachuo kuwagomea viongozi waliingizwa kwa hila na Mkandala, tulikaa kwa wiki moja bila kuwa na uongozi DARUSO, na hivyo yeye na kijana aliyejulikana kwa jina la SIDE, walijitangazia uongozi na kuendesha harakati za chuo kwa siku tatu. Walifanya kitu ambacho kilikuwa hakijifanyika pale udsm, na tuliwaunga mkono mpaka uchaguzi ulipofanyika upya
 
nibora kukosa jimbo kulko kumuweka DR yani slaaaa 2015 URAISIIIIWAKO
 
bado naamini wana Arumeru wana mtu wao anayeweza kuwawakilisha, haihitaji mtu kutoka karatu kwenda kuwawakilisha.... slaa needs to help nasari kushinda

slaa kugombea arumeru ni sawa na kusema chadema arumeru haina uwezo wa kushindana na ccm, au kama vile kuletewa mkenya kuombea tanzania kwenye bunge east africa kwamba tulio nao ni weak

i definitely oppose slaa kugombea arumeru, he is bigger than that...
Huu mpango umepangwa na CCM kwa malengo maalum kummaliza Dr Slaa! Wamekuwa wapole baada ya kuona Dr Slaa hata chembe ya harufu ya ubunge hataki.KIM KARDASH nasoma comments zako nyingi umekaa ki double agent! Endelea kubadili ID zako lakini huwezi kubadili mtindo wa uandishi wako!
 
mtawachanganya wameru, leo awe mbunge af baade kidogo awe rais, anyway wanaweza kufanya ili Arumeru nao liwe jmbo lililowahi kutoa rais ktk historia!sawa tu bwana kila la kheri
 
msisahau kuwa cuf nao walikua na mtaji igunga kilichowapata hawatakaa waahau na nyie cdm lazima mtambue ya kwamba uchaguzi huu wa arumeru unaweza kuwaletea matokeo kama ya cuf Igunga

kulinganisha mtaji wa CUF na CHADEMA ni kujisumbua, nini mtaji, CUF hata kama walikuwa washindi walishajizika kitambo, CHADEMA hata kama wakiweka jiwe na Cuf asimame ustaadh hawatapata kitu
 
Dr aendeleee na majukumu ya kuhamasiha n a kuwaelemisha wananchi umuhimu wa kuikana CCM na ubora wa CDM...
Kama ni ubunge kwa sasa inatosha aliisha fanya kazi yake na kila MTZ anamjua, na sasa bungeni kuna visu vya bucha ka Tundu Lissu, Wenje, Lema , Msigwa , Mdee n.k wao ni mara 40 zaidi ya wabunge wa magamba!
 
Jamani kwanini kumzungumzia? Yeye mwenyewe alijibu kwenye gazeti la jana lililoanza kutoa habari hizo, tena kwenye taarifa ya habari ya Mlimani Tv akatolea ufafanuzi. Kwa ufupi ''HATAKI'' mbona haya magazeti yanamlazimisha?
 
Back
Top Bottom