Pendekezo: SLAA amrithi SUMARI Arumeru!

Wapendwa wa Chadema,
Mimi naomba Dr Slaa awanie ubunge Arumeru kusudi arudi Bungeni kuweka nguvu mpya

kama chadema ina mgombea makini Arumeru haina haja ya kumnyang'anya fursa hii kwa sababu ya Dr Slaa. Tumeshuhudia baadhi ya majimbo yanaingia kwenye mgogoro kwa sababu ya kupingana na uteuzi wa vikao vya jimbo na kuleta jina kutoka makao makuu ya chama kwa ajili ya kugombea.

Tuwaache wananchi wa Arumeru waamue hatima yao.
 
Keshachoka kisiasa huyu..
Kwa sasa tunahitaji dam mpya za zenye nguvu bungeni na kwenye ulingo wa siasa!
Damu mpya kama huyu....

WasiraSteve(1).jpg
 
Mnahitaji nyie akina nani? wavua gamba bila shaka mmechoka na ndio maana hapa tunazungumzia mambo ya chadema lakini vidudu watu hamchoki kujiingiza kwenye mambo yasiyowahusu.
mtoa mada ameweka wazi kuwa hii ni kwa wanachadema tu, inanipa wasiwasi kuwa unaweza kuhudhuria kitchen party wakati ni kwa viburudisho tu
Hii sredi wapi imeandikwa ni ya wanamagwanda?
Kama mnataka huyo mzee akaangukie pua mpelekeni Arumeru. Na sera zake za ufisadi tu kichwani, sijui atazungumza nini Arumeru!!
 
Achilia mbali hilo, hata Ikulu pia anaipika, kasi, uwajibikaji. Bila yeye unadhani CCM wangevuana magamba, wangeridhia kuandika katiba mpya? wangekubali mabadiliko ya sheria mbovu ya kuandika katiba mpya.

Mi naona mleta mada labda angeshauri Mkapa arudi Ikulu 2015 kupitia CCM B.
Mkuu hata posho wabunge wametemeshwa!!!!!

 
alishinda urais sembuse ubungeee, najua hata wewe una uhakika atashinda, najua hamuombolezi kumtakia Sumari maisha mema, mnaomboleza kupoteza jimbo, nikupe matokeo?

We hayo matokeo kaa nayo tu hayawezi kusaidia chochote, wenzako wameshamtambua JK ndo Rais...
 
Hi thread imeanzishwa, na inashabikiwa, na maadui wa CDM. Wanataka Slaa aingie kwenye shindano la Arumeru ili wammalize kwa kutumia Tume ya Uchanguzi. Wanajua wakimmaliza Arumeru, hataweza kufurukuta tena 2015 kwenye Urais au hata Ubunge.

Nadhani Slaa ajikite kwenye mambo ya Katiba Mpya zaidi. Kwa sasa, CDM walio bungeni wanamwakilisha vya kutosha. Kwanza akirudi bungeni na kuanza kuongea kama akina Lissu na Mnyika atapotenza muonekano wake wa ki-Rais.
 
Wapendwa wa Chadema,
Mimi naomba Dr Slaa awanie ubunge Arumeru kusudi arudi Bungeni kuweka nguvu mpya

Dr Slaa ana kazi ya kuijenga Taifa hili ingawa watu wengi wanataka awe mbunge lakini mimi naona ni vema abakie kuwa kiongozi wa kitaifa maana CDM sasa ni chama kikubwa na kinahitaji viongozi wakuu kama secretariat yake iwe very strong na iwe busy na kazi za Chama zaidi kuliko za kibunge.


Nawasilisha....
 
unamaana gani kuchoka kisiasa?
Nikuwekee picha za wabunge wa ccm waliochoka bongo zao kazi kulalalala.
Unaelewa maana ya kuchoka kisiasa? Unaelewa maana ya kuishiwa sera?
Jaribu kumfuatilia slaa utaelewa ninachoomanisha!
 
Wakuu mleta hoja si mtu mwema kwa Chadema ana nia ya kuidhoofisha Chadema, hivi unadhani Meru kuna mchanganyiko wa makabila kiasi gani hata wamchague mtu ambaye siyo wa kabila lao? Unafikiri leo Mzee Mwinyi au Mkapa pamoja na kuwahi kuwa rais wakigombea pale Meru watachaguliwa? Na pia watanzania tumechoka na watu ambao hawana makazi ya kudumu katika maeneo wanayogombea na je wanaishi katika hilo? Mtoa hoja nia yako si nzuri, hivyo kajipange upya.
 
Keshachoka kisiasa huyu..
Kwa sasa tunahitaji dam mpya za zenye nguvu bungeni na kwenye ulingo wa siasa!
CCM mngetuonyesha njia mbona kwenu kuna vibabu hata meno havina bado vipo kwenye safu yenu???au ndo kamati ya ufundi??
 
Wakuu mleta hoja si mtu mwema kwa Chadema ana nia ya kuidhoofisha Chadema, hivi unadhani Meru kuna mchanganyiko wa makabila kiasi gani hata wamchague mtu ambaye siyo wa kabila lao? Unafikiri leo Mzee Mwinyi au Mkapa pamoja na kuwahi kuwa rais wakigombea pale Meru watachaguliwa? Na pia watanzania tumechoka na watu ambao hawana makazi ya kudumu katika maeneo wanayogombea na je wanaishi katika hilo? Mtoa hoja nia yako si nzuri, hivyo kajipange upya.

Usihukumu, honestly sikuwa na nia mbaya. Ni mawazo, kama wewe ulivyosema kuwa itakuwa vigumu kupata kwa vile sio mwemyeji wa huko. This is a point anyway. Ndio tunapeana mawazo hivyo.
 
mimi bado naulilia mchango wa dr slaa bungeni,lile jembe,hawa wapinzani wa sasa ukimuacha zitto ni wachumia tumbo tu,watu ni wabunge posho akiwemo kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni,jembe slaa arudi bungeni akamuongezeee nguvu mpiganaji zitto kabwe.
 
Kwa Bunge hili la Bibi Kiroboto haina haja ya kumpeleka Rais wetu wa mioyoni kusikiliza kinachoitwa busara za kiti, ambazo ziko juu hata ya kanuni za bunge. Dr aendelee kukijenga chama na kuongoza nchi kwa remote control kutokana na kuwa na serikali dhaifu. Akina Lissu wanamtosha kabisa bi Kiroboto.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom