Nimekua kimya nikijaribu kufuatilia hoja zenu waungwana,mnaodai ukatibu mkuu wa slaa ni mkubwa kuliko ubunge,hoja yenu dhaifu sana,umaarufu wa slaa hautokani na ukatibu mkuu wake bali ulitokana na ubunge sasa kwa nini asirudi bungeni akamalizie kazi aliyoianzisha?au mnataka asubiri nafasi ya ubunge wa kuteuliwa na rais mwaka 2013 mwishoni kufuatia muafaka wa haya mazungumzo ya upenuni kati ya jk na mbowe?kama hamjui ndio tunakoelekea!
Na nyie mnaodai eti slaa ni rais mnamdanganya pamoja na kujidanganya nyie!na pia mnaosema eti sijui ataibiwa kura na kufirisika kisiasa pia ni uongo!hivi kura huwa zinaibiwaje?ndugu zanguni amkeni msikubali kudanganywa na wanasiasa,tatizo wanasiasa wetu wa africa huwa hawasemi ukweli kwa kuogopa kuwajibika kutokana na kushindwa chaguzi ndio huwa wanakuja na kisingizio cha kuibiwa kura wakishindwa,hivi hamjiulizi kama wizi wa kura upo kwanini cuf inairesa ccm pemba?au kwanini Ndesambura anaitesa kila wakati ccm moshi mjini?au kwanini Mzee Said Arfi makamu mwenyekiti wa cdm amekua kwa muda mrefu hata wakati slaa hajulikani amekua akiitesa ccm huko mpanda kwake?au zitto kwa nini anitesa ccm?Huwezi kuiba kura,huwa mnakua mmeshindwa tu,msidanganyike na watu kujaa kwenye mikutano yenu ya kampeni au hapa jf watu wengi kuonekana wanaipenda chadema,wengi sio wapiga kura!