Mkuu post zako unataja kuwa CDM imeshindwa kihalali na mifano yako lukuki lakini hapo hapo huamini katika kushindwa
Mkuu watu makini hawafanyi mambo kwasababu fulani alifanya akaweza, unatakiwa kufanya tathmini yakinifu na kuzingatia factor mbali mbali, kila jimbo lina tabia zake,
Ok umetoa mfano wa Tarime nikweli yule bwana alimrithi vizuri Chacha lakini unajua sababu za kuja kupoteza jimbo kwa CCM uchaguzi mkuu, simply ni kwa sababu CDM walisimamisha mtu kwa matakwa ya chama.
Unapozungumzia swala la elimu hivi elimu gani unazungumzia hiza za Havard za kina Chenge au? hivi unaweza kulinganisha michango ya wasomi wangapi bungeni ukaweza kulinganisha na michango ya watu kama akina Kafulila na Mnyika wasio na degree.
Sitaki kuamini kama mapendekezo yako yote hayo ya Dr Slaa dhidi ya Mbowe kigezo ni elimu. you better think than that dude
Kumuita Joshua mbele ya chama si kuita wapigara kura mbele ya chama, ndio yale yale ya kusimamisha mgombea kwa matakwa ya chama badala ya wapiga kura.
Nimekuuliza mambo ya msingi lakini umekimbila mepesi kwa sababu tu eti Mrema aliweza temeke basi Slaa ataweza Arumeru mashariki, nyakati zimebadila sana mkuu watu wamepata mwamko na uelewa mkubwa wa nini wanataka wao, Temeke leo hii haina mzawa ni full wahamiaji toka bara unapo zungumzia Arumeru yaani kule ni wenyewe watupu mkuu, unahitaji uhakika wa kutosha kama watakubali mgeni kuja kuwawakilisha na si kwasababu Mrema sijui alifanya nini, NOPE
Mwisho kwenye red, maandiko yangu yamejaribu sana kuangalia factor hiyo, tuna maanagani tunaposema "wananchi wakitaka utashinda tu" je ni kwa kuwapelekea mtu au kwa wao kuamua mtu wampedae na kuona ni mwenzao
Rejea bandiko langu la kwanza pitia risk za Dr kugombea ndio utajua je wakati unakwenda kwenye uchaguzi wananchi wanataka?