Pendekezo: Prof. Lipumba awe mgombea wa upinzani Igunga

Pendekezo: Prof. Lipumba awe mgombea wa upinzani Igunga

NImesema ameombwa kugombea ubunge wa Igunga. Wewe leta hoja za Igunga, siyo kumchafua mwenzako.
 
Taarifa nilizozipata sasa hivi, yule mwandishi wa habari mashuhuri nchini, Bw. Said Kubenea anatarajiwa kugombea ubunge katika jimbo la Igunga lililowachwa wazi na mbaya wake Rostam Aziz. Tayari mazungumzo kati ya Kubenea ambaye mmoja wa wazazi wake wanatoka Igunga yamefanyika naye inasemekana amekubali ofa hiyo. Anatarajiwa kugombea kupitia chama cha magamba. Mwingine anayetajwa kutaka kujitosa jimboni Igunga, ni Hussen Bashe na Peter Kafumo.
Wewe unaweza kuwa mgonjwa fanya mpango ukapime Malaria ndugu.
 
Nakwambia anagombea. Jana alikuwa na kikao kirefu na Membe na Msekwa. CCM wanaona njia pekee ya kushinda jimbo la Igunga ni kumuweka Kubenea. Wamemhakikishia vikao vya chama vitampitisha. Lakini mkakati mzima unaonekana kutaka kumyamazisha yeye na gazeti lake. Wanaamini kuwa akijitosa katika mbio za ubunge Igunga, basi hataweza tena kuwachapa.

WanaJF mpeni Kubenea HAKI YAKE YA KUCHAGUA NA KUCHAGULIWA KUPITIA CHAMA ANACHOPENDA YEYE. Jamani huu ndio utamu wa SIASA,hiki si cha kushangaa kubenea ni mpiganaji muacheni, sio kila Mwana CCM basi hapaswi kuwa Mwanaharakati na mpiganaji wa TAIFA letu.NOOO SIO SAWA HATA KIDOGO.Mpeni haki yake ya KUCHAGUA NA KUCHAGULIWA.

Nimekuwa napinga sana hatua na juhudi za CCM za kuwafanya Watanzania wengine Kama wageni ndani ya TAIFA lao kwa kuwa si WanaCCM.Ili uwe na mchango wa kulitumikia TAIFA ni Lazima uwe MWANACCM.Hapana huo si UTU,ni UONEVU hivyo kupatikana kwa watu kama KUBENEA ndio mwanzo wa mageuzi.

Kwa kuwa dhamila yake ni mageuzi,akifika uko asitumie nafasi hiyo kwa faida ya wengi basi nae ATASTAHIKI LAWAMA za kutumwa na wanfamilia chakula wakati wa njaa kisha baada ya kupata chakula cha wanajamii anapotea nacho anakojua yeye,na kuwaacha wanajamii wakiendelea kuteseka na njaa.TUNAITAJI MCHANGO WA KUBENEA BUNGENI ACHENI AENDE SIO LAZIMA APITIE CDM HATA CCM NACHO NI CHAMA.JIBU LA TATIZO SI KUKIMBIA TATIZO BALI NI KUKABILIANA NALO.

HONGERA KUBENEA KAMA NI KWELI.
 
kwani kubenea ni muirani??hawezi chaguliwa na ccm APENDE ASIPENDE CCM IGUNGA INAONGOZWA NA NGOZI NYEUPE BWANA,LABDA AINGIE CDM

Hao wenye ngozi nyeupe ndio wanakuongoza sasa hivi. Nambie, Jakaya mweusi?
 
Hapa naona vitu viwili: Mwanahalisi na Ubunge. Sasa Kubenea anatakiwa achague moja ama Mwanahalisi liendelee kunawiri au Ubunge lakini hawezi kukamata vyote kwa pamoja. Angeniuliza, ningemshauri Mwanahalisi!.
 
sitashangaa pamoja na hali mbaya ya kimaisha iliyoko Igunga bado wanaweza wakachagua magamba tena akiwa ana ka ushombeshombe, mburushi, au muasia atapita kirahisi saaana si unajua wanyamwezi tena washazoea mateso toka enzi za kina Tippu tippu, na ule msemo MZIGO MZITO MPE MNYAMWEZI una ukweli kabisa

Pukudu hasira zako mbaya, badala ya kusaidia jambo wewe unatia moto, mimi nafikiri tunaweza kupata mbuge mzuri wa Igunga kutoka nje ya CCM, lakini tatizo kubwa hatujui huyu bwana Rostam kaachia ngazi akiwa na fikra gani kwa mtu ambaye atamrithi na je atampigia tafu kiasi gani maana jamaaa ana pesa chafu kuliko mimi na wewe na yule na hapa kumbuka alivyoweza kununua watu wa kulia kwenye hotuba yake ya kujivua gamba, pia endapo atakuwa anataka jimbo liende upinzani anaweza na atakuwa kasaidia sana kitu ambacho kwa tabia maburushi wengi hupenda kukionyesha kuwa wana uwezo wa kufanya chochote wakati wowote, pili wasomi wengi wa Igunga ambao ni wazuri kugombea na wanauzika kwa wanainchi ni wafanyakazi wa serikali (CCM) hivyo basi nashawishika kuwa ni vigumu kwao (ingawa wanaweza) kuchukua likizo ya kugombea ubunge kwa chama cha upinzani kwani kutenda hivyo kunatia wasiwasi wa hatma yao huko mbeleni,

Nafikiria sana na najaribu kuamini kuwa endapo yule mgombea wa CUF aliyeshindwa na RA uchaguzi uliopita basi angesimamishwa yeye na nguvu ya umma ikaelekezwa kwake ninaamini anaweza kushinda, au CCM basi watuletee kifaa kama Lembeli wa Kahama na kamwe si huyo Kafumu ambaye anajulikana ni dalali wa mafisadi aliyehusika kwa undani kabisa kutengeneza mikataba ya kifisadi ya madini,na huyo mwalimu Malembeka ukweli si mtu wa Igunga na kumchagua yeye ni sawa na kumchagua RA

Jambo la mwisho na muhimu kabisa safari hii na iwe vyovyote vile "Igunga ni kwa wana Igunga" hao waburushi, washombe, na akina Tippu Tippu hawana lao ila wakitaka wanakaribishwa uwanjani watumie demokrasia yao
 
Mh Saidi S Kubenea Mbunge mteule wa Jimbo la Igunga CHADEMA
Hapo ndio itaeleweka lakini sio Kubenea kupitia chama cha magamba..labda kubenea mwingine sio huyu mhariri wa mwanahalisi kumbuka walishamjeruhi mpaka kaenda kuponea India sasa iweje leo wamwone anafaa kugombea kupitia magamba?
 
Hakuna litakalo shindikana japo ni pigo kwa wanaharakati kwa mtu kama kubenea kuingia rasmi katika uongozi kwa tiketi ya magamba kwani ni dhahiri atabanwa mbavu na hatakuwa na uwezo wa kuendelea kufichua mabovu yao kama ilivyokuwa awali.
 
huo uchaguzi NEC wataubania usifanyike sasa hivi mpaka wapate mtu ambaye wana uhakika atashinda from ruling party
nakumbuka kulikuwa na sheria inayotoa kikomo cha muda ambao jimbo linaweza kukaa bila mwakilishi, nahivyo uchaguzi uwe umefanyika katika kipindi hicho... ila magamba kuna wakati waliwahi kuibadilisha ili "kuwakomoa" wale wabunge wa cuf waliogomeaga bunge nafikiri msimu wa 2000-2005
 
nitasikitika sana kama kubenea ataenda Igunga

Hivi hakuna wanyamwezi wazuri hadi aende huyu?? and we expect maendeleo ya kweli kabisaaa?? barabara nzuri, umeme, elimu, afya, teknohama na kilimo from kubenea??? mtu ambaye for the past 36 months all his mind was focused on Lowassa basi??

kweli watanzania ni mbayuwayu... we need a serius Tananian from Igunga mwenye uchungu na weledi wa kujua tanzania inataka ni na si mtu ambaye kila akiamka anaanza na Lowassa then bismillah

hapan!!!

kwa hilo, God forbid
 
Back
Top Bottom