Pendekezo: Prof. Lipumba awe mgombea wa upinzani Igunga

Malaria Sugu

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
2,653
264
CDM ilimshinikiza DK Slaa kuwa mgombea urais japo mwenyewe alikuwa hataki. Tumeona faida yake kuingiza wabunge wengi upinzani.

Kwa hivyo kwanini tusichukue nafasi ile kumshinikiza Mh Lipumba ili agombee ubunge Jimbo la Igunga:

  • Ni mzaliwa wa Tabora
  • Ni mwenyekiti wa Chama cha CUF ili kuongeza nguvu za upinzani akisaidiana na kina Mbowe, Lissu na wengine
  • Itaijenga Cuf kisiasa na kujenga Upinzani wenye nguvu bungeni
  • CDM haina nguvu sana kulinganisha na CUF kwa kuwa lipumba ndipo anapotoka.
 
Cdm Ilimshindikiza DK Slaa kuwa mgombea urais japo mwenyewe alikuwa hataki. tumeona faida yake kuingiza wabunge wengi upinzani.
Kwa hivyo kwanini tusichukue nafasi ile kumshindikiza Mh Lipumba ili agombee ubunge Jimbo la Igunga:
ni mzaliwa wa Tabora.
ni mwenyekiti wa Chama cha Cuf ili kuongeza nguvu za upinzani akisaidiana na Kichwa Mbowe.
Lissu na wengine.
Itaijenga Cuf kisiasa na kujenga Upinzani wenye nguvu bungeni
CDM haina nguvu sana kulinganisha na CUF kwa kuwa lipumba ndipo anapotoka.

Nakubaliana na wewe lakini hapo kwenye red umechemka, CUF ina nguvu zaidi Tabora mjini
na vijijini lakini nje ya hapo (Nzega, Igunga, Urambo, BUkene) hakuna kitu
 
hapo hata mimi nakubaliana na wewe, wangeungana CUF, NCCR na CDM wamsimamishe mgombea mmoja tu prof Lipumba.
 
Wote mnaounga mkono wazo hili ni CCM.

Sihitaji kwenda Chuo kujua uhusiano wa CUF na CCM!!!

Endapo CUF wangekua wapinzani wa CCM wazo lako ni zuri, Ila kwasasa CUF ni wapinzani wa CDM. kwahiyo unalolisema halitawezekana kamwe.
 
Hao CUF ni lini wamekuwa tayari kuwasaidia CHADEMA? na ni lini wanashirikiana na CHADEMA? tusijisahau mambo wanayowafanyia CHADEMA Bungeni
 
Hao CUF ni lini wamekuwa tayari kuwasaidia CHADEMA? na ni lini wanashirikiana na CHADEMA? tusijisahau mambo wanayowafanyia CHADEMA Bungeni

Mkuu,

Tukiweka mbali ushabiki wa Chama tunahitaji mtu kama Lipumba bungeni. Hali ya uchumi wa nchi unaenda kombo na walioko bungeni sio wajuzi wa uchumi waliobobea Lipumba anaweza kuongeza nguvu bungeni kuzidi kuikosoa serikali iliyo madarakani.
 
Nimeona Zitto ameandika kwenye twitter ameandika cdm wanajiandaa kuchukua jimbo la Igunga, nadhani mikakati itakayowekwa na cdm lazima kieleweke. Lipumba hatumuhitaji
 
CDM ilimshinikiza DK Slaa kuwa mgombea urais japo mwenyewe alikuwa hataki. Tumeona faida yake kuingiza wabunge wengi upinzani.

Kwa hivyo kwanini tusichukue nafasi ile kumshinikiza Mh Lipumba ili agombee ubunge Jimbo la Igunga:
  • Ni mzaliwa wa Tabora
  • Ni mwenyekiti wa Chama cha CUF ili kuongeza nguvu za upinzani akisaidiana na kina Mbowe, Lissu na wengine
  • Itaijenga Cuf kisiasa na kujenga Upinzani wenye nguvu bungeni
  • CDM haina nguvu sana kulinganisha na CUF kwa kuwa lipumba ndipo anapotoka.

Anasubiria urais wa Tanzania, 2015
 
Tukitazama mbali...LIPUMBA ASIMAME KWA UBUNGE IGUNGA.
Iwapo tutaacha itikadi za vyama, Lipumba nampa credits na pale atachukua.
 
Nimeona Zitto ameandika kwenye twitter ameandika cdm wanajiandaa kuchukua jimbo la Igunga, nadhani mikakati itakayowekwa na cdm lazima kieleweke. Lipumba hatumuhitaji

Shibuda ana ushahidi wa mazungumzo ya CDM na Rostam kuhusu kukabidhiana hilo jimbo, hapo Zitto anasafisha njia ya kwa Shibuda kuibomoa CDM kesho.
 
Mkuu,

Tukiweka mbali ushabiki wa Chama tunahitaji mtu kama Lipumba bungeni. Hali ya uchumi wa nchi unaenda kombo na walioko bungeni sio wajuzi wa uchumi waliobobea Lipumba anaweza kuongeza nguvu bungeni kuzidi kuikosoa serikali iliyo madarakani.
Msimshushie hadhi Prof. yeye si material ya ubunge ni mgombea urais wa kudumu wa CUF.
 
Yeye mwenyewe anaweza kukubali???
Yule ndoto zake ni kuwa rais tu!!!
 
Back
Top Bottom