pukudu hasira zako mbaya, badala ya kusaidia jambo wewe unatia moto, mimi nafikiri tunaweza kupata mbuge mzuri wa igunga kutoka nje ya ccm, lakini tatizo kubwa hatujui huyu bwana rostam kaachia ngazi akiwa na fikra gani kwa mtu ambaye atamrithi na je atampigia tafu kiasi gani maana jamaaa ana pesa chafu kuliko mimi na wewe na yule na hapa kumbuka alivyoweza kununua watu wa kulia kwenye hotuba yake ya kujivua gamba, pia endapo atakuwa anataka jimbo liende upinzani anaweza na atakuwa kasaidia sana kitu ambacho kwa tabia maburushi wengi hupenda kukionyesha kuwa wana uwezo wa kufanya chochote wakati wowote, pili wasomi wengi wa igunga ambao ni wazuri kugombea na wanauzika kwa wanainchi ni wafanyakazi wa serikali (ccm) hivyo basi nashawishika kuwa ni vigumu kwao (ingawa wanaweza) kuchukua likizo ya kugombea ubunge kwa chama cha upinzani kwani kutenda hivyo kunatia wasiwasi wa hatma yao huko mbeleni,
nafikiria sana na najaribu kuamini kuwa endapo yule mgombea wa cuf aliyeshindwa na ra uchaguzi uliopita basi angesimamishwa yeye na nguvu ya umma ikaelekezwa kwake ninaamini anaweza kushinda, au ccm basi watuletee kifaa kama lembeli wa kahama na kamwe si huyo kafumu ambaye anajulikana ni dalali wa mafisadi aliyehusika kwa undani kabisa kutengeneza mikataba ya kifisadi ya madini,na huyo mwalimu malembeka ukweli si mtu wa igunga na kumchagua yeye ni sawa na kumchagua ra
jambo la mwisho na muhimu kabisa safari hii na iwe vyovyote vile "igunga ni kwa wana igunga" hao waburushi, washombe, na akina tippu tippu hawana lao ila wakitaka wanakaribishwa uwanjani watumie demokrasia yao