maoniyangu
Member
- Jul 9, 2011
- 53
- 4
watu wa igunga ni wagumu sidhani kama upinzani utaweza kuchukua kirahisi
Wote mnaounga mkono wazo hili ni CCM.
Sihitaji kwenda Chuo kujua uhusiano wa CUF na CCM!!!
Endapo CUF wangekua wapinzani wa CCM wazo lako ni zuri, Ila kwasasa CUF ni wapinzani wa CDM. kwahiyo unalolisema halitawezekana kamwe.
Umesomeka sana mkuu hata mimi nawashangaa wanaotaka muungano wakati huu
nafikiri hata uongozi wa Chadema utapuuza, kumbuka CUF walivyokuwa wanabeza maandamano
bora kujulikana umeshindwa kwa jitihada zako kuliko kushinda kwa muungano wa kinafiki.
kweli mkuu hata mi nawashangaa hawa wanaopendekeza! Maendeleo na mabadiliko yataletwa na vijana sio hawa wakongwe wanaojiita eti wazoefu kumbe njaa tu. Mfano mzuri ni huyu six, watu walimwamini kumbe hakuna kitu ni unafiki tuDamu mpya zinahitajika, kwani Igunga hakuna watu wengine??? watu tumechoka kusikia haya majina ya wakongwe
Ondoa magamba katika list yako ya vyama maana hamna mwadilifu.Tatizo lawatanzania ni uvyama, tutachagua mtu muadilifu jamani,, CDM, UDP, CCM, NCCR, CUP vyote sawa, we need watu wa adilifu na watiifu kwa watu wao,
CDM ilimshinikiza DK Slaa kuwa mgombea urais japo mwenyewe alikuwa hataki. Tumeona faida yake kuingiza wabunge wengi upinzani.
Kwa hivyo kwanini tusichukue nafasi ile kumshinikiza Mh Lipumba ili agombee ubunge Jimbo la Igunga:
- Ni mzaliwa wa Tabora
- Ni mwenyekiti wa Chama cha CUF ili kuongeza nguvu za upinzani akisaidiana na kina Mbowe, Lissu na wengine
- Itaijenga Cuf kisiasa na kujenga Upinzani wenye nguvu bungeni
- CDM haina nguvu sana kulinganisha na CUF kwa kuwa lipumba ndipo anapotoka.
tangu mfumo wa vyama vingi uingie nchini mwaka 1995 hajawahi kutaka kugombea Ubunge wa mahali popote kwanini leo aje kugombea Ubunge?