PCCB: Tuna manufaa nayo?

PCCB: Tuna manufaa nayo?

Ukisoma katiba kwa makini utakuja kugundua kuwa Tanzania serikali inapaswa kupelekwa The Hague kwa mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu.

Mengi wanayofanya ni kinyume na sheria na katiba.... pia wanatoa majibu mepesi kwa maswali magumu...

Ila pastor kishoka usihofu kwa kuwa sisi twaendelea kukua na yale meno yetu yatakua na kuanza kuwang'ata.

Hivi hosea hajajiuzulu??
 
Ajiuzulu achekwe? aachie hizo pesa zote za Vikamati?

Hivi hujasikia tetesi kuwa kamati ya EPA inaweza ongezewa muda na kila mjume wa Kamati nasikia anakamata laki moja ya Tanzania kwa siku tangu kamati iundwe!

Unalipwa mshahara, halafu unapopewa kazi maalum bado unapewa posho kutimiza wajibu wako ambao unalipwa kwa kupitia mshahara?

Hii sijawahi isikia popote ila Tanzania!
 
...halafu goddam ripoti inafungiwa kabatini....
Pinda ashasema kuwa waliokwiba EPA ni wazito mno, je alimaanisha TISS au ndo mambo ya vitisho from takukuru??? nasikia hosea anajua sana kucheza karata zake.
Hivi yule waziri mkuu wa israel somebody Rabin alifanywa nini na yule kijana ambaye alikuja kufungwa miaka miwili?.....
 
Ahhh taratibu Ustaadh Msanii, hayo maneno ni makubwa sana na si swadakta hata kidogo. Hayana tofauti na yale maneno ya kuingia msituni...
 
Mchungaji..naomba nitume sehemu ya hoja yako katika makala yangu ya Jumatano... umenipa nyongeza nzuri sana... kama ni msosi wa pilau.. umenipa kachumbari, ingekuwa ngoma umenipa manyanga, na ingekuwa ni wimbo basi wako ni "lele mama"... thanks.. kuna kitu tutakionesha kuhusu TAkukuru na kutoa pendekezo ambalo hadi hivi sasa halijatolewa Tanzania kuhusu hii Taasisi.

Daring to go where no one dared to before..!

good work sir!
 
Kama mzee wetu wa Busara alivyokuwa akisema "Ruksa" kaka, inshallah ujumbe uwafikie walengwa na Taifa!
 
Kishoka,

Sioni sehemu katika sheria inayosema ni lazima wachunguze yote au lolote katika uliyo yasema.

Sheria ya Kuzuia na kupambanana na Rushwa, 2007-11

Majukumu ya Tume ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, 2, 1 (2)

Tume ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa imeanzishwa kutekeleza majukumu yafuatayo;-

a) Kuchunguza na kushauri juu ya shughuli na taratibu katika taasisi za umma na binafsi ili kurahisisha utambuzi na uzuiaji wa rushwa na kuongeza uwazi na ufanisi katika taasisi husika.

b) Kuhimiza na kuendeleza uungaji mkono wa jamii katika kupambana na vitendo vya rushwa.

c) Kushauri taasisi za umma na binafsi juu ya njia na namna ya kupambana na vitendo vya rushwa na kupendekeza mabadiliko ya taratibu za kiutendaji ili kupelekea ufanisi ambao taasisi inaonelea ni muhimu ili kupunguza vitendo vya rushwa.

d) Kushirikiana na taasisi mbalimbali kitaifa na kimataifa katika mapambano dhidi ya rushwa.

e) Kuchunguza/kupeleleza na kwa kutegemea maelekezo ya Mkurugenzi wa Mashtaka kuendesha kesi chini ya sheria hii na makosa mengine anayohusisha rushwa.

f) Kuchunguza/kupeleleza tuhuma zozote, kosa lolote kwa mujibu wa sheria hii, njama za kutenda kosa kwa mujibu ya sheria hii na kitendo cha ofisa wa umma kinachohushwa na rushwa.
________________________________________

Ni wapi hapo wanapewa jukumu la kuchunguza kila mahala panaponuka rushwa?

Hii sheria ina make sense? Mimi nadhani tatizo ni sheria.
 
Kuhani,

Sikuandika kwa kusema ni Sheria, nimeandika kwa kuangalia utendaji wao.

Najiuliza wao TAKUKURu kuwa pro-active kumchunguza Mrema wa TANROADS siku tatu baada ya hoja kuletwa Bungeni, lakini hoja nyingine ambazo zina miaka nenda rudi na hata ushahidi wa kimazingira kuwa kuna Rushwa ya hali ya juu, hujasikia TAKUKURU wakijituma kuchunguza!

Sheria ya TAKUKURU ina walakini, hata hivyo, utendaji kazi wao pia una walakini na unaonyesha wazi kuwa TAKUKURU inachagua ni kipi ikichunguze na kipi kipuuzie.

Ndio maana nimehitimisha kuwa kuna maana gani kuendelea kuwa na Imani na Serikali na vyombo vyake vya Dola na Sheria ambavyo vinafanya kazi kwa Upendeleo na Ubaguzi?
 
Nimekuelewa.

Uko sawa 100%.

Nyongeza ni kwamba, kwa sababu sheria ni kama inampa Hosea discretion ya wapi pa kuchunguza na nani wa kumshtaki, ni vigumu kumbana na kusema 'hapa mbona hukuchunguza.'

Yani, kwa mujibu wa job description yake, yeye kazi yake inawezekana anaitimiza. Anaweza kukukuonyesha time sheet yake ya mwaka mzima ambayo inaonyesha alikuwa anachunguza kesi za rushwa masaa 40 kila wiki ya mwaka. Ukiimuuliza 'na kesi hii mbona hukuchunguza,' atakwambia 'nani kasema nichunguze na hiyo pia.'

Sheria inasema: f) Kuchunguza/kupeleleza tuhuma zozote, kosa lolote kwa mujibu wa sheria hii...

Hiyo ni tofauti na tuhuma zote, na makosa yote.

Ni kama TUKUKURU inapewa nguvu kuchagua lolote kati ya yote, sio yote.
 
Kuhani.. umeonesha kitu kimoja muhimu sana.. watu wanapotunga sheria ili kuruhusu mambo fulani fulani. Ndiyo maana tunaposema mabadiliko ya sheria ni pamoja na kitu kama hicho cha lugha. Mtu anaposema "lolote" hana maana "yote"! Hivyo akiamua kuchunguza hili na kuacha lile anakuwa bado ndani ya wigo wa majukumu yake. Lakini ukimwambie achunguze "yote" unamlaziimisha kufanya kitu.
 
...daaah, Kuhani bana... we love and hate you man! You're daaaaym GooD!!

...Takururu iendelee kuwepo, ila ifanyiwe overhaul katika sheria zake, majukumu na malengo. sheria ilizoanza nazo na zile ilizoongezewa mwaka jana bado hazikidhi mahitaji ya Tanzania yetu. Kama mabadiliko hayafanyiki within 14 - 18 months.... Takururu haitakuwa na maana tena, bora ivunjwe.

SteveD.
 
SteveD;

Kuchunguza sio vibaya...ni kwa ajili ya kujua whats up!
 
takukuru inaweza kutimiza wajibu wake, kama itaongozwa na mtu aliyeteuliwa na chombo huru kama bunge, na awajibike kwa bunge.

pia nafasu ya mkurugenzi mkuu wa takukuru ingepewa jaji mmoja mstaafu, mwenye busara na uaminifu usiotiliwa mashaka katika jamii

viongozi wa mkoa wa takukuru nao wateuliwe kwa minajili hiyo hiyo nakadhalika.
takukuru ya wala rushwa kama hawa walioko sasa ni afadhali isingekuwepo.
wanachokifuata KWA MREMA WA TANROADS, NI BAADA YA KUSIKIA ANALIPWA AROUND 120M, HIVYO WANAMFUTA ILI AWAGAWIE SOO LIISHE. MREMA KAMA UPO HAPA JF , USIWAPE HATA SHILINGI
 
Ni bora kutokuwa na kitengo kama hiki.

Si kwamba tunakataa malengo yake ila hatuoni kama kinaweza kuyatekeleza malengo yake!
Kwa sasa kitengo hiki kinaonekana kama ni chombo cha kuhalalisha rushwa kubwa na kuzuia rushwa ndogo! Ni wazi kabisa kuwa chombo hiki hakina ubavu wa kushughulikia ruswa kubwa na ni mara elfu milioni kukifutilia mbali kitengo hiki na kuwafikisha mahakamani viongozi wake kwa kulidanganya Taifa kuhusu suala la Richmond.
 
Hao maofisa wa PCCB wanaovujisha hizo habari naona wameishiwa ... ningewaona ni wa maana sana kama wangeleta report ambazo zinahusu rushwa ya mabilioni na siyo hizi kesi ambazo impact yake ni ndogo sana!
 
Nakumbuka yule Trafic Police wa Tsh 3,000/= (Elfu tatu tu) Walivyomshupalia na kesi ikaenda mahakani haraka haraka.
 
Back
Top Bottom