Nifanye nini ili nisikate tamaa? Mwaka juzi nilijitoa mnoo, nilisoma kama kichaa na nilitumia gharama kubwa. Nilikuwa natafuta crdt moja na nilifanya masomo manne. Maskini mie, matokea yalivyotoka nikaambulia D, sio siri niliumia kupita maelezo. Mwaka jana nikaamua kujiandikisha tena, kusema kweli nilipoteza hamu ya kusoma kabisa, kila siku nikawa nasema nitasoma kesho. Matokeo yake mitihani ikafika nami sijajiandaa, hivyo sikufanya mtihani kabisa japo namba nilipata. Mwaka huu natamani nifanye mtihani lakin roho yangu inasita vibaya mnoo. Nishaurini mwenzenu, shule bado naipenda lakin ndo hivyo.