Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Kama hivi
 

Attachments

  • downloadfile-2.jpg
    downloadfile-2.jpg
    44.3 KB · Views: 2
Sijui na sidhan kama kwa sasa kuna Kiongozi tena Mkuu wa Mkoa tu ambaye anaweza kuwa na Backup ya Viongozi wa Dini kama alivyokua Mh Paul Makonda.

Hakuna na hakuna hakika!!.

Kwakua ukikubalika na Dini ,umekubalika Mbinguni .

Aliyesema Makonda, ndiye yule Ajaye, hakulopoka, alisema haya kwa sababu aliona anafaa na kustahili.

Ukikosa ufahamu kila tukio utalichukulia kama lilivyopangwa na muandaaji.

Maigizo ya Makonda yanawalenga watu wasiotafakari wala kuwa na uwezo mkubwa wa kupambanua mambo. Na hata viongozi anaowatumia ama ni wale kiuhalisia, anaona ana uwezo wa kuwahadaa au anaamini wana tamaa ya fedha. Ndiyo maana anawaalika, anawalipia gharama na kisha kuwazawadia bakshishi ya pesa. Kama angekuwa na dhamira ya kuomba toba, alistahili aende akatubu kwa familia ya Ben, Azory, Lisu, GSM, Manji, Mo na wengine wote aliowafanyia uharamia.

Lengo la Makonda kuwaalika viongozi wa dini kwa kile kinachoitwa kumpa baraka ni usanii na hadaa tupu. Kutokana na uwezo wake mdogo kichwani, anaamini akiwaalika hao viongozi atajisafisha na yale mambo yake yanayofahamika kuwa yeye ni uuaji, mtekaji, mpotezaji watu, na mporaji wa mali za watu. Anaamini tabia zake hizi chafu za kishetani, zitafutika kwa kupiga picha na viongozi wa dini!!
 
Vijana wa mjini Arusha wajulikanao kama Wadudu wamemuhakikishia mkuu wa mkoa huo mh Paul Makonda kwamba Wataujaza uwanja Siku ya Mei Mosi na Wanahamasisha Wana Arusha wote wawepo Uwanjani

Makonda amewashukuru sana vijana hao kwa upendo na amewataka wasijiite Wadudu kwa sababu wao wameumbwa kwa mfano wa Mungu wa Mbinguni

Nawatakieni Dominica njema
 
Vijana wa mjini Arusha wajulikanao kama Wadudu wamemuhakikishia mkuu wa mkoa huo mh Paul Makonda kwamba Wataujaza uwanja Siku ya Mei Mosi na Wanahamasisha Wana Arusha wote wawepo Uwanjani

Makonda amewashukuru sana vijana hao kwa upendo na amewataka wasijiite Wadudu kwa sababu wao wameumbwa kwa mfano wa Mungu wa Mbinguni

Nawatakieni Dominica njema
Bangi tu hizo wana uwezo gani wa kuujaza uwanja hao wahuni?
 
Back
Top Bottom