Paul Makonda: Endeleeni kufunga barabara maana tumepewa jukumu la kuwasikiliza na kuisaidia Serikali

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,399
3,916
ENDELEENI KUFUNGA BARABARA MAANA TUMEPEWA JUKUMU LA KUWASIKILIZA NA KUISAIDIA SERIKALI - MWENEZI MAKONDA

"Kitu kimoja nimegundua hapa, hii staili yenu ya kufunga barabara mnapoona msafara wa Viongozi wanapita ni nzuri sana kwa maana inasaidia kusikiliza ba kutatua kero na changamoto zenu tena hapo kwa hapo"

"Endeleeni kuwa na tabia hii hii ya kufanga barabara haswa kwa Viongozi kama Mbunge, Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa, kwa maana jukumu walilopewa na tulilopewa ni kuhakikisha tunawasaidia kazi Mhe. Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu, hatuwezi tukawa na changamoto katika stendi hapa tukakaa na kusubiria hadi Waziri Mkuu aje, au Makamu au Rais HAPANA ni lazima tuwajibike katika kufanya kazi, sisi ndio wa kufata nyie, kusikiliza, kupokea na kutatua, sasa kuna Viongozi hawafanyi hivyo kwahiyo hii staili yenu ni nzuri sana, tena mimi mkiniona popote nisimamisheni yawekana nikapita sehemu nikaona mambo safi kumbe zipo kero zimejificha sio za kuonekana hivyo nipeni nami kama msemaji wa Chama Kikubwa duniani nitazishughulikia"

Hayo yamesemwa na Mwenezi Makonda akizungumza na Wafanyabiashara katika stendi ya Nyamongoro Wilayi Ilemela akiwa njiani kuelekea Mkoani Simiyu katika muendelezo wa ziara yake, leo tarehe 13 Novemba, 2022.

#CCMKazini
#VitendoVinaSauti
#KaziIendelee

1699857387333.jpg
 
Back
Top Bottom