Makonda: Kuna UJINGA unaendelea wa kumtofautisha Hayati Magufuli na Rais Samia

Mimi nimeleta kama ilivyo na kama alivyotamka .na leo sitaki kutia neno lolote lile nasoma tu maoni yenu wasomaji wangu.
Wewe umesharudi huyu Jamaa Yako.Kwanza mnafiki ni yule ambae analazimisha mfanano ambao haupo.

Ndio maana nikasema Kuna miradi ambayo ilianzishwa awamu ya Magufuli inaendelezwa na mama na mara kadhaa Mama amesema lazima amalizs miradi ya mtangulizi wake.

Sasa Kuna ubaya gani kulinganisha? Maana ieleweke kwamba Magufuli alikuwa anachukuliwa kama benchline ya kipimo Sasa pale inapoonekana Samia kafanya zaidia Kwa nini asisifiwe Samia? Utamtaja Magufuli hapo Kwa lipi? 🤪🤪🤪🤪
 
Kwanza nimshukuru mama Samia Kwa kutupa uhahi.

Tukija kwenye mada hili swala halikuanza awamu hii, hizi ni hulka na tabia za wanaccm.

Hata yeye Bashite leo kuna wanaojikomba kwake Kwa sababu ya hicho cheo na wala siyo kama yeye Bashite.

Kama mpaka Majaliwa ni chawa mwanaccm gani mwingine atakuwa siyo chawa?
 
Wewe umesharudi huyu Jamaa Yako.Kwanza mnafiki ni yule ambae analazimisha mfanano ambao haupo.

Ndio maana nikasema Kuna miradi ambayo ilianzishwa awamu ya Magufuli inaendelezwa na mama na mara kadhaa Mama amesema lazima amalizs miradi ya mtangulizi wake.

Sasa Kuna ubaya gani kulinganisha? Maana ieleweke kwamba Magufuli alikuwa anachukuliwa kama benchline ya kipimo Sasa pale inapoonekana Samia kafanya zaidia Kwa nini asisifiwe Samia? Utamtaja Magufuli hapo Kwa lipi? 🤪🤪🤪🤪
Choice variable rafiki yangu.kwa maslahi mapana ya chama changu cha CCM nisingependa kuweka maoni yangu hapa kwa leo juu ya kauli ya kiongozi wangu katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa. maana kuna mambo natakiwa kuzingatia miiko na maadili ya chama chetu.

Vipi umemuona dada yetu Dkt Tulia anavyowachachafya wazungu huko kwenye vikao vya IPU.kwa hakika Sugu atafute biashara ya kufanya tu.maana wazungu tu wanasema ni lazima dkt Tulia ashinde kwa kishindo
 
Katika hilo Makonda nakuunga mkono. Kama taifa hili na Afrika kwa jumla tunataka kupiga hatua na kukata minyororo ya mabepari wenye uchu, hakuna namna ya kukwepa baadhi ya mitazamo na actions za Baba Magufuli.
Ninakubaliana na Makonda tatizo la sasa ni unafiki wa kunasabisha mafanikio na mtu binafsi na siyo ilani au sera ya chama,wakati wa Nyerere,Mwinyi na Mkapa kilichoangaliwa ni mafanikio ya Ilani na siyo Rais kama mtu binafsi,wananchi wanapigia Ilani iliyo nzuri. fullstop
 
Kwani Makonda anatumikia mabwana wangapi?

Kwani si Kuna miradi inayoitwa ya Magufuli na miradi ya awamu ya 6 au?
Kama mradi upi huo wa awamu ya sita?

Awamu ya sita kwa "Ilani" ipi ya uchaguzi?

Maana Ilani inayotumika kwa sasa ni ile ile ya 2020 ya Magufuli!

Hii awamu ya sita ilichaguliwa na uchaguzi mkuu upi?
Je!
Hizi awamu....awamu zina Impact gani na Maendeleo chanya kwa watanzania?

Acheni kuutumia uzwazwa wa wanyonge kwa kuwadhalilisha!
 
Makonda katika sherehe za kuipokea ndege mpya ya ATCL (BOEING 737-9 MAX) jijini Dar; amekemea tabia inayoonekana kuanza kukua na kukomaa kwa baadhi ya viongozi wa Serikali kwa ngazi mbalimbali ya kujaribu kutenganisha mafanikio yanayoendelea kutokea chini ya Rais Samia na kipindi cha awamu ya tano chini ya JPM.

Wakijaribu kuchafua huku na kusifia huku. Kitendo kicho makonda amekemea na kutaka tabia hiyo ife kuanzia leo.

Kwani hata kipindi cha kuomba kura wawili hao walizunguka kila mahali pamoja akiwemo waziri mkuu kasimu majaliwa.

Awataka waache UNAFIKI na KUJIKOMBAKOMBA.


Kwa hiyo kwenye yale ya kwenye viroba, kutekana na wizi wa kura walikuwa wote?
 
Kama mradi upi huo wa awamu ya sita?

Awamu ya sita kwa "Ilani" ipi ya uchaguzi?

Maana Ilani inayotumika kwa sasa ni ile ile ya 2020 ya Magufuli!

Hii awamu ya sita ilichaguliwa na uchaguzi mkuu upi?
Je!
Hizi awamu....awamu zina Impact gani na Maendeleo chanya kwa watanzania?

Acheni kuutumia uzwazwa wa wanyonge kwa kuwadhalilisha!
Hayo maswali Sasa angeulizwa Makonda kwamba hii ni awamu ya 6 Kwa Ilani ipi?

Pili awamu ya 6 hakuna lugha ya wanyonge hiyo ni tofauti mojawapo ambayo Makonda anatakiwa kujua.

Kuhusu miradi anzia hapa 👇
-Miradi ya Kilimo Cha Umwagiliaji zaidi ya Bil.300 ikiwemo BBT
-Miradi ya Maji ,Mama kumtua ndoo kichwani mwanamke hapa kachapa mamirai ya mabilioni Kila Mkoa ,Wilaya na Vijijini nikiweka orodha nitajaza seva
-Miradi ya Afya , nadhani unakumbuka Mkopo wa COVID 19,tozo za miamala nk ,hapa mama amejenga zaidi ya vituo vya Afya 450 vs 350 vya Mwendazake,hapo sijataja mavitendea kazi
-Ukija kwenye Ajira ndio usiseme ,yule mwingine alikuwa anasingizia Sgr na bwawa 🤪🤪🤪

Kiufupi Mama ni nouma zaidi ndio maana wazee wa legacy mnayumba 😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁
 
Kwa utaratibu uliowekwa na Chama pendwa wa kumtukuza kwa mapambio na kumsujudu Rais! PM hamjamtendea haki Mama.
Yote aliyofanya JPM sifa zinapaswa kumwendea Mama!
Hata JPM yapo tuliyomsifu wakati aliyafanya JK mf.Daraja la Kigamboni,nk
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mimi leo wala sina maneno mengi ila nataka tu kuwaambia kuwa katika siku ya leo ambapo ni siku ya mapokezi ya ndege mpya iliyonunuliwa na serikali yetu ya CCM. Mheshimiwa Paul Makonda Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa .

Kwa hasira kali na kuonyesha moyo wake kujaa jazba na uchungu moyoni ametumia muda wa dakika mbili aliopewa kusalimia kuwashambulia wanasiasa aliowaita wanafiki,wajinga na wanasiasa uchwara wanaojipendekeza na kutaka kuonyesha kuwa mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia kuwa Hayati Dkt Magufuli hahusiki nayo.

Amesema huo ni unafiki mkubwa sana na ujinga kwa sababu Rais Samia anatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025.ambayo Rais Samia na Hayati Dkt Magufuli waliinadi kwa pamoja.hivyo anachokifanya Rais Samia ni Katika kuendelea na kazi hiyo ya utekelezaji wa ilani ya CCM.

Ametoa marufuku na onyo kali kwa wanasiasa kuwa leo iwe ndio mwisho wa tabia hiyo ya unafiki na ujinga huo wa kumuweka kando Hayati Dkt Magufuli katika mafanikio ya Rais Samia. amesema kuwa Waziri Mkuu Mh kasimu Majaliwa ndiye yule yule waziri mkuu wao wote wawili yaani Hayati Dkt Magufuli pamoja na Rais Samia.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Kwanini hauweki tena namba yako ya simu?
 
Kama hawataki atenganishwe kwakuwa walizunguka nchi nzima kwa pamoja kujinadi kwa Wapiga Kura, basi akubali pia kuwa, kwa sasa anamalizia kipindi chao cha pili cha miaka kumi kukaa Ikulu. Anapaswa kukaa pembeni wengine waingie kwenye kinyang'anyiro 2025.
 
Kwa utaratibu uliowekwa na Chama pendwa wa kumtukuza kwa mapambio na kumsujudu Rais! PM hamjamtendea haki Mama.
Yote aliyofanya JPM sifa zinapaswa kumwendea Mama!
Hata JPM yapo tuliyomsifu wakati aliyafanya JK mf.Daraja la Kigamboni,nk
Na huu ndio ukweli ndio maana nauliza ,Makonda anamtumikia bwana yupi?

Mfano Terminal 2 ya Julius Nyerere Airport alianzisha Ujenzi JK lakini sifa za JPM,the same to Tazara Flyover ,Tanzanite bridge nk nk
 
Back
Top Bottom