Paul Makonda: Ahsante Mungu katikati ya machozi umenipa mapacha wawili!

Status
Not open for further replies.
Ajifunze namna ya kuwa mzazi. Amshukuru mungu wake kimya tu. Hajui upepo anaowapulizia watoto wake.

Aliyoyafanya katika uongozi wake huenda malipo yake yakapitia kwa watoto hao, si vizuri kuwanenea maneno haya malaika hawa lakini uzoefu wa Karma, imani na philosophy huwa havina unafiki.

Atambue kwamba kuna wanaolia kwamba kuzaa si kupata na ni heri matumbo yao yangefungwa.

Aache ujinga, ni muda wa kusimama na kuwa mwanaume.
Kuna wenzake sasa hivi wanawapiga mnada mabint zao...
Your browser is not able to display this video.
 
CHADEMA watasema ni njama ya CCM ili Makonda azungumziwe na CHADEMA idode kule uchochoroni Arusha, wanaogopa viwanja vikubwa sikuhizi.
 
Mkuu wa mkoa wa Dsm mstaafu Paul Makonda amemshukuru Mungu kwa mkewe kujifungua mapacha wa kike na kiume.

Makonda amesema katikati ya machozi aliyonayo sasa Mungu amemkumbuka na kumpa zawadi.

My take; Sijajua Paul Makonda analilia nini?!!

Maendeleo hayana vyama!
 
Wakati ukiendelea kumshukuru Mungu na kutupia mapicha uwakumbuke na wale wana wa wenzako waliodhulumiwa uhai wao kupitia wewe hata kufikia kupigwa ban ya kuingia marekani

Wale nao wana wazazi wanaowapenda kama unavyowapenda wakwako
Nao pia wana maumivu kama nawe utakapopata maumivu ukisikia Kegan ama wadogo zake wameumizwa bila hatia

Uzazi na kuwa mzazi ni zaidi ya kumshukuru Mungu na kwa maneno matamu na kutupia picha nzuri kwenye mitandao

Umeandika Mungu kakuheshimisha katikati ya matatizo...na wale walionusurika kifo kupitia udhalimu wako watasemaje!? Je kati yako wewe na wao ni nani yuko juu kwa sasa?

Ulijisahau sana...sasa hivi ndio unajua nini maana ya kuitwa mzazi...Badala ya kumshukuru Mungu mitandaoni nakushauri jitenge na hadhira ukajifungie mahali pa upweke usali na kumuomba Mungu sana aepushe uzao wako na karma mbaya...

Wote walioumia kupitia mikono na mdomo wao...damu yao bado inakutafuta ..imezaa kisasi...inasubiri kikue na kukomaa...JITENGE kabisa na media ukajinyenyekeshe chini ya miguu ya Mola ukiomba msamaha na kufanya kitubio
 
Ukibarikiwa hakuna haja ya wewe kupigana na matangazo. Acha hiyo baraka ifanye matangazo. Watu wanaotakiwa kufahamu umebarikiwa watafahamu tu. Wakufurahi na ww watafurahi, watakaoumia wataumia.
 
daaaah sijui kwanini binadamu hua tunakoswa aibu wakati tunajua tunamkufuru mwenyezi MUNGU
 
Mbona hajamshukuru Mheshimiwa Rais na Mwenyekiti wa chama chake?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…