Paukwa... Pakawa!

Kuna mfano mmoja nilitoa kuwa inasemekana kuwa watu wa Ulaya wanapenda sana process (how you do things). Kwa upande mwingine waMarekani wanapenda results (How you accomplish things).

Attitudes hizi kwetu hatuna. Tunapenda tu kuzungumza big things and big Ideas.

Kama tuna nia ya kweli kwa kushikamana na kwa ujumla bila kujali tofauti zetu za kiitikadi, tunaweza kuunda mfumo wetu wa ProcSult ambayo ni blend ya Process na Results!
 
Rev. Kishoka,
Mkuu wangu hatukuwa maskini kwa bahati mbaya...
Aliyoyazungumza Zakumi ndio ukweli wa WATU na MAZINGIRA tuliyokuwa nayo.. Miaka arobaini ya Uhuru bado tunaagiza hata sindano kisha maneno mengi sana utadhani sisi ndio tumeandika vitabu vya uvumbuzi..
Sii kazi rahisi kabisa kushikamana kwanza hatujipendi wenyewe na pengine maumbile yetu maanake ukiambiwa hufafanani na Watanzania tunaona sifa!..Ni maskini jeuri na taifa lililokwisha kata tamaa kimaisha hivyo sisi ni Ombaomba msikitini hadi Umur Kiyama!..
 
Kwa kweli watz tuna matatizo sana na sijui nini hasa nia yetu. Tumelalamika sana juu ya ufisadi na mafisadi, leo JK amefanya kweli, tumeanza kuponda mara wengine ajiuzuru, na hoja zingine nyingi za kumkatisha tamaa.

Tumuungeni mkono Rais ili afanikishe zoezi hili, akishindwa yeye tumeshindwa wa tz
 
Haitawezekana Watanzania wote wafikiri kitu kilekile. Toafauti ni lazima zitakuwapo tu. Hata katika kuleta hoja ya ufisadi baadhi ya Watanzania walikuwa 'against' wakisema Tz hatujafikia 'level' ya huo ufisadi.

Kwa upande wangu kupata watu wanaoweza kuona jitihada za Kikwete (serikali) na wengione kuonyesha kuwa hawajaona kunaleta 'balance'. Tufuraihie kupanuka kwa uhuru wetu na watu kuweza kutoa dukuduku zao. Kitu unachokiona wewe inawezekana webgine hawajakiona na wana uhuru wa kusema kama hawajaona hizo jitihada.

Mimi nawapongeza wote waliowezesha kufikia tulipofikia kwa upande wa ufisadi. Ilikuwa kazi kwelikweli. Na hasa nawapongeza akina Dr Slaa. Wamefanya kazi nzuri sana japo sifa nyingi hazitaenda kwao. Lakini kelele zao za kuonyesha kuna moshi zimetuwezesha kuona kuna moto!
 
Sober,

Nikipima na kusoma kilichofanyika na hata "nia" ya kufikisha Mramba, Yona, Patel na Lukaza, natatizwa na lilelinalojionesha kwangu kuwa hawa wamepelekwa mahakamani si kwa nia au madhumuni ya kweli kuwa wachukuliwe hatua, bali ni kutokana na mashinikizo na sababunyingine za kufanya kuonekane kuwa sasa Serikali inafanya kazi yake.

Tumeshajiuliza sana hapa kuhusu suala la EPA kuwa Deloitte and Touche walifanya audit, wakatoa ripoti moja mbaya sana kuhusu BOT. Ripoti hiyo, hata Utoah ambaye ni mdhibiti na mkaguzu mkuu wa Serikali aliafikiana nayo na kutoa tathmini kuwa BOT imefanya kwa makusudi au kwa uzembe wa kupindukia kuruhusu hujuma za EPA.

Dr. Slaa akatoa kauli bungeni na sis tukapiga kelele, lakini Serikali yetu kwanza ikatoa kauli kukanusha kuwepo hujuma kubwa kama hiyo. Ni mpaka pale mabalozi wa nchi tajiri walipoanza kupiga kelele wakiongozwa na Mark Green wa USA, yule jamaa wa Neatherlands, Norway na Ujerumani na mpaka nchi moja wafadhili walipotoa kitisho kusitisha misaada (unakumbuka Membe alvyojibu kwa kiburi kuwa sisi ni nchi huru tusiingiliwe?) ndipo taratibu Serikali na Bunge la CCM likakubali kuna tatizo nao wakaipa kazi ya uchunguzi kampuni ya Earnst and Young.

Kina E&Y wakaja na majibu yale yale ya Deloitte Touche na Utoah, wakawasilisha serikalini. Rais na Serikali, wakaundia tume chini ya IGP, DPP, AG na Takukuru ambao walikuwa wanalipwa laki moja kwa siku. Kamati hii teule, ikapewa muda, nayo ikashindwa kumaliza uchunguzi ikabidi iombe iongezewe muda.

Kamati ilipomaliza utafiti na uchunguzi wake, ikawasilisha ripoti ikulu na kusema inasubiri uamuzi wa Rais.

Wabunge wakahoji, ripoti iko wapi? Ikulu ikasukuma ripoti kwa Sitta na wabunge watoe maamuzi, Bunge likajivua jukumu hilo, hivyo faili likarudi Ikulu.

Sasa wakati wa danadana hizi, Mama Killango akatoa kauli hapendwi mtu, wakaja kina Serukamba, Kisumo na Kingung'e kutoa kauli kali na chafu na kudai kuwa hakuna la msingi kuhusu EPA. Zaidi, CCM ikabadilisha kibao na kuanza kuhodhi sakata lote la EPA kwa kudai kuwa eti, wao ndio walioliibua na si mtu mwingine.

Wakati E&Y wanafanya uchunguzi wao, Manumba ambaye ni DCI alitoa kauli kuwa wao Polisi hawawezi kuanza kufanya uchunguzi wowote mpaka E & Y wamalize uchunguzi wao.

Sasa najiuliza, ikiwa karibu miezi 18 tumekuwa tukiimba EPA, EPA, EPA na kwanza Serikali na Waziri wake Meghji wakakanusha hakuna wizi au hujuma, Manumba akasema anasubiri Ikulu impe maelekezo ya nini cha kufanya, unategemea kufikishwa kwa hawa jamaa Mahakamani kutanipa furaha zaidi ya kuhoji kwa kuangalia mashitaka waliyosomewa?

Zakumi anadai kuwa ni heri basi tuwafunge hata kwa hayo makosa madogo madogo, je hiyo ndiyo suluhisho na njia ya kuhakikisha kuwa hakuna tena uhujumu?

Sasa hivi, minong'oni ni kuwa ili CCM ishinde kwa kishindo, inabidi suala la EPA na ufisadi yapatiwe japo namna ya kufanana na ufumbuzi. Zaidi ni ukweli kuwa wahisani wamesema hawatoi pesa zao kusaidia bajeti yetu mpaka kieleweke.

Sasa kwa nini mnamkasirikia au kufadhaishwa na Mchungaji anaposema kuwa hili ni changa na hakuna nia ya kweli kutafuta ufumbuzi?

Ama nikupeni mfano mwingine. Lowassa, Karamagi, Chenge na Msabaha. Hawa walifanya uzembe na wanatuhumiwa kuwa wamekula mlungula. Lakini baada ya wao kujitoa kwenye madaraka, hata ndaniya CCM yenyewe hawajachukuliwa hatua, hawajapewa karipio badala yake wanafanywa ni wafalme, wamepewa maandamano kuwapokea, bado wananyenyekewa ndani ya chama na v=hivyo kuonyesha umma kuwa wao wana nguvu na Serikali haina nguvu.

Ni mpaka pale matatizo yetu yatakapotatuliwa kwa nia ya kweli na usahihi wa kutatua, ndipo nitapata faraja. kinyume na hapo, ni changa mbalo nimelivalia miwani.

Mchungaji Ni ruhusu ni tumie vigezo vyako kujengea hoja!

Personaly siwezi kusema kinachotokea kwa watu kupelekwa mahakamani na all the movement sio kitu bora na historical in the country.

Lakini ninahoji kama namna kinavyofanyika kinaeleleza Nobility na credibility ya mfumo fulani wa kiutendaji unaojua fika unachokifanya.

Yaani ni kweli ndani ya serekali yetu kuna mfumo imara na madhubuti kutuaminisha kwa dhati kabisa kuwa uko hivyo tunavyouona leo. Huo mfumo umeanza lini kuwa hivyo tunavyoona. Ulikuwepo tangu lini? Chunguza vigezo alivyoorothesha mchungajia hapo juu. Ni kweli huo mfumo ilikuwawapo wakati yote hayo yanatokea?

Why Bother with all this?

Hivi ukisikia watu mia moja wasio na wazo wala ujuzi wa kurusha ndege wamechukua ndege dar airport na wamezirusha kuelekea toronto ...na kwa bahati wawili wakafanikiwa kutua salama huko Canada. Hilo halitakuwa jambo la kuwasifia hao waliofika salama..Si haki kuwasifia na kufanya sherehe na hoi hoi...? Nafikiri jibu ni ndio.Maana Mungu amejalia.

Lakini hiyo ndio ichukuliwe kuwa ndio taratibu sahihi za kufanya kazi kwenye viwanja na huduma za ndege?

Singekataa kuwasifia ...

Ningefanya hivyo huku nikijua fika udhaifu na mapungufu katika mchakato wote katiaka kufanya kazi na huduma za ndege. Kuona udhaifu na mapungufu hayo si kwa sababu nawachukia wafanya kazi wa viwanja vya ndege nk .. lakini ni uchambuzi katika kujua zaidi.

Ninachosema ni kuwa kinachofanywa na sereakali ya awamu ya nnne so far it very ok.

Lakini tungetaka kujua is it systematical? Ni parten gani kinafuata? Ni motive gani inakisukuma.

What is wrong on analysing that ?

Yes tunataka kujua kama wanabahatisha....!!!

au kama hawabahatishi !!!

Tunataka kujua mfumo na misingi ya mwenendo wote... Ili kama ni madhubuti na umekamilika ... tujue. lakini fuata vigezo hapo juu...mfumo huu ulikuwapo all the time.... when all that was taking place?

Kama wanabahatisha au vinginevyo tuwasifie ..lakini tutawasifu tukujia kuwa wanabahatisha au vinginevyo. Hapo tutakuwa sisi si majuha... tutantoa sifa zenye vigezo na zenye maono!! Na kwa namana hiyo tunakuw a kwnye nafasi nzuri ya kuboresha..huku tukisifu na kuona tunakokwenda au tunapopelekwa.

This isnt so far away from being very scientific. Na sio kuwa we are emotional and subjective to the whole thing. Hakuna haja ya watu kuogopa kuangalia hili swala kwa undani...na hata hivyo ni mchakato tu!

Kikwete and all the comapany wanaweza kuwa wazuri tu...! But kama haku-analyse the whole issue critically linaweza likawapelekea kusipo. that is why we ask them or anybody...kama kuna critical analysis iliyofanywa..ilwekwe hadharani sio vibaya tukishare. Na sio kufikirikwamba we are negative to what is happening.

Tusione aibu kutaka kujua mfumo unaotumika tangu kuanza kwa awamu ya nnne.

Umabadilika? and why?

Ni uleule?..kama ni hivyo tulikosea kuutizama?

Kama ni uleule na ulitegemewa kuyaleta haya yanayotokea sasa sawa...Lakini tudhibitishiwe!

Inawezakana kabisa ...We had a wrong perception na serekali ya awamu ya nne. Nakama ni hivyo sindio tunataka uchambuzi.

Personaly i really love what is happening! but also I should not be terrified to question it criticaly.
 
- Mzizi wa fitina kukatwa next week kati ya Jumanne na Jumatano, confirmed!

Mkapa, RA, Mgonja,Lowassa, Karamagi hapa ni kama kuna mizizi miwili sijui upi utakatwa. Maana naona kama tunaangalia zaidi upande wa EPA na hatuangalii sana upande wa Richmond, Rada etc
 
Kikwete and all the comapany wanaweza kuwa wazuri tu...! But kama haku-analyse the whole issue critically linaweza likawapelekea kusipo. that is why we ask them or anybody...kama kuna critical analysis iliyofanywa..ilwekwe hadharani sio vibaya tukishare. Na sio kufikirikwamba we are negative to what is happening.

Tusione aibu kutaka kujua mfumo unaotumika tangu kuanza kwa awamu ya nnne.

Umabadilika? and why?

Ni uleule?..kama ni hivyo tulikosea kuutizama?

Kama ni uleule na ulitegemewa kuyaleta haya yanayotokea sasa sawa...Lakini tudhibitishiwe!

Inawezakana kabisa ...We had a wrong perception na serekali ya awamu ya nne. Nakama ni hivyo sindio tunataka uchambuzi.

Personaly i really love what is happening! but also I should not be terrified to question it criticaly.

Azimio,

Hakuna kitu kizuri kama Utu na Uungwana.

Nalizungumzia hili la Utu na Uungwana si kwa mara ya kwanza bali ni mara nyingi nimmekuwa nikiomba Serikali iwe wakweli na kukiri kwetu inapokosea au kufanya uzembe. ZSerikali na watendaji wakija mbele ya Umma na kuomba radhi kwa makosa yao ikiwa pamoja na uzembe(mfano ni Lowassa na Richmond), ni rahisi kwetu kuwasamehe na kufanya kazi nao hata kutoonekana kuwa wachochezi.

Lakini, watendaji wetu wengi hawana utu wala uungwana. Wao wanajiona ni Miungu ya duniani na hawawezi kuwa wanyenyekevu na kuomba radhi pale panapokuwa na makosa kutoka kwao. Badala ya kuomba radhi na kupata kuungwa mkono na wananchi, wao wanakuwa na kiburi na jeuri.

Sasa viburi na jeuri zao zinatukwaza wananchi nasi hufikia mahali kuanza kuhoji kila kitu, kupima na kutafiti kila kitu maana hatuna tena imani na watendaji hawa na hasa pale tunapojua wazi kabisa kuwa wanachotuambia ni batili na uongo.

Kama Serikali isingekuwa kwenye denial kuhusiana na suala la EPA pale lilipotokea, si ajabu athari zake hasa kwa CCM zisingefikia hapa ilipo. Leo hii tusingekuwa tukimhoji kila mtu na kila jambo kuhusiana na uchunguzi wa EPA, watu wasingepoteza muda kusumbuana na Ballali au sasa tunavyohoji udhaifu wa mashitaka.

Same thing with Lowassa na Richmond, ilikuwa ni rahisi kusema tumecheza pata potea na si kiburi na jeuri iliyotoka miyoyoni mwao na vinywani mwao.

Nimesema hapo juu, pamoja na kuwa msimamo wangu kuhoji mchakato mzima wa kesi hizi za EPA na Mramba/Yona ni uleule, lakini kwa minajili ya kisiasa jinsi ninavyofikiri turufu hii inachezwa, basi niko tayari kumuunga mkono Kikwete ikiwa nta itaganda kwenye vidole!
 
- Again ninaomba ksuema kuwa tuko kwenye the right track, na huu ni wakati wa kumpa rais ushirikiano wetu, na hasa ningetegemea kuwaona upinzani waki -take charge, maana huu ndio hasa wakati wao, pale tunapoambiwa hakuna ushahidi wao ndio wanaopaswa kujitokeza na ushahidi mzito, maana sisi wananchi walipa kodi tunawalipa ruzuku kila mwezi, sasa tunawalipa ruzuku for what kama sio watusaidie wka mambo kama haya?

- Kuendelea kumlaumu rais after all this kwa kweli sioni kama ni productive, kwa sababu rais anatakiwa afanye nini zaidi ya haya aliyokwisha fanya tayari? Amefungua mlango sasa sisi wananchi tu-take a charge na pia tu-take advantage, Mramba na Yona wako rumande sio kwa sababu ya kushindwa dhamana, isipokuwa ni kuthibitisha kwamba wahusika wa ushitaki wako serious, binafsi ninataka kutoa pongezi nzito sana kwa rais na wahusika wote wa hii operation, na ningependa kuwapa moyo kwamba baadhi yetu wananchi tuko nyuma yao na tuko tayari kuwapa msaaada ikibidi, lakini nasema hvi rais amefanya ya kwake, sasa ni zamu yetu wananchi kumalizia na hasa ninategemea Upinzani kutuongoza hapa, maana ndio hasa sababu ya kuwapa ruzuku.

Ahsante Rev!

Jemedari Mkuu amina!
Katika yote mimi niyoyamwagia wino ndio hasa nilikuwa sijajua nani wa kushikilia bango hili saga. Umenipa jibu muruwa kabisa. Na wananchi pia wanatakiwa kufahamu hivi hivi kuwa ruzuku kwa wapinzani si fadhila ni kwa sababu wako kazini so wachape kazi kwa bidii wakati ndio huu
 
hapo umenena hii ni ze comedy inaendelea na tusubiri kuona mwisho wake maana waliofanya hayo yote wanapeta ila wanaopelekwa mahakamani ni wale mbuzi wa kafara
 
Mkulu Kishoka,

Heshima mbele bro, kwa kweli kinachoendelea so far ni mapema mno kusema wazi kwamba exactly ni nini hasa, between sheria na siasa, lakini:-

1. Wananchi wa Tanzania, tumeonewa vya kutosha na tumenyanyaswa na viongozi hasa wezi kwa muda mrefu sana, wakati wa Sokoine na uhujumu uchumi tumeona dagaa wakiswekwa lupango, huku papa wakiendelea kunawiri na kutucheka, tunasikia Sokoine alitaka kufanya kweli lakini Mwalimu alikataa kabisa, sasa this time is for real tunaona papa wakiswekwa lupango.
- Sokoine alikuwa tayari ana list ya viongozi wa juu mawaziri wakiwemo aliotaka wakamatwe, kwa kuhujumu uchumi na pia alimuhakikishia Mwalimu kwamba ana ushahidi wa kutosha, kati ya viongozi hao walikwemo Barongo, na Kahama, katika kutayarisha ushahidi wake Sokoine alishikirikiana sana na Kaisi, na Kolimba. Lakini Mwalimu alipokataa wasishikwe, Kaisi ambaye sasa alikuwa RC Bukoba was so upset kwamba akaamua kwa hasira kumuweka ndani Barongo alipofika Bukoba, na hata Kahama pia lakini Mwalimu akamlazimisha kumuacha haraka sana the minute alipojaribu kule Bukoba uwanja wa ndege, wakati sir George anashuka kutoka Dar. Kina balozi Magombe wamefanya mambo ya aibu sana huko majuu, kina Maryogo na wengine wengi sana, lakini ninampa heshima rais kwa kuimaliza hii tabia ya kulindana kwa viongozi, rais ameweka mfano sasa ni wajibu wetu wananchi ku-take it form there!
Ahsante Rev!

Mkuu Field Marshall,
Mwalimu alikokusea nini, ama aliwakosea nini ancestors wako? Katika postings zako naona unapopata mwanya lazima uchomekee lawama kwa Mwalimu! Let the old man rest in Eternal Peace, Amen. Kalifanyia makubwa Taifa hili, makubwa ambayo wala hayawezi kulinganishwa na si rahisi kufutwa.

Naelewa unajua mengi ama umesimuliwa mengi kutokana na sources zako, lakini I think it is uncalled for kutumia informations ulizonazo kuchafua majina ya wazee waliolitumikia taifa hili ambao wala hatuoni mijimali waliyojilimbikizia kwa kutoshitakiwa na Mwalimu!

Let's be realistic, Barongo, Sir George na Mzee Maryogo ndio 'papa' walioachiwa kuendelea kunawiri na kuwachekeni?! Mzee Barongo, kama sikosei, ni marehemu na kafa maskini baada ya kulitumikia taifa hili kwa uwezo wake wote pamoja na elimu duni aliyokuwanayo. Tumeishasahau jinsi alivyokuwa akihamasisha Kilimo Bora? Sioni sababu ya msingi ya kuwataja na kuwachafua wazee hawa ambao walijitolea kulitumikia taifa letu kabla na baada ya Uhuru na hawakutumia nafasi zao kujilimbikizia mijimali. Wapo waliotamani, lakini tamaa zao hazikuweza kutimia kutokana na udhibiti na jicho kali la Mwalimu.

Nimetoa tabasamu kubwa kusoma jina la Kaisi! Nsa ni mwanajeshi, huenda alitumia taaluma yake bila utaratibu!

Awamu ya Kwanza kulikuwa na uozo gani mkubwa sana uliotendeka wa kuweza kulinganishwa na haya tuliyoyashuhudia ndani ya awamu zilizopita na tunayoyashuhudia hivi sasa, tunayojadili? Mind you, UTU aliokuwanao Mwalimu ulimfanya awe makini sana alipopelekewa tuhuma dhidi ya kiongozi ama mtu yeyote yule. Hakupenda kumuonea mtu. Kabla hajatoa uamuzi wa jambo lolote zito, alikuwa mwepesi kufanya utafiti wake binafsi kwa kuwatumia watu mbalimbali na kwa kupata mawazo ya watu makini walioaminika, wakiwemo viongozi wenziwe, nje ya mfumo. Kutokana na taarifa alizopata, aliweza pia kuwajua wafitini wa wakati huo. Kama alimwambia Kaisi awaachie aliowakamata, alikuwa na uhakika hao hawakuwa ‘wahujumu’ uchumi wa wakati huo.

Mwalimu alimheshimu sana Sokoine na kuithamini sana kazi nzuri aliyokuwa akiifanya kuhusu uhujumu uchumi. Tusisahau kwamba hapa tunazungumzia Rais na Waziri Mkuu wake. Kabla ya Sokoine (Waziri Mkuu) kuchukua hatua yoyote ya aina hiyo lazima alishauriana na kukubaliana na (Rais) Mwalimu. Kwa maana hiyo, suala la kuwashughulikia wahujumu uchumi halikuwa la Waziri Mkuu pekee. Nashindwa kupata picha ya Sokoine kunung'unika pembeni kwamba alitaka Barongo na Sir George wakamatwe lakini Mwalimu amekataa bila sababu! Sokoine hakuwa mnafiki!

And, Mzee Maryogo of all the people! FEMS, huyu mzee atakufa maskini kwa sababu ya uadilifu wake. Pia atakufa maskini kwa sababu yeye ni 'maskini jeuri', neno ‘kujipendekeza’ halimo kwenye vocabulary ya mzee Maryogo! Alipokuwa Utalii, aliweza kuokoa mamilioni ya fedha za Serikali kwa kumpelekea Mwalimu taarifa za kufichua njama za uhujumu. Ah! na marehemu Magombe naye alikuwa 'papa' wa uhujumu?!

Tuwasifie ma-Rais wetu na viongozi wa awamu zilizopita, awamu ya sasa na awamu zijazo kwa hatua wanazochukua kwa manufaa ya taifa letu. Mazingira ya miaka 40 iliyopita hayawezi kamwe kufanana na ya juzi, jana, leo, ama kesho. Tutakuwa hatumtendei haki Mwalimu aliyejitahidi kwa akili zake zote, kwa nguvu zake zote na kwa uwezo wake wote kutuwekea misingi bora ya uadilifu, tukaibomoa wenyewe.

FEMS, no hard feelings, ni kujaribu kukupunguza munkari dhidi ya Mwalimu na marehemu wengine!
 
Nimefurahi kusikia wanaowashtaki Mramba na Yona si Kikwete ila serikali, na wanafanya kazi pale Kikwete anapotoa go ahead!

So hatuna serikali, ila mpaka iambiwe na Kikwete!!!!!

hapa kutakuwa na uonevu, kuwa wezi fulani waende na wengine wasiende

Kwa hiyo mwizi yeyote awe raiskwa sababu hatuna imani na atakayekuja!

Yaani katika watanzania milioni 40, we can not trust someone to lead us???

ina maana una confirm jamii ya watanzania ni fisadi wote, so siyo kosa kabisa Kikwete kuwa rais hata kama naye aliingia mikataba mibovu na kuua watu!!

Inabidi tuwe clean, siyo kusema huyu afadhali msafi kuliko huyu?? kichekesho hiki.

Mchakato mzima wa kumpata rais Tanzania ni kichekesho kwenye vyama vyetu, wanampata ka presha za muda huo na sio nini alifanya siku za nyuma.

UKIFIKA WAKATI UKAONA KIKWETE ANAFAA KWA URAIS NA UKAONA HAKUNA WA KUM-REPLACE BASI FORGET CCM WILL RULE FOREVER!!!!!!

Hatuko katika process ya kupata pure gold. Kuna vicious circle ya ufisadi na rushwa na inayotakiwa kufanyiwa kazi.

Vilevile suala kumpata mtu atakayetawala vizuri kwa muda wote sina uhakika nalo kuwa ni la umuhimu sana kwa wakati tulio nayo. Lakini akitokea mtu aka-rise to the occasion na kujibu matatizo ya watanzania japo partially atakuwa ametusaidia zaidi wakati tukimsubiri Mussa.
 
UKAGUZI WA MAJENGO BENKI KUU NI USANII MWINGINE

Jamani usanii umetuzidi watanzania. Nahisi magazeti pia hutumiwa kuwajenga hoja zenye kiini macho na kuwazuga wananchi tu – propaganda za kuficha ukweli. Ni kitu cha kufarahisha sana jinsi gazeti la Nipashe la Jumapili 30 Novemba 2008 lilivyoandika kichwa cha habari kikubwa kuwa kampuni ya kimataifa ya wakaguzi wa hesabu wa katika masuala ya majengo M/S Mekon Arc Consult Limited ikishirikiana na kampuni mbili za kimataifa AQE Associates and Bureau for Industries Ltd wameshaanza kazi na wameanza kuuliza maswali kuhusu gharama. Ukweli ni kwamba tenda ya ukaguzi huo – Value for Money, ilikuwa ya ushindani wa kimataifa na makampuni makubwa ya ukaguzi huo wa kitaalamu kutoka nje ya nchi – Africa Kusini, Uingereza, Marekani, Kenya, Uganda walilita tenda zao lakini wote walipigwa chini kwa kuogopa mambo yasiwe kama yale ya wakaguzi wa EPA. Viongozi wenye hekima serikalini waliopendekeza Ernst & Young wachaguliwe kufanya uchunguzi wa EPA wamelaumiwa vibaya sana na vigogo mbalimbali mafisadi serikarini kwani Ernst & Young waliwashikia bango serikari pamoja ni kupigwa mikwara kibao na kuahidiwa tenda kibao za consulting iwapo wangeisaidia serikali kuficha ukweli. Sasa Governor mpya Ndulu alikuja na moto mkali na nia ya kusafisha Benki lakini mambo yanakuwa magumu na naye kashaonywa asaidie kuzima moto na kufukia mashimo, aibu inatosha.

Kampuniya Mekon Arch Consult Limited inamilikiwa na Mtu anaita Moses Mkony yeye hapo zamani alishakuwa Engineer wa serikalini akipafanyakazi National Housing Corporation. Kwa sasa amestaafu na kufungua kampuni yake hiyo ya Mekon Arch Consult Limited iliyokuwa na ofisi zake sehemu ya Kijitonjama kichochoro cha karibu na shule ya msingi kijitonyama.

Kampuni hiyo imeshirikiana na kitengo cha Bureau for Industrial Cooperation (BICO) ni kitengo cha chuo kikuu cha Dar es Salaam chenye kutoa ushauri/consultancy kwa mambo mbali mbali ya ufundi kwa ujumla. Ni mradi wa Chuo Kikuu na sio kampuni binafsi lakini kiongozi wa BICO ni Dr. B.B. Nyichomba. Angalia web page ya BICO katika web site ya chuo kikuu Dar es Salaam

Aqe Associates Ltd pia ni kampuni local ya Quantity Surveyors wako pale Samora Avenue Dar es Salaam,. Tel 255 22 2118225; Tel 255 754 261482 na inamilikiwa na maofisa wa chuo cha Ardhi Institute pale Chuo kikuu, Mmoja wa associates ni Dr. Aldo Lupala mhadhiri pale Ardhi. Hawa ni kuku wa kienyeji mtupu, hakuna hata mzungu wala “ya kimataifa”

Sasa hapo jameni kuna ukweli kuhusu stori ya mwandishi wa Nipashe ya jumapili. Hizi ni kampuni za kimataifa za kukagua mahesabu ya ujenzi kweli? Makao makuu ya MEKON yako uchochoroni kijitonyama nyumba ya kupanga hii kampuni na bwana Mkony wanababe wa kukagua Benki kuu kweli. Kipato chao kidogo kabisa, wanawezaje kuwa independent wakati total income yao ni kiduchu na wanataka kukagua benki kuu yenye mabilioni, je code of ethics za Engineers zinakubali hali kama hiyo?

Watakuwa prone for intimidation kani consulting fee toka Benki kuu kwa kazi hiyo ni kubwa mno.

Benki kuu/Gavana kaamua kuchagua kijikampuni kilicho very local, wenyekukimiliki wako hoi kwa poverty wakikimbiza vijitenda vya ujenzi hapa na pale. Kwa makusudi Gavana anataka aweze kuwa–control. Kwani wamejifunza baada ya kuajiri makampuni ya kimataifa yanakuwa ngangari na kuwashikia bango.

Nafikiri ni suala la muandishi wa nipashe kupotosha ukweli aidha makusudi baada ka kula rushwa ya watuhumiwa ili kuanza kuweka kiini macho, au mwandishi kutoku-fanya utafiti wa kina.

Mkitaka kufuatilia ofisi za Mekon ziko wapi, nitawapa picha ya ofisi hizo, ni kujumba kiko Kijitonyama, ukiwa unatokea makumbusho kuelekea mwenge, unakata kona ya kushoto ya lami pale science kuelekew tandale. Ukiwa barabara hiyo ya Tandale hesabu kona ya tatu kushoto, oposite na car show room moja kata kona hiyo ya kushoto kama uanenda kanisa la KKKT Kijitonyama utaona bango mkono wa kushoto, wanauza makuti ya kusuka, Ukipotea ulizia wanakouza makuti ya kusuka na mafuta ya taa. Ofisi ya Mekon iko hapo. Mekon, Plot 602, Kijitonyama, P O Box 31924 Dar es Salaam, Tel. +255 22 2700784, Fax. +255 22 2647552, Mobile. +255 744 262 249 email
moses_mkony@hotmail.com au mekon@africaonline.co.tz

Kiini macho hicho cha Gavana Ndulu tumekishutukia. Je kampuni hizo zina utaaalamu wa wa uchunguzi wa kina wa kimahesabu na uwezo wa kugundua wizi wa kalamu?

WANANCHI PASI HIYO, TUENDELEE KUPINGA RUSHWA NA UBADHILIFU WA FEDHA ZA UMMA.

NAOMBA WASOMAJI MUINDELEZE HOJA HII, WANA-NCHI WAPATE UPEO WA SIRI NA VIINI MACHO VYA SERIKARI.
 
Mkuu Field Marshall,
Mwalimu alikokusea nini, ama aliwakosea nini ancestors wako? Katika postings zako naona unapopata mwanya lazima uchomekee lawama kwa Mwalimu! Let the old man rest in Eternal Peace, Amen. Kalifanyia makubwa Taifa hili, makubwa ambayo wala hayawezi kulinganishwa na si rahisi kufutwa.

Naelewa unajua mengi ama umesimuliwa mengi kutokana na sources zako, lakini I think it is uncalled for kutumia informations ulizonazo kuchafua majina ya wazee waliolitumikia taifa hili ambao wala hatuoni mijimali waliyojilimbikizia kwa kutoshitakiwa na Mwalimu!

Let's be realistic, Barongo, Sir George na Mzee Maryogo ndio 'papa' walioachiwa kuendelea kunawiri na kuwachekeni?! Mzee Barongo, kama sikosei, ni marehemu na kafa maskini baada ya kulitumikia taifa hili kwa uwezo wake wote pamoja na elimu duni aliyokuwanayo. Tumeishasahau jinsi alivyokuwa akihamasisha Kilimo Bora? Sioni sababu ya msingi ya kuwataja na kuwachafua wazee hawa ambao walijitolea kulitumikia taifa letu kabla na baada ya Uhuru na hawakutumia nafasi zao kujilimbikizia mijimali. Wapo waliotamani, lakini tamaa zao hazikuweza kutimia kutokana na udhibiti na jicho kali la Mwalimu.

Nimetoa tabasamu kubwa kusoma jina la Kaisi! Nsa ni mwanajeshi, huenda alitumia taaluma yake bila utaratibu!

Awamu ya Kwanza kulikuwa na uozo gani mkubwa sana uliotendeka wa kuweza kulinganishwa na haya tuliyoyashuhudia ndani ya awamu zilizopita na tunayoyashuhudia hivi sasa, tunayojadili? Mind you, UTU aliokuwanao Mwalimu ulimfanya awe makini sana alipopelekewa tuhuma dhidi ya kiongozi ama mtu yeyote yule. Hakupenda kumuonea mtu. Kabla hajatoa uamuzi wa jambo lolote zito, alikuwa mwepesi kufanya utafiti wake binafsi kwa kuwatumia watu mbalimbali na kwa kupata mawazo ya watu makini walioaminika, wakiwemo viongozi wenziwe, nje ya mfumo. Kutokana na taarifa alizopata, aliweza pia kuwajua wafitini wa wakati huo. Kama alimwambia Kaisi awaachie aliowakamata, alikuwa na uhakika hao hawakuwa ‘wahujumu’ uchumi wa wakati huo.

Mwalimu alimheshimu sana Sokoine na kuithamini sana kazi nzuri aliyokuwa akiifanya kuhusu uhujumu uchumi. Tusisahau kwamba hapa tunazungumzia Rais na Waziri Mkuu wake. Kabla ya Sokoine (Waziri Mkuu) kuchukua hatua yoyote ya aina hiyo lazima alishauriana na kukubaliana na (Rais) Mwalimu. Kwa maana hiyo, suala la kuwashughulikia wahujumu uchumi halikuwa la Waziri Mkuu pekee. Nashindwa kupata picha ya Sokoine kunung'unika pembeni kwamba alitaka Barongo na Sir George wakamatwe lakini Mwalimu amekataa bila sababu! Sokoine hakuwa mnafiki!

And, Mzee Maryogo of all the people! FEMS, huyu mzee atakufa maskini kwa sababu ya uadilifu wake. Pia atakufa maskini kwa sababu yeye ni 'maskini jeuri', neno ‘kujipendekeza’ halimo kwenye vocabulary ya mzee Maryogo! Alipokuwa Utalii, aliweza kuokoa mamilioni ya fedha za Serikali kwa kumpelekea Mwalimu taarifa za kufichua njama za uhujumu. Ah! na marehemu Magombe naye alikuwa 'papa' wa uhujumu?!

Tuwasifie ma-Rais wetu na viongozi wa awamu zilizopita, awamu ya sasa na awamu zijazo kwa hatua wanazochukua kwa manufaa ya taifa letu. Mazingira ya miaka 40 iliyopita hayawezi kamwe kufanana na ya juzi, jana, leo, ama kesho. Tutakuwa hatumtendei haki Mwalimu aliyejitahidi kwa akili zake zote, kwa nguvu zake zote na kwa uwezo wake wote kutuwekea misingi bora ya uadilifu, tukaibomoa wenyewe.

FEMS, no hard feelings, ni kujaribu kukupunguza munkari dhidi ya Mwalimu na marehemu wengine!

Bibi Ntilie:

Wengine bado tulikuwa shule ya msingi lakini tunakumbuka sana kilichotokea 1983. Barongo alikamatwa katika uhujumu wa uchumi. Na alitolewa ndani bila sababu za kueleweka na habari zilitokea kwenye gazeti la uhuru.

Kitendo cha kutolewa kwa Barongo hakikumfurahisha Sokoine. Na ilibidi Barongo arudishwe ndani.

Nyerere alikuwa mtu mwenye huruma na alisamehe sana viongozi waliofanya makosa. Na viongozi wengi wali-take advantage ya huruma zake.

Kwa context ya kile alichozungumza Field Marshall, kama Sokoine angeachiwa plan za uhujumu uchumi azifanye mwenyewe basi baadhi ya mawaziri wangekuwa ndani na labda tusingekuwa katika vicious circle tulizonazo sasa.
 
UKAGUZI WA MAJENGO BENKI KUU NI USANII MWINGINE

Jamani usanii umetuzidi watanzania. Nahisi magazeti pia hutumiwa kuwajenga hoja zenye kiini macho na kuwazuga wananchi tu – propaganda za kuficha ukweli. Ni kitu cha kufarahisha sana jinsi gazeti la Nipashe la Jumapili 30 Novemba 2008 lilivyoandika kichwa cha habari kikubwa kuwa kampuni ya kimataifa ya wakaguzi wa hesabu wa katika masuala ya majengo M/S Mekon Arc Consult Limited ikishirikiana na kampuni mbili za kimataifa AQE Associates and Bureau for Industries Ltd wameshaanza kazi na wameanza kuuliza maswali kuhusu gharama. Ukweli ni kwamba tenda ya ukaguzi huo – Value for Money, ilikuwa ya ushindani wa kimataifa na makampuni makubwa ya ukaguzi huo wa kitaalamu kutoka nje ya nchi – Africa Kusini, Uingereza, Marekani, Kenya, Uganda walilita tenda zao lakini wote walipigwa chini kwa kuogopa mambo yasiwe kama yale ya wakaguzi wa EPA. Viongozi wenye hekima serikalini waliopendekeza Ernst & Young wachaguliwe kufanya uchunguzi wa EPA wamelaumiwa vibaya sana na vigogo mbalimbali mafisadi serikarini kwani Ernst & Young waliwashikia bango serikari pamoja ni kupigwa mikwara kibao na kuahidiwa tenda kibao za consulting iwapo wangeisaidia serikali kuficha ukweli. Sasa Governor mpya Ndulu alikuja na moto mkali na nia ya kusafisha Benki lakini mambo yanakuwa magumu na naye kashaonywa asaidie kuzima moto na kufukia mashimo, aibu inatosha.

Kampuniya Mekon Arch Consult Limited inamilikiwa na Mtu anaita Moses Mkony yeye hapo zamani alishakuwa Engineer wa serikalini akipafanyakazi National Housing Corporation. Kwa sasa amestaafu na kufungua kampuni yake hiyo ya Mekon Arch Consult Limited iliyokuwa na ofisi zake sehemu ya Kijitonjama kichochoro cha karibu na shule ya msingi kijitonyama.

Kampuni hiyo imeshirikiana na kitengo cha Bureau for Industrial Cooperation (BICO) ni kitengo cha chuo kikuu cha Dar es Salaam chenye kutoa ushauri/consultancy kwa mambo mbali mbali ya ufundi kwa ujumla. Ni mradi wa Chuo Kikuu na sio kampuni binafsi lakini kiongozi wa BICO ni Dr. B.B. Nyichomba. Angalia web page ya BICO katika web site ya chuo kikuu Dar es Salaam

Aqe Associates Ltd pia ni kampuni local ya Quantity Surveyors wako pale Samora Avenue Dar es Salaam,. Tel 255 22 2118225; Tel 255 754 261482 na inamilikiwa na maofisa wa chuo cha Ardhi Institute pale Chuo kikuu, Mmoja wa associates ni Dr. Aldo Lupala mhadhiri pale Ardhi. Hawa ni kuku wa kienyeji mtupu, hakuna hata mzungu wala “ya kimataifa”

Sasa hapo jameni kuna ukweli kuhusu stori ya mwandishi wa Nipashe ya jumapili. Hizi ni kampuni za kimataifa za kukagua mahesabu ya ujenzi kweli? Makao makuu ya MEKON yako uchochoroni kijitonyama nyumba ya kupanga hii kampuni na bwana Mkony wanababe wa kukagua Benki kuu kweli. Kipato chao kidogo kabisa, wanawezaje kuwa independent wakati total income yao ni kiduchu na wanataka kukagua benki kuu yenye mabilioni, je code of ethics za Engineers zinakubali hali kama hiyo?

Watakuwa prone for intimidation kani consulting fee toka Benki kuu kwa kazi hiyo ni kubwa mno.

Benki kuu/Gavana kaamua kuchagua kijikampuni kilicho very local, wenyekukimiliki wako hoi kwa poverty wakikimbiza vijitenda vya ujenzi hapa na pale. Kwa makusudi Gavana anataka aweze kuwa–control. Kwani wamejifunza baada ya kuajiri makampuni ya kimataifa yanakuwa ngangari na kuwashikia bango.

Nafikiri ni suala la muandishi wa nipashe kupotosha ukweli aidha makusudi baada ka kula rushwa ya watuhumiwa ili kuanza kuweka kiini macho, au mwandishi kutoku-fanya utafiti wa kina.

Mkitaka kufuatilia ofisi za Mekon ziko wapi, nitawapa picha ya ofisi hizo, ni kujumba kiko Kijitonyama, ukiwa unatokea makumbusho kuelekea mwenge, unakata kona ya kushoto ya lami pale science kuelekew tandale. Ukiwa barabara hiyo ya Tandale hesabu kona ya tatu kushoto, oposite na car show room moja kata kona hiyo ya kushoto kama uanenda kanisa la KKKT Kijitonyama utaona bango mkono wa kushoto, wanauza makuti ya kusuka, Ukipotea ulizia wanakouza makuti ya kusuka na mafuta ya taa. Ofisi ya Mekon iko hapo. Mekon, Plot 602, Kijitonyama, P O Box 31924 Dar es Salaam, Tel. +255 22 2700784, Fax. +255 22 2647552, Mobile. +255 744 262 249 email
moses_mkony@hotmail.com au mekon@africaonline.co.tz

Kiini macho hicho cha Gavana Ndulu tumekishutukia. Je kampuni hizo zina utaaalamu wa wa uchunguzi wa kina wa kimahesabu na uwezo wa kugundua wizi wa kalamu?

WANANCHI PASI HIYO, TUENDELEE KUPINGA RUSHWA NA UBADHILIFU WA FEDHA ZA UMMA.

NAOMBA WASOMAJI MUINDELEZE HOJA HII, WANA-NCHI WAPATE UPEO WA SIRI NA VIINI MACHO VYA SERIKARI.

TAFADHALI IWEKE HII IWE NEWS MPYA YA KUCHANGIA
 
You are absolutely right Rev!

Hapa inabidi tuwe makini.Kwa kawaida katika mifumo ya kiutawala, wanasiasa in this case Mawaziri huwajibika kisiasa kwa makosa/mapungufu yaliyotendwa na watendaji walio chini yao. Mara nyingi Raisi atamtaka waziri husika awajibike kwa kujiuzuru.

Tukumbuke kwamba waziri siyo tecnocrat. kazi kubwa ya waziri ni kutoa miongozo ya kisera (policy direction), kutetea bajeti ya wizara ( bread winner for his ministry), na ndio kioo cha wizara (public face of the ministry). juu ya yote ndiye 'accountable officer i.e. the buck stops with the minister!

Je waziri anafanyaje maamuzi? there is a time honoured established ministerial decision making process/bureucracy ambayo inabidi waziri ajiridhishe kwamba imefuatwa kabla hajaweka sahihi yake kwenye document yoyote ile. na document inamfikia waziri ikiwa imeambatana na dokezo kutoka kwa PS/Commissioner/Mkurugenzi. Hawa nao hawatakiwi kukurupuka tu ..wanatakiwa wazingatie ushauri wa wataalamu walio chini yao ambao watakuwa wamefanya 'upembuzi yakinifu' kabla ya hoja hoja haijapelekwa kwa waziri.

At least in theory thats how things are supposed to be done. In reality kuna mazingira fulani ambayo yanapelekea utaratibu huu usifuatwe: corruption, political considerations, national security and of course amri kutoka juu. Hapa ndio unaona watu wazima wanapitisha mikataba ya mangungo kama vile hakwenda shule! Utaratibu wa aina hii umeota mizizi, in fact umegeuka kuwa 'utaratibu mbadala' na watawala wameamua kuukubali bila kuona haya.

Katika level ya baraza la mawaziri kuna utaratibu unaitwa " collective responsibility". wataalamu watakuwa wamefanya upembuzi yakinifu, hoja imeandaliwa, inaletwa kama "cabinet paper" , mawaziri wote wana afiki. siyekubali, anajiuzuru! hoja ikiwalipukia kwa wananchi, baraza zima la mawaziri linatakiwa lijiuzuru. siyo kumtoa kafara waziri mmoja mmoja kwa maamuzi yaliyofanywa jumla! iko wapi principle ya collective responsibility?

Vyombo vyetu HURU vya usimamizi: Takukuru, CAG, BRELA etc hawa tuna assume wanao utaalamu wa kutosha kusimamia na kugundua ubadhirifu wa watendaji mara tu unapojitokeza ama unapoelekea kujitokeza! Hivi vyombo ndio tumaini la wananchi dhidi ya watendaji na wanasiasa wabadhirifu. So walikuwa wapi miaka yote hiyo wakati hawa jaamaa wajitotea mali za wananchi? wengi wa viongozi wa hizi taasisi ni matajiri wa kupindukia (at least by Tanzanian standards). Je wao ni safi? Kama si safi je tuna uhakika gani kwamba hizi kesi za EPA wamedhamiria kuziendesha vizuri ili mtanzania apate haki yake?
Sambamba na kesi ya EPA tuna uhakika gani kwamba haitatokea EPA nyingine? Ndiyo maana mabadiliko makubwa katika vyombo vya usimamizi wa mali za mtanzania inabidi yafanyike sambamba na hizi kesi za EPA.

Halafu inabidi watanzania kulipa umakini suala la Political Party Financing. Hii issue ni ya muhimu sana kwani ndiyo imepelekea kuundwa kwa Kagoda, madudu ya Meremeta and whatever else .Wakati wa uchaguzi wa urais marekani kikomo cha juu kabisa cha mtu binafsi kuchangia kampeni ya mgombea ilikuwa dollar 2300. Inabidi ndungu zangu vitabu vya mahesabu vya vyama vyetu vya siasa viwe wazi na kuwe na ukomo katika kufadhili vyama. Otherwise ufadhili huu wa vyama kwa jinsi ulivyo sasa hauna tofauti na "ununuzi wa vyama vya siasa, viongozi wake na wanachama wake". Vyama vya siasa vinalipa vipi hizi fadhila za mafedhuli? EPA na Richmond zipetupa mifano ni jinsi gani nchi ilivyo mikononi mwa genge la majambazi wanaovalia suti za bei mbaya, tai za kupenzeza na kalamu zao za "parker"! Bila ya Mangula na Makamba kufika mahakamani hizi kesi za EPA ni viini macho tu.

Kila niwaonapo Mramba na Yona mahakamani, nyuma yao ama pembeni yao inabidi wawepo watendaji waliokuwa chini yao..at least fifty other people nao wakishtakiwa kwa uzembe, kumshauri waziri vibaya, kuliingizia taifa hasara, kujitajirisha isivyo halali...etc etc.

to be continued........
 
Mkuu Field Marshall,
Mwalimu alikokusea nini, ama aliwakosea nini ancestors wako? Katika postings zako naona unapopata mwanya lazima uchomekee lawama kwa Mwalimu! Let the old man rest in Eternal Peace, Amen. Kalifanyia makubwa Taifa hili, makubwa ambayo wala hayawezi kulinganishwa na si rahisi kufutwa.

Naelewa unajua mengi ama umesimuliwa mengi kutokana na sources zako, lakini I think it is uncalled for kutumia informations ulizonazo kuchafua majina ya wazee waliolitumikia taifa hili ambao wala hatuoni mijimali waliyojilimbikizia kwa kutoshitakiwa na Mwalimu!

Let's be realistic, Barongo, Sir George na Mzee Maryogo ndio 'papa' walioachiwa kuendelea kunawiri na kuwachekeni?! Mzee Barongo, kama sikosei, ni marehemu na kafa maskini baada ya kulitumikia taifa hili kwa uwezo wake wote pamoja na elimu duni aliyokuwanayo. Tumeishasahau jinsi alivyokuwa akihamasisha Kilimo Bora? Sioni sababu ya msingi ya kuwataja na kuwachafua wazee hawa ambao walijitolea kulitumikia taifa letu kabla na baada ya Uhuru na hawakutumia nafasi zao kujilimbikizia mijimali. Wapo waliotamani, lakini tamaa zao hazikuweza kutimia kutokana na udhibiti na jicho kali la Mwalimu.

Nimetoa tabasamu kubwa kusoma jina la Kaisi! Nsa ni mwanajeshi, huenda alitumia taaluma yake bila utaratibu!

Awamu ya Kwanza kulikuwa na uozo gani mkubwa sana uliotendeka wa kuweza kulinganishwa na haya tuliyoyashuhudia ndani ya awamu zilizopita na tunayoyashuhudia hivi sasa, tunayojadili? Mind you, UTU aliokuwanao Mwalimu ulimfanya awe makini sana alipopelekewa tuhuma dhidi ya kiongozi ama mtu yeyote yule. Hakupenda kumuonea mtu. Kabla hajatoa uamuzi wa jambo lolote zito, alikuwa mwepesi kufanya utafiti wake binafsi kwa kuwatumia watu mbalimbali na kwa kupata mawazo ya watu makini walioaminika, wakiwemo viongozi wenziwe, nje ya mfumo. Kutokana na taarifa alizopata, aliweza pia kuwajua wafitini wa wakati huo. Kama alimwambia Kaisi awaachie aliowakamata, alikuwa na uhakika hao hawakuwa ‘wahujumu' uchumi wa wakati huo.

Mwalimu alimheshimu sana Sokoine na kuithamini sana kazi nzuri aliyokuwa akiifanya kuhusu uhujumu uchumi. Tusisahau kwamba hapa tunazungumzia Rais na Waziri Mkuu wake. Kabla ya Sokoine (Waziri Mkuu) kuchukua hatua yoyote ya aina hiyo lazima alishauriana na kukubaliana na (Rais) Mwalimu. Kwa maana hiyo, suala la kuwashughulikia wahujumu uchumi halikuwa la Waziri Mkuu pekee. Nashindwa kupata picha ya Sokoine kunung'unika pembeni kwamba alitaka Barongo na Sir George wakamatwe lakini Mwalimu amekataa bila sababu! Sokoine hakuwa mnafiki!

And, Mzee Maryogo of all the people! FEMS, huyu mzee atakufa maskini kwa sababu ya uadilifu wake. Pia atakufa maskini kwa sababu yeye ni 'maskini jeuri', neno ‘kujipendekeza' halimo kwenye vocabulary ya mzee Maryogo! Alipokuwa Utalii, aliweza kuokoa mamilioni ya fedha za Serikali kwa kumpelekea Mwalimu taarifa za kufichua njama za uhujumu. Ah! na marehemu Magombe naye alikuwa 'papa' wa uhujumu?!

Tuwasifie ma-Rais wetu na viongozi wa awamu zilizopita, awamu ya sasa na awamu zijazo kwa hatua wanazochukua kwa manufaa ya taifa letu. Mazingira ya miaka 40 iliyopita hayawezi kamwe kufanana na ya juzi, jana, leo, ama kesho. Tutakuwa hatumtendei haki Mwalimu aliyejitahidi kwa akili zake zote, kwa nguvu zake zote na kwa uwezo wake wote kutuwekea misingi bora ya uadilifu, tukaibomoa wenyewe.

FEMS, no hard feelings, ni kujaribu kukupunguza munkari dhidi ya Mwalimu na marehemu wengine!

- Mkuu nimeshangazwa sana kwamba na mtu mzito kama wewe unaweza kujiunga na hii michezo ya kugeuka geuka rangi it is very sad!, mara Mwalimu mara mafisadi, labda nikuulize na wewe serikali ya sasa imekukosea nini hasa au iliwakosea nini mababu zako?

- The ishu hapa sio Mwalimu, isipokuwa ni lazima kuangalia mizizi wa huu mti wa mafisadi umetokea wapi hawa mafisadi wote tulionao leo ni wanafunzi wa Mwalimu, sina shida ya kubishana na maneno ya Mwalimu lakini ni haki yangu kuangalia tatizo la ufisadi lilikoanzia, ninasema limeanzia kwa Mwalimu kwa sababu hawa mafisadi wote ni wanafunzi wa Mwalimu.

- Mwalimu ninamheshimu sana lakini haina maana nikwepe ukweli kuwa mafisadi tulionao leo ni wananfunzi wake, au? Hao uliojaribu kuwaosha hapo juu sina hata haja ya kurudia tena maana ni aibu waliyofanyia taifa, ndio maana Sokoine aliamua kujiuzulu baada ya kugundua kua Mwalimu hakuwa serious na kushughulikia papa, alitaka dagaa tu! Toafuti ya awamu ya kwanza na sasa ni kwamba under Mwalimu wote tulikuwa mabubu, lakini siku hizi kifua mbele wote tunasema tena wazi bila kuogopa, lakini ufisadi ni ule ule tu hakuanza leo ulianiza kwa Mwalimu!

Ahsante Mkuu ila I am very dis-appointed, maana sikutegemea! Ingawa umejitahidi sana lakini not me FMES! Yaani I am so dis-appointed kwamba sitarudi tena hii topic na wala sitakujibu tena!
 
FMES,
Kuwa mwanafunzi wa mtu haina maana kuwa utaiga au kufuata aliyokufundisha. Binadamu ndivyo tulivyo. Mwinyi alijiita kichuguu kwa kulinganishwa na Mwalimu lakini akawa wa kwanza kulizika azimio la Arusha na kutuletea azimio la Zanzibar. Na juzi tu katwambia kuwa azimio la Arusha lilikuwa ndoto. Huyu wa sasa anasema ukizungumzia azimio la arusha leo watakuona chizi. Ni kweli kulikuwepo na rushwa wakati wa utawala wa Mwalimu lakini kulikuwa pia na hofu ya kuogopa kugunduliwa na authorities na subsequent consequences. Lakini wakati wa Mwinyi lilikuwa jambo la fahari kuonekana unakula na wakubwa, wafanyibiashara etc. etc. Na huyu wa awamu ya tatu ndiyo kabisa akatumbukia kwenye limbwi la uozo wa rushwa na matokeo yake ndiyo hayo ya akina Zombe, Mahita na kukumbatiwa kwa mafisadi.
 
Tangu baada ya Yona na Mramba kushtakiwa kwa kosa la "Abuse of Power na kusababisha loss of 11 billion shilingi kwa Taifa" , nadhani itakuwa ni muda muafaka kujadlili Abuse of Power ni nini. Ni nani ni wahusika ? Kama wataalam wa wizara walimshauri Waziri wao nao hawahusiki? Je Mawaziri wana uwezo wa kuingia Mkataba wowote bila ridhaa ya Rais au Baraza la Mwaziri? Je
Kitendo cha Hakimu Henzeron ni mfano wa Abuse of Power?
 
Heri said:

Heri,

..kuna mahali nimesoma kwamba Mramba alipuuza ushauri wa TRA na kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni ya Alex Stewart. kwa upande mwingine Waziri wa Fedha anayo mamlaka ya kutoa msamaha wa kodi. nadhani sheria inaelekeza kwamba Waziri ndiye mwenye uamuzi wa mwisho ktk suala hili. Waziri wa Fedha halazimishwi na sheria kutafuta ridhaa ya Cabinet ktk kutoa misamaha ya kodi.

..swali ni kama Mramba alifuata vigezo alivyotakiwa kuvifuata ktk kutoa misamaha ya kodi. kama sijakosea msamaha wa kodi waliopewa hawa Alex Stuwart ulionekana kama wa kiholela-holela usiozingatia kanuni na taratibu zilizowekwa.

NB:

..has any one thought about who is going to be on the Prosecution/Defence witness[sp?] list. I dont this case can be decided without Commisioner of TRA, and PS of the Treasury, testifying.

..sijui kama wananchi mnakumbuka kesi ya John Magufuli na yule mwenye kituo cha mafuta kule Mwanza. nadhani ile ni clearer example of abuse of power. Magufuli alipuuza ushauri wa kisheria wa wataalamu wake mwenyewe. mahakama pia imeiagiza serikali kulipa mabilioni ya shilingi.

..pamoja na mambo ya vicarious liability, yaani serikali kulipa gharama za uzembe wa mtumishi[magufuli] wake, lakini nadhani huyu alipaswa kujiuzulu kwa hasara aliyotuingiza, na aibu ya kupatikana na hatia mahakamani.
 
UKAGUZI WA MAJENGO BENKI KUU NI USANII MWINGINE

Sasa hapo jameni kuna ukweli kuhusu stori ya mwandishi wa Nipashe ya jumapili. Hizi ni kampuni za kimataifa za kukagua mahesabu ya ujenzi kweli? Makao makuu ya MEKON yako uchochoroni kijitonyama nyumba ya kupanga hii kampuni na bwana Mkony wanababe wa kukagua Benki kuu kweli. Kipato chao kidogo kabisa, wanawezaje kuwa independent wakati total income yao ni kiduchu na wanataka kukagua benki kuu yenye mabilioni, je code of ethics za Engineers zinakubali hali kama hiyo?

Watakuwa prone for intimidation kani consulting fee toka Benki kuu kwa kazi hiyo ni kubwa mno.

Benki kuu/Gavana kaamua kuchagua kijikampuni kilicho very local, wenyekukimiliki wako hoi kwa poverty wakikimbiza vijitenda vya ujenzi hapa na pale. Kwa makusudi Gavana anataka aweze kuwa–control. Kwani wamejifunza baada ya kuajiri makampuni ya kimataifa yanakuwa ngangari na kuwashikia bango.

Mkuu Abura,
Usishangae, wakiwa katikati ya tenda watanunua ama kujenga Kwaliti Plaza yao. Tanzania hata upepo unazidisha hesabu, mambo ya dola 1=bilioni
 
Back
Top Bottom