Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,471
Zakumi,
Hapo umenena mkuu.
Kwenye Biblia kua sentenso inayosema "mwanadamu siku zake ni miaka 70"!
Sasa unajiuliza, je ukishajipatia kila kitu kama Johnson Lukaza alivyojichumia kabla hata ya kuwa na miaka 35, je ile mingine 35 iliyobakia atafanya nini?
Zaidi Uchotaji huu laiti ungekuw ani mara moja na utumike kama mtaji au msingi, bali huendelea milele.
Sasa kwenye uchotaji, kunakuja rushwa na kuvunja sheria nyingine ambako hufikisha kupotea au kutoweka kwa ushahidi muhimu.
Nikirudi kwenye nia halisi ya kusema kuwa hili ni changa la macho, kwa kina Jeetu Patel na Lukaza, sijui ni vipi tunaweza kuwashikisha adabu. Je hatuwezi kuwashitaki kwa kutumia ile sheria ya uhujumu uchumi na hata kuwafilisi?
Inapokuja kwa Yona na Mramba, hata ukiwaingiza kina Chenge, Lowassa, Karamagi, Meghji, Msabaha, Mgonja, Mboma na wengine, inakuwa kama ni tosha kuwamaliza kisiasa kwa kuwashitaki kwa uzembe, matumizi mabaya ya madaraka na kupotea kwa mali za umma kutokana na maamuzi mabovu na uongozi mbaya.
Nafikiri doa hili litanata kama gundi kuliko kutafuta wapi walificha hela!
Rev Kishoka:
Kama unatafuta mtaji basi ni lazima uwe na business plan. Na ukiwa na business plan basi ata pesa ya mkopo wa benki itakufanya uwe tajiri. Bottom line: watu hawana business plans na sio wafanya biashara.
Kama mchangiaji mmoja alivyosema wanasiasa wa bongo hawajuhi biashara. Na ukiwaondoa kwenye siasa, hawawezi kuishi.
Hivyo sita-entertain any idea kuwa mtu achukue pesa na akafanye biashara. Serikali ina wafanyakazi wengi na kila mmoja akisema achukue mara moja tu kama mtaji, hatutafika mbali. Na huu ndio mwanzo tulipoanzia, kila mtu alifikiri kuwa atachukua mara moja tu. Lakini imeonekana it's very easy kuichukua hiyo pesa kuliko kuifanyia kazi.
Binadamu wengi ni kama mkondo wa maji unaotiririka. Wakishaona njia nyepesi za kupita, basi ubunifu wa njia nyingine unakuwa hautumiki.
Kama ulisoma vitabu vya Abunuwasi, kuna jamaa alikuwa anapendwa na mfalme kwa sababu ya porojo zake na kila siku alikuwa anaalikwa kwenye meza ya chakula. Jamaa alijisahahu kufanya kazi. Taabu aliipata pale mfalme alipofariki na yeye kutotakiwa na warithi.
Watanzania wakiweza kuziba mapengo ya wizi wa mali za umma basi watu wataanza kuwa wabunifu wa njia zingine.