PreGE2025 Patrick Assenga avuliwa Uanachama CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Tawi la Msimbazi, Kata ya Tabata, Jimbo la Segerea mkoa wa kichama wa chama hicho wa Ilala mkoani Dar es Salaam kimemvua rasmi uanachama mwanachama wake Patrick John Assenga, kwa kile kilichoelezwa kupinga hadharani maazimio rasmi ya chama, yakiwemo ya ajenda ya No Reforms No Election.

Katika barua iliyoandikwa Mei 6, 2025 na Katibu wa Tawi, Jacob Roman kwenda kwa Assenga, chama kimesema Assenga ambaye ni mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, amevuliwa uanachama kwa kukiuka Katiba ya chama toleo la mwaka 2019, hasa Kanuni ya Maadili kifungu kidogo (iii) kinachokataza kupinga misimamo ya chama nje ya vikao.

“Chama kilikupa siku 14 kuwasilisha maelezo yako kwa njia ya maandishi hukufanya hivyo, Hivyo basi chama hakitasita kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yako kwa kosa ulilotenda makusudi ukijua unavunja katiba ya chama ya mwaka 2006 toleo la 2019 kipenele cha 03 kanuni ya maadili kifungu kidogo cha (iii)”, imeeleza sehemu ya barua hiyo.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Tawi limeeleza kuwa kwa msingi wa Ibara ya 5.4.3 ya Katiba ya CHADEMA, Assenga anakosa sifa ya kuendelea kuwa mwanachama, na hivyo amevuliwa rasmi uanachama wake kutokana na mwenendo unaodaiwa kuwa kinyume cha itikadi, falsafa, madhumuni, maadili na sera za chama.

Pia soma: Pre GE2025 - John Mrema avuliwa uanachama wa CHADEMA

“Pamoja na kushindwa kuwasilisha maelezo yako katika siku za nyongeza kamati tendaji ya Tawi imeketi na kupitia kwa umakini tuhuma zako ambazo ukiwa kiongozi hukupaswa kuzitenda, hivyo basi kwa kosa hili adhabu yake inaangukia Ibara ya 5.4 inayosema "kukoma kwa uanachama" ukiwa mwanachama wa CHADEMA mwenye usajili wa kadi No. cdme 11126 ya tarehe 22/06/2021 ambayo ni ya kidijiti”, imeeleza barua hiyo.

Chama kimetoa taarifa kuwa Assenga ana haki ya kukata rufaa katika ngazi ya juu ya chama kama ilivyoainishwa katika Katiba.

View attachment 3326318
Aende Chauma
 
Kazi nzuri. Hawa vibaraka wa CCM wakaifanye kazi yao vizuri sasa.
 
Ndio na alikua against na Chama nilishangaa sana kwakweli nikawaza labda ana tatizo la akili kwasasa
nitaitafuta --- wanasiasa wa aina hiyo ni wa kufurushwa tu
 
Swala la kwamba wanatumika lina Ushahidi au ni hisia tu?
Lipo wazi sana..

Yule wa pale Arusha alipopinga maamuzi ya mkutano mkuu wa CCM kumpitisha Samia kua mgombea urais mlimtishia maisha na kumfuta uanachama

Kila chama kina taratibu zake namna ya kukiendesha, Asenga aliitwa ili asikilizwe hakutokea akapewa muda wa Ziada bado hakutokea ulitaka abembelezwe yeye kama nani?
 
Lakini sio Kwa kukiuka katibana taratibu mliojiwekea wenyewe
Lissu alikiuka taratibu za chama kwa kufanya mikutano bila idhini ya chama, kuongea na wanachama bila idhini ya chama na nafasi yake hairuhusu kufanya hivyo, mbona hakufukuzwa?

Waliogawana pesa ambazo Lissu anasema ni za mama Abdul wamefukuzwa lini?

Wenje alipeleka rushwa kwa Lissu kwanini hafukuzwi?

Lissu anasema mbowe alitafuna pesa za chama, kwanini Mbowe hafukuzwi?
 
Back
Top Bottom