mafarisayoo
JF-Expert Member
- Oct 7, 2016
- 1,332
- 957
Wishavuliwa MUDA mrefu sanaCovid 19 vipi au wakubwa wale?
Wishavuliwa MUDA mrefu sanaCovid 19 vipi au wakubwa wale?
Labda Kama walivuliwa mawigiWishavuliwa MUDA mrefu sana
Hao umeona wanapinga msimamo wa chama wa REFORMS? Wako kimya kwahiyo watulie hivo hivoLissu alikiuka taratibu za chama kwa kufanya mikutano bila idhini ya chama, kuongea na wanachama bila idhini ya chama na nafasi yake hairuhusu kufanya hivyo, mbona hakufukuzwa?
Waliogawana pesa ambazo Lissu anasema ni za mama Abdul wamefukuzwa lini?
Wenje alipeleka rushwa kwa Lissu kwanini hafukuzwi?
Lissu anasema mbowe alitafuna pesa za chama, kwanini Mbowe hafukuzwi?
nitaitafuta --- wanasiasa wa aina hiyo ni wa kufurushwa tu
Sure mkuu huyu katibu anapaswa apate promosheni..Barua makini iliyoandikwa kitaalamu (professionalized letter) tena toka kwa kiongozi wa ngazi ya chini ya tawi tu...
Lakini barua za kina afande kamanda Jumanne Muliro (RPC - kanda maalumu DSM), ni hovyo, unprofessional utadhani viongozi hawa wenye dhamana kubwa kuongoza taasisi nyeti na muhimu, polisi kama hakwenda shule kabisa...
Kamanda mzima anaaindika "Father Charles Kitima alikuwa akipata kinywaji...🤔🤔🤔🤔"
Sielewi principles za vikao vyao kama kunakuminya maoni ya wajumbe.Kama nje ni madikteta hivi kwenye hicho kikao ndo angepewa uhuru wa kutoa maoni?
Kule kule 😆😆Wapi😀😀
Kwani hayahamia CHAUMA huyu?Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Tawi la Msimbazi, Kata ya Tabata, Jimbo la Segerea mkoa wa kichama wa chama hicho wa Ilala mkoani Dar es Salaam kimemvua rasmi uanachama mwanachama wake Patrick John Assenga, kwa kile kilichoelezwa kupinga hadharani maazimio rasmi ya chama, yakiwemo ya ajenda ya No Reforms No Election.
Katika barua iliyoandikwa Mei 6, 2025 na Katibu wa Tawi, Jacob Roman kwenda kwa Assenga, chama kimesema Assenga ambaye ni mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, amevuliwa uanachama kwa kukiuka Katiba ya chama toleo la mwaka 2019, hasa Kanuni ya Maadili kifungu kidogo (iii) kinachokataza kupinga misimamo ya chama nje ya vikao.
“Chama kilikupa siku 14 kuwasilisha maelezo yako kwa njia ya maandishi hukufanya hivyo, Hivyo basi chama hakitasita kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yako kwa kosa ulilotenda makusudi ukijua unavunja katiba ya chama ya mwaka 2006 toleo la 2019 kipenele cha 03 kanuni ya maadili kifungu kidogo cha (iii)”, imeeleza sehemu ya barua hiyo.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Tawi limeeleza kuwa kwa msingi wa Ibara ya 5.4.3 ya Katiba ya CHADEMA, Assenga anakosa sifa ya kuendelea kuwa mwanachama, na hivyo amevuliwa rasmi uanachama wake kutokana na mwenendo unaodaiwa kuwa kinyume cha itikadi, falsafa, madhumuni, maadili na sera za chama.
Pia soma: Pre GE2025 - John Mrema avuliwa uanachama wa CHADEMA
“Pamoja na kushindwa kuwasilisha maelezo yako katika siku za nyongeza kamati tendaji ya Tawi imeketi na kupitia kwa umakini tuhuma zako ambazo ukiwa kiongozi hukupaswa kuzitenda, hivyo basi kwa kosa hili adhabu yake inaangukia Ibara ya 5.4 inayosema "kukoma kwa uanachama" ukiwa mwanachama wa CHADEMA mwenye usajili wa kadi No. cdme 11126 ya tarehe 22/06/2021 ambayo ni ya kidijiti”, imeeleza barua hiyo.
Chama kimetoa taarifa kuwa Assenga ana haki ya kukata rufaa katika ngazi ya juu ya chama kama ilivyoainishwa katika Katiba.
View attachment 3326318
View attachment 3326414
Mrema ana njaaTangu Mrema aongee ule utumbo nimezarau sana kundi lake
Mawazo yao wapeleke kwenye vikao na sio kuanzisha nje ya chama kwa kivuli cha CDMMisingi ya demokrasia kuifuata yote ni kazi ngumu mno.maana demokrasia inataka hata wachache,wenye mawazo tofauti na ya wengi,nao waheshimiwe!
Mkuu hivi ukimfumania live mkeo anatafunwa na jirani yako ukimpa talaka ni kukosa busara? Hao watu wanatumika na CCM kuihujuma Chadema wazi wazi, wamediriki hata kufungua kesi mahakamani Chadema isimamishwe kufanya shughuli za kisiasa na mratibu wa hujuma hiyo ni Ofisi ya Msajili wa vyama kwa maelekezo ya CCM.Sidhani kama kuwafukuza chama ni busara.
Boniyai hayupo kwenye huo ujinga.Bado Bon
Ni sawa ila maazimio yakishafikiwa na vikao vya juu, kinachofuata ni utekelezaji wala si kuwa kinyume....Misingi ya demokrasia kuifuata yote ni kazi ngumu mno.maana demokrasia inataka hata wachache,wenye mawazo tofauti na ya wengi,nao waheshimiwe!
Then hii ni hatari....niliadhani wana mashiko. Wanapotaka chadema ifungiwe shughuli za kisiasa watafaitikaje sasa?Mkuu hivi ukimfumania live mkeo anatafunwa na jirani yako ukimpa talaka ni kukosa busara? Hao watu wanatumika na CCM kuihujuma Chadema wazi wazi, wamediriki hata kufungua kesi mahakamani Chadema isimamishwe kufanya shughuli za kisiasa na mratibu wa hujuma hiyo ni Ofisi ya Msajili wa vyama kwa maelekezo ya CCM.
😀😀😀Huu ndo wakati sahihi wa kutenganisha ngano na magugu.
Acha uvivu soma baru hapo juu alafu sema kama kuna kanuni/sheria haijafuatwaSielewi principles za vikao vyao kama kunakuminya maoni ya wajumbe.
Lakini je, nje waneonesha udikteta gani kwa wanachana ama viongozi wake?
Tuje upande 'B' je Ccm unaweza kuchongoroa mdomo wa kutoa maoni kipinzani nje ya utaratibu wa vikao wakakuacha?
Wale Ni akina baba wanaleta ruzuku/chakula mezani tone tone hawezi mfukuza covid 19.Covid 19 vipi au wakubwa wale?