Pata picha hii ingetokea hapa Tanzania

Pata picha hii ingetokea hapa Tanzania

Anaconda ana ukubwa kiasi gani?
Anaconda mkubwa ana uwezo wa kumeza binadamu,nguruwe mkubwa,mbuzi,kondoo,mamba picha ni kama huyo hapo.Ila kwa binadamu hata chatu wa huku kwetu ana uwezo huo akiwa anachonda.PNG mkubwa unajua kabla hajameza anavunja vunja mifupa kwa hivyo umbo linakuwa dog😵na picha mfano wa Anaconda mkubwa
 
Nyoka hapaswi kuachwa aendelee kuishi. Ndiyo chanzo cha laana kwa Adam na Eva
Nyoka anayeongelewa kwenye vitabu vya dini sio nyoka kama mnavyomjua huyu tulio naye ingekuwa hivyo kwenye gharika la Nuhu asingepandishwa kwenye Safina.Pia wanavyosema Eva alimdanganya Eva akala tunda la mti wa kati sio tunda la mti wa kati kama unavyojua wewe tunda.Vitabu vya dini vina mafumbo mengi.Na wanavyosema Bustani ya Eden je hiyo bustani iko wapi hadi leo mbona hatuioni.Mambo ya imani ni mbele kwa mbele tumche mungu tu
 
😂😂😂
"Hili joka si bure"
 
Anaconda mkubwa ana uwezo wa kumeza binadamu,nguruwe mkubwa,mbuzi,kondoo,mamba picha ni kama huyo hapo.Ila kwa binadamu hata chatu wa huku kwetu ana uwezo huo akiwaView attachment 1603914 mkubwa unajua kabla hajameza anavunja vunja mifupa kwa hivyo umbo linakuwa dog😵na picha mfano wa Anaconda mkubwa
We naona unatumia stori za vijiweni tu.

La, unaweza niwekea vipimo vya anaconda hapa?

Halafu chatu na anaconda wala huwa hawavunji mifupa kama unavyodai.

Tumia mtandao kufuta ujinga ulonao.
 
Chatu kukatisha barabara wilaya ya chato ni kawaida,ila chatu kuonekana posta sasa hiyo lazima iwe ajabu
 
Anaconda mkubwa ana uwezo wa kumeza binadamu,nguruwe mkubwa,mbuzi,kondoo,mamba picha ni kama huyo hapo.Ila kwa binadamu hata chatu wa huku kwetu ana uwezo huo akiwaView attachment 1603914 mkubwa unajua kabla hajameza anavunja vunja mifupa kwa hivyo umbo linakuwa dog😵na picha mfano wa Anaconda mkubwa
Contrary to myth, the snake does not crush the prey, or break its bones. However, several natural observations exist involving wild Anacondas that show broken bones in large prey. ... Further, multiple species of snakes have been shown to constrict with pressures higher than those shown to induce cardiac arrest.
 
We naona unatumia stori za vijiweni tu.

La, unaweza niwekea vipimo vya anaconda hapa?

Halafu chatu na anaconda wala huwa hawavunji mifupa kama unavyodai.

Tumia mtandao kufuta ujinga ulonao.
kama havunji mifupa anakuviringa kutafuta nini? nijibu kwanza hapo ndio maana anaitwa the constrictor soma maelezo haya mimi natoka sehemu zenye nyoka wakubwa misitu ya CONGO najua ninachoongea sitokei Kariakoo.Nyoka wenye sumu hawahitaji kuvunja vunja kitu maana wakiuma wanasubiri kiumbe kizimie wameze nyoka wote wasio na sumu kama chatu na anaconda inabidi watumie mbinu ya constriction
How do snakes kill humans?
They can reach lengths of more than 10m (32ft) and are very powerful. They attack in an ambush, wrapping themselves around their prey and crushing it - squeezing tighter as the victim exhales. They kill by suffocation or cardiac arrest within minutes
 
Watu wangeishukuru awamu ya tano kwa juhudi za kumuuua chatu
 
Watanzania tuna shida sana...yaani akionekana nyoka tu lazima wamuue.

Kuna siku kanyoka kadogo kalikatiza kwenye eneo la biashara, nikachukua fimbo nikakasogeza ili kaende kwenye vichaka. Aisee nilimaindiwa kinoma, wadau walikatafuta wakakaua.
 
Huyo kwenye video ni chatu wa Amerika ya Kusini, ajulikanaye kama anaconda.

Inadaiwa kuwa hapo ni kwenye mji wa Porto Velho, nchini Brazil.

Joka lilikuwa linavuka barabara na watu wakasimamisha magari yao na kuliacha livuke kwa amani na utulivu na bila kulidhuru wala kuliua.

Wengine wakashuka toka kwenye magari yao na kulipiga picha za kawaida na video kwa kutumia simu zao.

Hatimaye joka likamaliza kuvuka na likatokomea kwenye kichaka.

Hiyo ingetokea hapa Tanzania....hahahaa!

Si ajabu yangesemwa mengi sana.

Kwanza, nadhani lingeuliwa. Kama si kwa kukanyagwa na gari basi kwa kupondwa mawe.

Ingiza sasa na zile imani za kijinga.

Si ajabu kuna watu ambao wasingelala usiku kwa kuamini kuwa limetumwa.

Watu wangehaha kwenda kwa waganga [emoji1787] ili kujua kulikoni!

Wakati hakuna lolote zaidi ya ecosystem kuwa kazini.

ushasema ni america ya kusini
 
Binafsi ningemuua na kuchukua magamba yake. Moyo maini na minofu mingine ningeuzia wachina. Nisingemwacha ningemkanyaga na tairi kisha nakamata break kwa kichwa.
 
Huyo kwenye video ni chatu wa Amerika ya Kusini, ajulikanaye kama anaconda.

Inadaiwa kuwa hapo ni kwenye mji wa Porto Velho, nchini Brazil.

Joka lilikuwa linavuka barabara na watu wakasimamisha magari yao na kuliacha livuke kwa amani na utulivu na bila kulidhuru wala kuliua.

Wengine wakashuka toka kwenye magari yao na kulipiga picha za kawaida na video kwa kutumia simu zao.

Hatimaye joka likamaliza kuvuka na likatokomea kwenye kichaka.

Hiyo ingetokea hapa Tanzania....hahahaa!

Si ajabu yangesemwa mengi sana.

Kwanza, nadhani lingeuliwa. Kama si kwa kukanyagwa na gari basi kwa kupondwa mawe.

Ingiza sasa na zile imani za kijinga.

Si ajabu kuna watu ambao wasingelala usiku kwa kuamini kuwa limetumwa.

Watu wangehaha kwenda kwa waganga 🤣 ili kujua kulikoni!

Wakati hakuna lolote zaidi ya ecosystem kuwa kazini.

Mnaliacha dude hatarishi kama hilo ili 'mvumbue' nini, eti? Ningeshaliulia mbali, mizaha yenu hii ya kucheka na visivyochekewa mwishowe mnasababisha majangatu.
 
kama havunji mifupa anakuviringa kutafuta nini?
Anajivingirisha ili aweze kukukaba vizuri. Ni anakupuga kabali. Ushawahi kupigwa kabali wewe?

Hiyo kabali inakata mzunguko wa damu. Mzunguko wa damu ukikatika, moyo unashindwa kufanya.

Moyo ukishindwa kufanya kazi, kwisha habari yako. Unakufa kwa mshtuko wa moyo au cardiac arrest.

Ukishakufa, ndo chatu anaanza kukula sasa.

Hilo ndo lengo la hiyo kabali.

Chatu hali chakula chake kikiwa hai.

Na katika kukupiga hiyo kabali, havunji mifupa. Hizo habari za kuvunja mifupa ni hekaya za abunuasi tu.

Hata wewe unaweza ukafanya kautafiti kako kadogo uone kama ni kweli au la.

nijibu kwanza hapo ndio maana anaitwa the constrictor
Wewe naona hata lugha ya Kiingereza imekutupa.

Chatu wanaitwa constrictors kwa sababu wanaua mawindo yao kwa njia ya asphyxiation.

Constriction maana yake ni kubana.

Wao wanakubana. Kukubana huko kunakata mzunguko wa damu. Mzunguko wa damu ukikatwa, unakosa na oksijeni.

Ukikosa oksijeni, moyo unashindwa kufanya kazi.

Moyo ukishindwa kufanya kazi, unakufa.

soma maelezo haya mimi natoka sehemu zenye nyoka wakubwa misitu ya CONGO najua ninachoongea sitokei Kariakoo.Nyoka wenye sumu hawahitaji kuvunja vunja kitu maana wakiuma wanasubiri kiumbe kizimie wameze nyoka wote wasio na sumu kama chatu na anaconda inabidi watumie mbinu ya constriction
Maelezo unayonambia niyasome, wewe mwenyewe hujayaelewa.

Tumia teknolojia iliyo karibu yako kufuta ujinga ulonao!

How do snakes kill humans?
They can reach lengths of more than 10m (32ft) and are very powerful. They attack in an ambush, wrapping themselves around their prey and crushing it - squeezing tighter as the victim exhales. They kill by suffocation or cardiac arrest within minutes
Maelezo uloyaleta mwenyewe yanasema “they kill by suffocation or cardiac arrest.

Ni wapi panasema they kill by breaking the bones of their prey?

Na kuna sababu kwa nini chatu haui windo lake kwa kuvunja mifupa.

Kama una akili utafanya utafiti ujue ni kwa nini hawaui kwa kuvunja mifupa ya windo....
 
Back
Top Bottom