Pasco wa JF aje Hapa!


Mmewasahau Rejao na Ritz. Huyu wa pili aliahidi kwamba CDM Arumeru Mashariki ikishinda anatembea kama alivyozaliwa mtaani. Tumtafute athibitishe

Naona ushindi wa Chadema unakuchanganya, ebu weka hiyo post yangu niliyosema hayo maneno kwenye uchaguzi wa Arumeru.
 
Mkuu,
Umeshaenda kuedit nini?...angalia usiadhirike ukubwani broda!

Hayo maneno yalikuwa kule Uzini, sasa Chadema mwenzako kwa furaha naona kaamua kunizingua...naona leo ni sherehe tu, mkuu Pasco kateleza jamani ndio ubinadamu sio kila kitu unachosema kinakuwa sahihi humu Jamvini tumeongea mengi lakini watu wa Arumeru Mashariki ndio wamechagua mbunge wao.
 
Adimit defeat is not a sportsman...Congratulate Chadema.
Ha ha haa eti itakuwa kama Uzini na Igunga.....tuliwaambia AR sio Igunga.

Pale mwanzo ulikomaa na wazee wa Kishili wamekusaidia nini, afadhali mwenzako Rejao hadi sasa bado anasubiri kura za vijijini hajaamini kama kura hazijatosha.
 

leo safi, respect mkuu, yale yalikuwa maneno yakishabiki tu, sawa na makocha wa simba na yanga wakijigamba kabla ya mechi kuanza sio?
 
Ritz leo uko mtulivu sana hadi raha aisee!
Mkuu, wewe ni mwanamageuzi, umeguka mwili mzima, bado MKIA tu!
Hamia Airtel mkuu!
 

Mkuu Ritz kumbe upo mzee mwenzangu,ulijificha wapi kiongozi?teh teh teh!kuhusu hiyo kauli ya kutembea uchi hata mimi nakutetea,ulisema uzini na wala si Arumeru!naona kamanda mwenzetu kateleza kidogo!
 
Jamani mbona tunapoteza nguvu kutafuta wafu kati ya walio hai?
Tusherehekee ushindi bwana.......................... hao tusubiri tu tukishatangaziwa mazishi tukasaidie kumwaga udongo.
Hongera sana wana Arumeru, Lizaboni, Kirumba na Kiwira. I am very proud of you all.
 
Pasco, yako wapi?
Hii si aibu kwa umri wako mzee mwenzangu?
Mtu kama wewe, kwa kazi yako hutakiwi kuwa mnafiki, maana unadeal na Media...umeishushia sana hadhi PPR

Pasco hajaishushia hadhi PPR bali ni PPR imejishushia hadhi kwa kuwa na mtu kama Pasco. Nafikiri ni harakati zake za kupata ajira Synovate.

Shame upon him
 
Yako mengi sana!
Yaje hapa tuyarambe...kudadadeki.

Ninachompendea Pasco ni kwamba anafanana kila kitu na Lusinde ila tofauti yake ni kwamba Pasco anajitahidi sana kuficha tabia zake za kuzaliwa hivi mvionavyo ni viashiria tuu vya tabia zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…