Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,988
Jamani hii ni siasa tu. Tusipeleke vitu vikawa hadi vionekane kuwa ni personal. Kwenye haya mambo kuna passion (hisia kali) na wakati mwingine watu wanaweza kuzichukua hizo hisia na kuzifanya kuwa ni za binafsi. Kaitka wakati wa kampeni na hizi siasa watu huweza kuwa pande mbili tofauti tena kwa ukali sana lakini wakati wote tukumbuke kuwa ni siasa. Tatizo kuwa tumeanza kujenga tabia - ya aibu - kuwa kwa vile watu wako pande mbili tofauti (pro-ccm and pro-cdm) basi ni lazima wawe na uadui wa kuchukiana.
Tusipoangalia sisi sote hatutakuwa tofauti na wale waliokata wabunge wa CDM mapanga au ambao wanapigana na kuumizana kwa sababu za kisiasa tu. Tujifunze kupingana bila kupigana, kulumbana bila kuumana na kukosoana bila kukosana. Kama sisi hapa hatuwezi kutofautiana bila kufanyana duni basi hatuna tofauti na watu wengine ambao hawana wigo mpana wa kushirikiana namna hii.
So Pasco alichukua upande ambao historia imehukumu ni wa makosa; so what? So kina Ritz, Ribosome na wengine walishabikia sana CCM na kubezana sana CDM so what? it is JUST POLITICS! kwa kawaida inatakiwa tufike mahali baada ya mambo haya siasa kuweza kucheka, kuchekeana na kuchekeshana tusubiri mtanange mwingine. NDIVYO tutakavyozidi kukomaa katika demokrasia. BInafsi nilitarajia watu waliochekeshwa na Pasco wangeamua kumtafuta ili kumkaribisha kunywa naye bia na kucheka pamoja.
Vinginevyo, tutaanza kutengeneza visasi visivyo na sababu.