Pasaka: Asili, umuhimu wake na tamaduni zetu

Pasaka: Asili, umuhimu wake na tamaduni zetu

Pasaka njema kwa wanaoiamini!

Je neno sahihi linalomaanisha sikukuu hii ni lipi,easter au passover. Kumekua na mabishano mengi sana hapa,wengine wakisema easter ni sherehe za kipagani na hazina uhusiano na sherehe ya pasaka iliyokua imeamriwa na Mungu.

Na kama ndio hivyo ni kwa nini neno ester ndio linatumika badala ya passover?

Naomba kujuzwa tofauti ya haya mambo na nini kimepelekea neno passover halitumiki badala yake tunatumia easter.

Karibuni sana.
Ukitaka mwaka ambao yesu alifufuka mwaka 33 baada ya kuzaliwa kwake
 
Mimi huwa najiuliza kila siku.
Inakuwaje watu washeherekee siku ya KUFA mungu wao!??

Mi kwa kweli ukristo wangu unaanza kuporomoka.

Cc picchu
Utaporomoka kwa ujinga wako tuna huzuni na kifo na furaha na ushindi wa kifo yaani ufufuko sasa wapi sherehe ya kufa MUNGU wetu

Nenda ukafundishwe kujilpua
 
Ukichunguza utaona mengi.Ila ni ajabu.Hata Krismasi haiko kwenye Biblia lakini inasherehekewa! Si makanisa yote yanakubali vitu ambavyo haviko kwenye Biblia.Mimi ni Mkristo ILA Ista, naiona kama siku zingine tu.
Mkuu huu mwez Wa nisani n sawasawa na mwz wa ngap ktk kalenda ya kawaida
 
Kwa kifupi:Kwa ninachofaham Yesu alipokua akiishi duniani wayahudi waliendelea na taratibu zao za kawaida. Pasaka ilikua moja ya sikukuu zao walipokumbuka kutoka utumwani -"Exodus."Kwa bahati nzuri au mbaya Yesu baada ya kufa nae alifufuka siku ile ile ya ile sherehe. Inaruhusiwa kunisahihisha if nimekosea
Ikiwa hvyo ndivyo je, waisrael wao pasaka yao walikuwa wanafanya mwezi Wa ngap?
 
Pasaka njema kwa wanaoiamini!

Je neno sahihi linalomaanisha sikukuu hii ni lipi,easter au passover. Kumekua na mabishano mengi sana hapa,wengine wakisema easter ni sherehe za kipagani na hazina uhusiano na sherehe ya pasaka iliyokua imeamriwa na Mungu.

Na kama ndio hivyo ni kwa nini neno ester ndio linatumika badala ya passover?

Naomba kujuzwa tofauti ya haya mambo na nini kimepelekea neno passover halitumiki badala yake tunatumia easter.

Karibuni sana.

Biblia Inasema
Nini Kuhusu Ista?
Jibu la Biblia
Sherehe ya Ista haiungwi mkono na Biblia.
Ukichunguza historia, utaona maana halisi ya Ista
—ni desturi inayotegemea maadhimisho ya kale
ya kusheherekea uwezo wa kuzaa. Fikiria mambo
yafuatayo.
1. Jina: Kitabu Encyclopædia Britannica
kinasema hivi: “Chanzo cha jina la
Kiingereza Easter hakijulikani; katika karne
ya nane, kasisi Mjerumani, Venerable Bede,
alitoa jina hilo kutoka kwa mungu wa kike
wa Wajerumani wa majira ya masika
aliyeitwa Eostre.” Vitabu vingine
vinahusianisha jina hilo na Astarte, mungu
wa kike wa uzazi wa Wafoinike ambaye
anajulikana kama Ishtari kwa Wababiloni.
2. Sungura: Mnyama huyo ni ishara ya
uwezo wa kuzaa “iliyokuwa ikitumiwa
zamani katika sherehe za wapagani wakati
wa majira ya masika huko Ulaya na
Mashariki ya Kati.” —Encyclopædia
Britannica.
3. Mayai: Kulingana na kamusi Funk &
Wagnalls Standard Dictionary of Folklore,
Mythology and Legend, kutafuta mayai ya
Ista ambayo inasemekana kuwa yaliletwa
na sungura wa Ista, “si mchezo wa watoto
tu, bali ni masalio ya sherehe za kale za
uwezo wa kuzaa.” Watu wa tamaduni
fulani huamini kwamba yai la Ista
lililopakwa rangi “lina nguvu za kimuujiza
za kuleta furaha, ufanisi, afya, na ulinzi.”—
Traditional Festivals .
4. Mavazi mapya ya Ista: “Ilionwa kuwa
kukosa adabu na hivyo bahati mbaya
kumsalimu mungu wa kike wa Skandinavia
wa Majira ya Masika, au Eastre, ikiwa mtu
hakuwa amevalia nguo mpya.”— The Giant
Book of Superstitions.
5. Maombi ya kucha kwa jua:
Yamehusianishwa na sherehe za waabudu
wa kale wa jua “zilizofanywa mwanzoni
mwa majira ya masika ili kulikaribisha jua
na uwezo wake mkubwa wa kuvipa uhai
tena vitu vyote vilivyokuwa vikikua.”—
Celebrations—The Complete Book of
American Holidays.
Kitabu The American Book of Days kinaeleza
vizuri chanzo cha Ista kinaposema: “Hakuna
shaka kwamba Kanisa katika siku za mapema
lilichukua desturi za zamani za kipagani na
kuziingiza katika Ukristo.”
Biblia inaonya kuhusu kumwabudu Mungu kwa
kufuata mapokeo au desturi ambazo
zinamchukiza. ( Marko 7:6-8 ) Barua ya Pili kwa
Wakorintho 6:17 inasema hivi: “‘Mjitenge,’ asema
Yehova, ‘na mwache kugusa kitu kilicho najisi.’”
Ista ni sikukuu ya kipagani na wote wanaotaka
kumpendeza Mungu wataiepuka.
 
Licha ya tarehe kubadirika lkn najiuliza inakuaje wakatoliki wanajua pasaka hadi 2020 huko zitaangukia tarehe gani.
Na inakuwaje waislam pia wanajua kama huu mwaka mfungo utaanza mwez wa 06???na wanajua mpaka mwaka 2090 mwez utaokuwa wa mfungo
 
ungeanza kujiuliza kwa nini idd inabadilika balika miezi?
Eid na Chrismas ziko straight foward mkuu. Chrismas iko fixed kila Decemba25, Eid kila mwezi mwandamo ukichomoza tayari, nayo siyo tarehe ya kuzaliwa mtu. Na hufuata kuandama kwa mwezi ambapo huwa ni siku 29 au 30.Na ni rahisi kujua Eid ya mwakani itaangukia lini kwa sababu mwezi mwandamo kwa mwaka hupishana kwa siku 11,sababu yake ni kuwa tarehe ya kawaida, miez 7 ina siku 31,miezi 4 ina siku 30 na mwez mmoja una siku 28/29!Sasa kwa mwezi mwandamo huwa na siku 30 au 29 tu. Hivyo inakuja utofauti wa siku 11. Ndiyo maana kama Eid mwaka jana ilikua ni 25-7-2015,basi mwaka huu INAWEZA kuwa 14 au 13-7-2016!

Sasa mshangao ni tarehe ya Pasaka kubadilika wakati kalenda kama ni kifo au kuzaliwa ni fixed. Kadri ya fafanuzi zilizotolewa, zinashindwa kubainisha tofauti hii ya kimantiki. Kuna walakini sehemu. Halafu kinachoshtusha ni ile kusema RC, kana kwamba RC ndiyo reference ya Mambo ya Ukristo pekee.
 
Mkuu hii sherehe haijawekewa tarehe ila imewekewa siku. (Ijumaa -jpili) hivyo tarehe zake zitabadilika kila mwaka.
X mas imewekewa tarehe hivyo siku ya wiki itabadilika ila tarehe haibadiliki. Pascal imewekewa siku maalum ya wiki hivyo tarehe itabadilika kila mwaka.
Hivyo uhalisia wa tarehe haupo kabisa. Labda tukio hilo linaloadhimishwa halikua na tarehe sahihi ambayo watu wa kumbukumbu za kalenda, tarehe na mambo ya kale hawana uhakika bali ni range ya week kati ya mwishoni mwa March na mwanzoni mwa April?
 
2016 ni kwasababu tumeanza kuhesabu tangu kuzaliwa kwa simple.

Historical miaka inapungua kuelekea kuzaliwa Yesu mpaka zero ambao ndiyo center ya moja baada ya kuzaliwa yesu.
 
2016 ni kwasababu tumeanza kuhesabu tangu kuzaliwa kwa simple.

Historical miaka inapungua kuelekea kuzaliwa Yesu mpaka zero ambao ndiyo center ya moja baada ya kuzaliwa yesu.
Una Ushahidi gani kuwa Yesu alizaliwa miaka 2016 iliopita?

Leta andiko. Acha blah blah.
 
Una Ushahidi gani kuwa Yesu alizaliwa miaka 2016 iliopita?

Leta andiko. Acha blah blah.
We boya umejiandaa kubisha eti..! Wewe hapo ulipo una miaka mingapi? Ama ulizaliwa mwaka gani? Jiulize mwaka wowote uliozaliwa huo mwaka umeanza kuhesabiw kutoka wapi?
 
We boya umejiandaa kubisha eti..! Wewe hapo ulipo una miaka mingapi? Ama ulizaliwa mwaka gani? Jiulize mwaka wowote uliozaliwa huo mwaka umeanza kuhesabiw kutoka wapi?

Nimezaliwa 1380. Na nina umri wa miaka 57.

Sasa nipe ushahidi wa Andiko linalosema Yesu kazaliwa Miaka 2016 iliopita.

Maneno ya mipasho peleka jikoni
 

Attachments

  • Screenshot (7).png
    Screenshot (7).png
    64.7 KB · Views: 73
Eid na Chrismas ziko straight foward mkuu. Chrismas iko fixed kila Decemba25, Eid kila mwezi mwandamo ukichomoza tayari, nayo siyo tarehe ya kuzaliwa mtu. Na hufuata kuandama kwa mwezi ambapo huwa ni siku 29 au 30.Na ni rahisi kujua Eid ya mwakani itaangukia lini kwa sababu mwezi mwandamo kwa mwaka hupishana kwa siku 11,sababu yake ni kuwa tarehe ya kawaida, miez 7 ina siku 31,miezi 4 ina siku 30 na mwez mmoja una siku 28/29!Sasa kwa mwezi mwandamo huwa na siku 30 au 29 tu. Hivyo inakuja utofauti wa siku 11. Ndiyo maana kama Eid mwaka jana ilikua ni 25-7-2015,basi mwaka huu INAWEZA kuwa 14 au 13-7-2016!

Sasa mshangao ni tarehe ya Pasaka kubadilika wakati kalenda kama ni kifo au kuzaliwa ni fixed. Kadri ya fafanuzi zilizotolewa, zinashindwa kubainisha tofauti hii ya kimantiki. Kuna walakini sehemu. Halafu kinachoshtusha ni ile kusema RC, kana kwamba RC ndiyo reference ya Mambo ya Ukristo pekee.
Siku na tarehe
Mbali tu na kujua Ukumbusho unapaswa kuadhimishwa mara ngapi, kielelezo ambacho Yesu aliweka kinatusaidia kuelewa siku na tarehe ya Ukumbusho huo. Kulingana na kalenda ya Biblia, alianzisha mwadhimisho huo Nisani 14, 33 W.K. baada ya jua kutua. (Mathayo 26:18-20, 26) Tunaendelea kuadhimisha Ukumbusho tarehe hiyohiyo kila mwaka kama tu Wakristo wa karne ya kwanza walivyofanya.*

Ingawa Nisani 14, 33 W.K. ilikuwa siku ya Ijumaa, inawezekana tarehe hiyo kuwa siku tofauti kila mwaka. Badala ya kufuata kalenda ya sasa ya Kiyahudi, tunatumia kanuni ileile iliyotumiwa wakati wa Yesu ili kujua siku ambayo tarehe ya Nisani 14 itaangukia.
KWA NINI WAISRAELI WALISHEREHEKEA PASAKA?
3, 4. Ni nini kilichotukia kabla ya Pasaka ya kwanza?

3 Ulimwenguni pote, mamilioni ya watu wasio Wayahudi wanajua kwa kadiri fulani kilichotukia kabla ya Pasaka ya kwanza. Huenda walisoma kitabu cha Biblia cha Kutoka, walisimuliwa au kuona sinema inayohusu tukio hilo.

4 Baada ya Waisraeli kuwa watumwa kwa miaka mingi huko Misri, Yehova alimtuma Musa na Haruni ndugu yake, wakamwambie Farao awaachilie huru watu Wake. Mtawala huyo wa Misri mwenye kiburi alikataa kuwaruhusu Waisraeli waende zao, hivyo Yehova akaipiga nchi ya Misri kwa mfululizo wa mapigo yenye kuangamiza. Mwishowe, Mungu alileta pigo la kumi lililoua wazaliwa wote wa kwanza Wamisri, na hivyo Farao akawaacha Waisraeli waende zao.—Kut. 1:11; 3:9, 10; 5:1, 2; 11:1, 5.

5. Waisraeli walipaswa kujitayarishaje ili waachiliwe huru? (Tazama picha kwenye ukurasa wa 17.)

5 Hata hivyo, Waisraeli walipaswa kufanya nini kabla ya kuachiliwa huru? Ulikuwa wakati wa majira ya kuchipua ya mwaka wa 1513 K.W.K., katika mwezi wa Kiebrania wa Abibu, uliokuja kuitwa Nisani, wakati ambapo saa za mchana hulingana kwa urefu na saa za usiku.* Mungu alisema kwamba katika siku ya kumi ya mwezi huo, Waisraeli walipaswa kuanza kujitayarisha kufanya mambo fulani Nisani 14. Siku hiyo ilianza jua lilipotua kwa kuwa kulingana na Waebrania, siku ilianza na kwisha jua lilipotua. Katika Nisani 14, kila familia ilipaswa kuchinja kondoo dume (au mbuzi), kuchukua sehemu ya damu na kuipaka juu ya miimo ya mlango na sehemu ya juu ya mlango wa nyumba. (Kut. 12:3-7, 22, 23) Kila familia ilipaswa kumla mwana-kondoo aliyechomwa kwa moto, mboga, na mkate usiotiwa chachu. Malaika wa Mungu angepita katikati ya nchi na kumchinja kila mzaliwa wa kwanza wa Misri, lakini Waisraeli waliotii wangelindwa, kisha Farao angewaruhusu waende zao.—Kut. 12:8-13, 29-32.

6. Watu wa Mungu walipaswa kuendelea kuionaje Pasaka?

6 Hivyo ndivyo ilivyotukia, na Waisraeli walipaswa kuendelea kukumbuka ukombozi wao. Mungu aliwaambia hivi: “Siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaisherehekea ikiwa sherehe kwa Yehova katika vizazi vyenu vyote. Nanyi mtaisherehekea kama sheria mpaka wakati usio na kipimo.” Mwadhimisho huo uliofanywa siku ya 14 ulifuatiwa na sherehe ya siku saba. Nisani 14 ndiyo iliyokuwa siku ya Pasaka, lakini siku zote nane za sherehe hiyo ziliitwa pia Pasaka. (Kut. 12:14-17; Luka 22:1; Yoh. 18:28; 19:14) Pasaka ilikuwa mojawapo ya sherehe rasmi (“sikukuu,” Union Version) ambazo Wayahudi walipaswa kusherehekea kila mwaka.—2 Nya. 8:13.

7. Yesu alianzisha nini wakati wa Pasaka ya mwisho halali?

7 Yesu na mitume wake walisherehekea Pasaka kila mwaka kwa sababu walikuwa Wayahudi na hivyo walikuwa chini ya Sheria ya Musa. (Mt. 26:17-19) Mara ya mwisho waliposherehekea Pasaka, Yesu alianzisha mwadhimisho mpya ambao wafuasi wake wangekumbuka kila mwaka, yaani, Mlo wa Jioni wa Bwana. Lakini walipaswa kuuadhimisha siku gani?
 
Heri za Pasaka kwa wahusika wote.

Swali langu ni moja tu, Kumbukumbu zangu zipo sahihi sana na toka 2013 huwa nasikia hiki kitu kuwa yesu alikufa miaka 2000 ilitopita, hamna namba yaani mwaka kamili ambao yesu alikufa? Au rekodi haziko sawa?

Kila mwaka wakati wa eidha xmas au pasaka, kwa xmas husema kumbukumbu za kuzaliwa yesu miaka 2000 iliyopita na pasaka pia husema kumbukumbu za kufufuka kwa yesu miaka 2000 iliyopita, hii miaka 2000 imekuwa ikitajwa toka miaka ya nyuma, je ni lini itakuwa miaka 2050 au miaka 3000?

Shukrani natanguliza.
Yesu alizaliwa tarehe 1/10/02 BC yaani tarehe 1 Mwezi wa 10 mwaka wa 2 BC .Ikiwa Yesu hangekufa sasa hivi angekuwa na miaka 2016 na miezi 6.Hivyo Yesu alizaliwa miaka 2016 iliyopita.
 
Nimesoma kutoka sijaelewa kabisa uhusiano wake na pasaka.....

Na bado nasubiri maana kabisa ya hii sikukuu ni kuadhimisha kifo cha yesu au ina mambo mengine

Mkuu endelea tu kusoma ila kiukweli utaambulia patupu ila tu kama utaamua kufuata kama kondoo machinjoni
 
Back
Top Bottom