Pasaka: Asili, umuhimu wake na tamaduni zetu

Pasaka= Passover

Passover- kupita juu ya..

Asili ya Pasaka, ilianza enzi za Wanaisrael, kipindi kile wakiwa utumwani Misri, chini ya utawala Wa Farao..

Mungu alimwagiza Malaika kuwaangamiza watoto wote wa Wana Wa Misri...ila, Mungu akamwagiza Malaika, kila Nyumba anayoishi Muisrael, apake damu juu ya mlango, ndio ikazaliwa neno "Passover"

Kwahiyo, kitendo kile kiliitwa Ukombozi kupitia damu iliyowekwa juu ya milango yao( wana Wa Israel).

Yesu Kristo, alitumia falsafa hiyo. Alitumia damu yake kama ukombozi kwa kizazi cha agano jipya.
 
Sasa kama ilianza kabla ya YESU inakuwaje inaunganishwa na Ufufuo wa YESU ??? Jamani Mbona mnatudanganya ??
 
Heri ya Pasaka,

Pokea hili japo ni wiki zimepita toka kuiadhimisha.

Naomba maoni yenu juu ya uelewa wangu juu pasaka na easter.

Pasaka ni sikuku ya kiyahudi kwa asili, ilikua sikukuu ya ukombozi toka kwa Wamisri. Kisa cha jina pasaka ni malaika mtoa roho alipitia kila nyumba Misri na kufanya yake alipoona nyumba haijapakwa damu kwenye miimo ya nyumba (pass over).

Pili ni kuvushwa kwenye bahari ya shamu. Hii sherehe iliambatana na sikuku ya mavuno.Tukio la pasaka /sikuku ya mavuno ilikua ni ijumaa kiasili kabla ya siku ya sabato/pumziko. (Yesu alikula pasaka pia kabla ya kifo chake).

Hivyo sikuku ni Ijumaa kwa maana ya sikuku kiyahudi.Wakristo husheherekea juma pili kwa sababu ya kufufuka mtume Yesu ambayo ni jumapili, lengo kusherekea ushindi /kushinda kifo, kutimiza maandiko kwamba atafufuka, hivyo asinge fufuka basi kulikua hakuna haja ya kusherekea siku hiyo. Hivyo kwakupigwa kwake wakristo wamepona.

Pasaka halina mbadala wa jina hilo. Pasaka ni pasaka tu iwe ni kingereza ni pasaka na kichina na nk. linatamkwa hivyo hivyo.

Kwanini easter?

Easter ni sherehe ya tamaduni za watu wa ulaya kwa Mungu wao ambae alikua ni Mungu wa uzazi na rutuba. (Mungu mke) hivyo husherekea pale mazao yao yanapokua yamechanua vizuri hasa kipindi hiki kwao.

Pasaka ni kufa na kufufuka kwa Yesu Masia.
Easter ni shukurani kwa Mungu mke ambae si sio wakristo.

Tunasherekea Pasaka ama Easter?

Kufanana kwa sikuku ya wapagani hakuiondolei maana halisi ya pasaka, (huwezi sogeza sikukuu ya uhuru kisa wengine washerekea siku hiyo kitu kingine kabisa...).
Wasabato na Mashahidi wa Jehova sijui lama mna sherekea hii sikuku, kasio nielekezeni ni kwanini?

Pendekezo langu;

Kama unamaanisha Pasaka mtakie mwenzio Pasaka na kama unataka kumtakia Easter mtakie Easter na sio Pasaka.
 
Huu ni ukweli ambao viongozi,wa dini hawatataka uujue,

Wakatoliki wanadai kwamba pasaka ni sherehe ya ufufuo wa Kristo, lakini siyo kweli. Kwa sababu kama kweli pasaka ni kusherehekea ufufuo wa Kristo wangekuwa na tarehe moja tu ya kusherehekea ufufuo huo kila mwaka, lakini siyo hivyo, mwaka mmoja watasherehekea tarehe tofauti, na mwaka mwingine tarehe tofauti. Je katika nchi yetu ya Tanzania hakuna waliokufa ambao hukumbukwa na taifa? Bila shaka wapo! Kwa mfano, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, tarehe ya kifo chake ni moja tu katika mwezi aliofariki, yaani tarehe 14/October, siyo kwamba mwaka huu tarehe 14, mwaka kesho tarehe 20, mwaka kesho kutwa tarehe 2, kama pasaka inavyosherehekewa leo, haijulikani kuwa ufufuo huo wa Yesu unasherehekewa tarehe gani kila mwaka. Je kifo si kama tu kuzaliwa? Je kwanini basi wasingeifanya Pasaka kama vile Krisimasi ambayo husherehekewa kila mwaka tarehe 25 mwezi wa kumi na mbili? Japokuwa na Krisimasi yenyewe nayo asili yake ni ya kipagani vile vile kama Pasaka ya leo na sherehe nyingine nyingi tu za kanisa.

Kama wewe ni mkatoliki muulize katekista wako au padri wako, kwamba Je kanisa linatambuaje kama tarehe fulani itakuwa ni pasaka? Au kama wewe ni dhehebu jingine linalosherehekea pasaka, unaweza kumuuliza mchungaji wako lakini akishindwa, nakushauri nenda kwa Padri kamuulize swali hilo. Au nenda kwa kuhani wa kanisa la kipagani lolote kama vile; Wahindu, Wabudha n.k., ukwaulize kuwa Je tarehe ya “Easter” (pasaka) inahesabiwaje? Hao wote watakuambia kuwa tarehe ya Easter inahesabiwa kwa mwezi kamili wa kwanza (first full moon) wa majira ya vuli, wakati watakapoitambua tarehe hiyo ndipo wanatangaza kuwa Jumapili inayofuata ni Easter.

Tarehe ya Easter ni katika Ikwinoksi-majira ya vuli kati ya machi 22 na Aprili 25, wakati jua linavuka ikweta, na siku hiyo ikifika, usiku na mchana zote huwa na urefu sawa wa masaa 12. Yafuatayo ni maelezo kutoka katika kanisa Katoliki lenyewe yanayohusu tarehe ya pasaka.

“1170 katika Baraza la Nicaea mwaka 325 BK, makanisa yote yalikubaliana kuwa Easter, Pasaka ya wakristo, lazima isherehekewe siku ya jumapili inayofuata mwezi kamili [full moon] wa kwanza baada ya ikwinoksi ya majira ya vuli. Kwa sababu ya mbinu mbali mbali za kuhesabu siku ya 14 ya mwezi wa Nisani, tarehe ya pasaka katika makanisa ya magharibi na mashariki siyo sawa. Kwa sababu hii, makanisa kwa sasa yanatafuta makubaliano ili kwa mara nyingine tena yasherehekee siku ya ufufuo wa Kristo katika tarehe ya kawaida.”(Vyanzo: http://www.vatican.va/liturgical_y…/…/2003/catechism_en.html, na Catechism of the Catholic Church - IntraText).

Maana ya jina Easter.

Jina awali la kingereza linalotumika kuielezea Pasaka hii iliyoanzishwa na kanisa Katoliki ni “Easter” ambalo ukitoa herufi 2 mwishoni linamaanisha “mashariki.” Jina hili lilikuwa jina la miungu ya kipagani, tena lilitumika kuwakilisha sikukuu za kipagani za Ikwinoksi ya majira ya vuli (Machi 21 na Aprili 25).
Jina Easter ni sawa na jina “Astarte” mungu mke wa Ashuru anayejulikana kama “malikia wa mbinguni” (Angalia neno “Easter” katika Dictionary ya English to English).

Mpendwa Bede, mwanahistoria wa Kikristo wa karne ya nane, alionyesha kuwa jina Easter lilitokana na sikukuu ya “Oestre” (“Ostere,” “Ostara”), mungu mke wa Waingereza wa majira ya vuli na uzaaji. Kulikuwa pia na mungu mke wa Teutonic (Kijerumani) aliyejulikana kama “Eostre” (pia alijulikana kama “Eastre” “Estre”), ambaye alikuwa ni mungu mke wa giza na nuru, uzaaji na majira ya vuli. Ni kutokana na miungu hawa ambapo jina Easter (Pasaka) lilianzishwa. Sikukuu ya heshima yake ilifanyika wakati wa Ikwinoksi.” -Controlled by the Callendar, p 42.

“Ishtar alikuwa mama mkuu, mungu mke wa uzaaji na malikia wa mbinguni.” -Microsoft Encarta Multimedia Enyclopedia.

Harafu angalia kwa makini Ishtar “malikia wa mbinguni” ndiye yule yule Beltis, au Semiramis, au Astarte mungu mke wa Ashuru ambaye jina lake ni” (“Easter”). Jina jingine la mungu mke huyo ni “Asht-tart” ambalo kwa kiebrania ni “Ashtoreth.” Ibada ya Ashtorethi mfalme Sulemani aliingiza katika Israeli wakati amemwasi Bwana, na kusababisha Israeli imwache Bwana na kuleteleza uharibifu wa kitaifa.

kwa sababu wameniacha mimi wakaabudu Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni, na Kemoshi, mungu wa Wamoabi, na Milkomu, mungu wa wana wa Amoni wala hawakuenda katika njia zangu, kutenda mema machoni pangu, kuzishika sheria zangu na hukumu zangu, kama Daudi baba yake. (1 Wafalme 11:33).

Leo pia ibada hii ya Ashtorethi imeingizwa kanisani na mapapa na kuleta uharibifu wa Kanisa la Kristo, Mungu hatanyamaza juu ya hili, bali atachukua hatua kama alivyochukua hatua kwa Israeli ya zamani. Jipone nafsi kwa kuachana na upagani huu.

“Nini maana ya neno Easter lenyewe? Siyo jina la Kikristo. Linachukua asili ya ukalidayo katika paji lake la uso kabisa. Easter siyo kitu kingine zaidi ya Astarte, moja ya majina ya Beltis, malikia wa mbinguni… mungu mke wa Ashuru, au Astarte, anatambulika kama Semiramis. By Athenagoras (Legatio, vol. ii. p. 179), na [by] Lucian (De Dea Syria, vol. iii. p. 382)…sasa, hakuna jina linaloweza kwa hakika zaidi kutoa picha ya sifa ya Semiramis kama malkia wa Babeli, kuliko jina la ‘Asht-tart,’ kwa maana hilo humaanisha “Mwanamke yule aliyefanya minara”…Ashturit, harafu…ni kwa wazi jina hilo hilo kwa kiebrania ni ‘Ashtoreth.'” -Alexander Hislops, The Two Babylons, pp 103, 307-308)
 
Haya wafia dini njoon huku

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kinachosherekewa ni Kufufuka kwa Kristo sio siku
umedanganywa , pasaka sio ufufuko wa YESU, hata YESU mwenyewe alisheherekea Pasaka sio EASTER... soma biblia vzr

Mathayo 15 :7
Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema,
watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami
Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.
 
Nadhani mtoa mada ni Atheist anajaribu kuonesha u stubborn wake
 
Back
Top Bottom