Kabla ya Bw Yesu hajaondoka yeye mwenyewe alishiriki mara 33 ktk sikukuu hii; je ni mwezi upi wa kusheherekea pasaka...?
KUMBUKUMBU 16...utunze mwezi wa Abibu , ukamfanyie pasaka bwana Mungu wako kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku Bwana Mungu wako, na umchinjie pasaka bwana mungu wako, ktk kundi la kondoo na la ng'ombe mahali atakapochagua, bwana apakalishe jina lake , usimle pamoja na mikate iliyotiwa chachu.
je ni ipi sheria ya kula pasaka aliyopewa MUSSA....?
KUTOKA 12;43...Bwana akawaambia Mussa na Haruna,amri ya pasaka ni hii;mtu mgeni asimle.lkn mtumishi wa mtu awaye yote aliyenunuliwa kwa fedha ukiisha kumtahiri ndipo hapo atamla pasaka
..je kuhusu pasaka.....je YESU alikula pasaka...?
LUKA 2;41.basi , wazee wake huenda Yerusalemu kila mwaka , wakati wa sikukuu ya pasaka.( hii ni kabla ya BW YESU hajazaliwa, sasa kama leo hii tunaitikadi kuwa pasaka ni kufa na kufufuka iweje yeye yeye mwenyewe ale kufa na kufufuka kwake.?
LUKA 22;1...ikikaribia sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu , iitwayo sikukuu ya PASAKA
MARKO 14;12 .. hata siku ya kwanza ya mikate isiyochachwa,walipoichinja pasaka, wanafunzi wake wakamwambia , ni wapi utakapo tuende tujuandalie uile pasaka..? (sasa kama BW YESU alishiriki kwenye sikukuu hii ni nani aliyeleta uongo....?)
WAKORINTHO (1) 5-7basi jisafisheni, mkaitoe ile chachu ya kale , mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu, kwa maana pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani KRISTO, ........PAULO