Mkuu kila kinachotokea kinaakisi malezi na makuzi ya watu wa jamii husika.
Nimekaa mahali katika shughuli inayonipa fursa ya kushuhudia vizazi tofauti katika nchi yetu jinsi vilivyo kitabia,perceptions,matumizi ya akili,etc.Amini ndugu zangu kama tutaendelea hivi,ipo shida kubwa inakuja mbele.
Kizazi cha watu wanaojua kuwaza,kuamua na kutenda kwa usahihi kilirithiwa na kizazi cha watu wanaowaza,kuamua na kutenda bila kutathmini kama ni sahihi au la,nacho sasa kinarithiwa na kizazi cha watu wasiowaza,wasioamua wala wasiotenda,no guts at all.
Tujiulize,tumefikaje hapo?
Sasa usije ukawalaumu Tiss ilhali wanaruhusiwa kurecruit maafisa toka jamii isiyofikiri wala isiyotaka responsibilities kabisa,na bado ndani ya jamii hiyo hiyo,kutokana na corruption na undugulization,tiss inarecruit mbegu mbovu zaidi ktk jamii mbovu!
10 years ago nilikuwa nainteract na vijana ambao ukimwambia kesho njoo ofisini twende mahali sikuhitaji kumfundisha dressing code,leo hii nainteract na vijana ambao hata chupi yake tu anaionyesha nje,sasa mtu huyu ambaye chupi tu kuificha ni shida,unategemea aingie tiss na kuwa na siri hata akilewa pombe?
Wapo vijana wa tiss nawajua,yaani hadi najiuliza where are we going as a nation?!Tunakosea wapi,the problem is so deep rooted.
Katika situation ya hivi,tiss ilipaswa kuwa makini sana ili kupata wenye unafuu toka jamii hii iliyochoka kichwani.Ilihitaji sana mkono wa wazee wetu kutumia busara zao kongwe kuandaa kizazi kipya kwa njia sahihi.You just trigger it,na wanaendeleza mengine wenyewe.
Wazee hawawezi kwenda na sayansi ya sasa,ila hawashindwi kuandaa kizazi chenye maadili ya kupambana na changamoto za sasa.
Zamani tulikuwa tunatumia nguvu nyingi kuelekeza vitu vidogo kwa watoto wadogo ndani ya nyumba,sasa hivi tunatumia nguvu kubwa kuelekeza vitu vidogo hata kwa vijana wakubwa wa chuo kikuu,tunakoelekea tujiandae kutumia nguvu kubwa kutiisha jamii hata katika level za wafanyabiashara,askari,hakimu etc.Tatizo linazidi kupanda kichwani and who knows,maybe kuna siku tutalazimika kumtiisha hadi Rais na makamu wake ikulu,huku watu wa kufanya hivyo wakiwa hawapo,maana jamii itajaa watu wasiowaza na kutenda!Sijui nani atatukomboa.