Part 3: TISS bado safari ngumu

My Son drink water

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
4,932
13,283
Ukitaka kufanikiwa kimaisha, jifunze kwa watu waliofanikiwa, jenga urafiki na watu wenye mafanikio, jipendekeze kwao, jifanye mjinga siku ipite, kumbe lengo lako kuna kitu unachokitafuta.

Usijifanye mjuaji, kubali kukosolewa, pokea mawazo ya watu mbalimbali kisha uyachuje na kuchukua yale unayoona yanaweza kukusaidia, hiyo ndo siri ya mafanikio.

Idara yetu ya usalama wa taifa inatakiwa iige mafanikio ya idara zilizofanikiwa zaidi Duniani, MOSSAD, MI6,CIA,PSIA(Japan) huwezi kufanikiwa kwa kuendelea kuiga mifumo iliyoshindwa, na ndo maana kila kitu chetu hakiendi, tumebakia kuwa watu wa kulia lia kila siku na umaskini usio koma.

Sikushangaa kumwona waziri mkuu wetu akizindua Gereza, kuzindua Gereza ni mkosi, ni balaa, ni nuksi, ni laana, ni futureless.

Duniani pote ktk ufuatiliaji wangu wa habari za mataifa mbalimbali sijawahi kuona kiongozi mkuu wa serikali kwa level ya waziri mkuu akizindua Gereza, bali huwa nawaona wakizindua viwanda.

Kuzindua Gereza ni ishara ya kukata tamaa, unazindua ili nani akalale humo?

Wakati Uholanzi wanafunga magereza sisi tunazidi kuyajenga, 95% ya uhalifu inasababishwa na hali mbovu ya uchumi na si vinginevyo.

Ni idara ya usalama wa taifa pekee ndo yenye uwezo mkubwa wa kutengeneza mazingira ya utawala bora yanayopelekea uchumi imara kwa watu wake, hili Japan na Israel wamefanikiwa sana.

Kwa sasa Israel ina kiwango cha maisha bora mno kwa watu wake kuliko nchi nyingi tu za Ulaya.

Israel ni nchi ya 20 Duniani kwa kuwa na uchumi bora, na ni nchi ya pili Duniani baada ya Marekani kuwa na makampuni makubwa ya Technology na kampuni zingine kubwa kuzidi kuwekeza Israel na siyo China ambayo wengi wanaisifia, huu ni utundu uliotukuka wa vijana wa MOSSAD.

Mossad wanatumika kuhakikisha Israel iko salama kwa kitu, haki, Demokrasia, utu, uzalendo vimetamalaki Israel.

Sasa unawezaje kuwaiga Rwanda hao choka mbaya badala ya kutamani kuwa Kama Japan au Israel?

Binafsi huwa natamani kuwa na pesa nyingi na mafanikio Kama MO Dewji, sitamani kuwa maskini.

Huwa natamani sana kuiona Tanzania ikifanikiwa kiuchumi Kama Australia, ukiwa ktk nchi hii huhitaji maneno ya magazeti ya kisiasa kuwa eti nchi uchumi umekua, mandhali ya nchi na watu wake pekee yatosha kukujulisha kwamba hii ni nchi yenye uchumi mzuri.

Naporudi nyumbani Tanzania huwa nakaribishwa na mandhali iliyopauka kimaskini na nyuso za watu waliokata tamaa kwa ugumu wa maisha, Halafu nikienda kwenye kibanda cha magazeti nakutana na habari ya uchumi wa Tanzania kuzidi kupaa, naishia kucheka kwa huzuni.

Mtu mmoja alikuwa akitibiwa India eti kila siku gharama za matibabu ni sh mil 150, huyu naye mlishindwa kumdhibiti kwa wizi mkubwa wa kishamba hivi?

INAENDELEA

Mbona kila linalofeli nchi hii lawama ni kwa TISS !?

TISS haiwezi kufanya kila kitu. Jambo la msingi ni kuboresha taasisi zetu nyingine zifanye kazi kwa ubora.

Hii kuitegemea TISS ifanye kila kitu ndio inaturudisha nyuma. Kukitokea rushwa lawama kwa TISS, mikataba mibovu lawama kwa TISS. Wakati huo huo kuna taasisi zinazohusika na hayo mambo.

Tukiachana na hayo, mimi ukiniuliza ni kwa nini tunapiga hatua za polepole kwenye maendeleo, ntakwambia tatizo ni elimu.

Elimu yetu imetengeneza lundo la wasomi ambao mchango wao kwenye taifa hili ni kiduchu sana. Sana sana taifa linaingia hasara ya kuwahudumia tu.
 
Unajua undani wa TISS?
 
Afrika tunapambana lakini bado Western countries bado wameshikilia uchumi wetu sokoni ndio wana amua nani apande nani ashuke
 
mkuu TISS wanawajibika kwa kila hatua na kila maamuzi ndani ya nchi hii, kauli za viongozi kubariki wananchi kuua vibaka ni kielelezo TISS hawawezi kunusa tena bali wameshikwa pabaya na Viongozi wa kisiasa... tatizo la ukosefu wa ajira, upotevu wa raia, maisha kuwa magumu na ukosefu wa huduma za kijamii kama maji ni kielelezo pia taasisi hii nyeti imesahau majukumu yake na kujipatia majukumu mengine kama vile PSU na kuratibu usalama wa chama na viongozi wa chama pekee.

NOTE... TISS inatakiwa kuundwa upya kwa malengo mapya kwa maana ujamaa siyo agenda yetu tena.
 
Ukitaka kufanikiwa kimaisha, jifunze kwa watu waliofanikiwa, jenga urafiki na watu wenye mafanikio, jipendekeze kwao, jifanye mjinga siku ipite, kumbe lengo lako kuna kitu unachokitafuta.

Usijifanye mjuaji, kubali kukosolewa, pokea mawazo ya watu mbalimbali kisha uyachuje na kuchukua yale unayoona yanaweza kukusaidia, hiyo ndo siri ya mafanikio.

Idara yetu ya usalama wa taifa inatakiwa iige mafanikio ya idara zilizofanikiwa zaidi Duniani, MOSSAD, MI6,CIA,PSIA(Japan) huwezi kufanikiwa kwa kuendelea kuiga mifumo iliyoshindwa, na ndo maana kila kitu chetu hakiendi, tumebakia kuwa watu wa kulia lia kila siku na umaskini usio koma.

Sikushangaa kumwona waziri mkuu wetu akizindua Gereza, kuzindua Gereza ni mkosi, ni balaa, ni nuksi, ni laana, ni futureless.

Duniani pote ktk ufuatiliaji wangu wa habari za mataifa mbalimbali sijawahi kuona kiongozi mkuu wa serikali kwa level ya waziri mkuu akizindua Gereza, bali huwa nawaona wakizindua viwanda.

Kuzindua Gereza ni ishara ya kukata tamaa, unazindua ili nani akalale humo?

Wakati Uholanzi wanafunga magereza sisi tunazidi kuyajenga, 95% ya uhalifu inasababishwa na hali mbovu ya uchumi na si vinginevyo.

Ni idara ya usalama wa taifa pekee ndo yenye uwezo mkubwa wa kutengeneza mazingira ya utawala bora yanayopelekea uchumi imara kwa watu wake, hili Japan na Israel wamefanikiwa sana.

Kwa sasa Israel ina kiwango cha maisha bora mno kwa watu wake kuliko nchi nyingi tu za Ulaya.

Israel ni nchi ya 20 Duniani kwa kuwa na uchumi bora, na ni nchi ya pili Duniani baada ya Marekani kuwa na makampuni makubwa ya Technology na kampuni zingine kubwa kuzidi kuwekeza Israel na siyo China ambayo wengi wanaisifia, huu ni utundu uliotukuka wa vijana wa MOSSAD.

Mossad wanatumika kuhakikisha Israel iko salama kwa kitu, haki, Demokrasia, utu, uzalendo vimetamalaki Israel.

Sasa unawezaje kuwaiga Rwanda hao choka mbaya badala ya kutamani kuwa Kama Japan au Israel?

Binafsi huwa natamani kuwa na pesa nyingi na mafanikio Kama MO Dewji, sitamani kuwa maskini.

Huwa natamani sana kuiona Tanzania ikifanikiwa kiuchumi Kama Australia, ukiwa ktk nchi hii huhitaji maneno ya magazeti ya kisiasa kuwa eti nchi uchumi umekua, mandhali ya nchi na watu wake pekee yatosha kukujulisha kwamba hii ni nchi yenye uchumi mzuri.

Naporudi nyumbani Tanzania huwa nakaribishwa na mandhali iliyopauka kimaskini na nyuso za watu waliokata tamaa kwa ugumu wa maisha, Halafu nikienda kwenye kibanda cha magazeti nakutana na habari ya uchumi wa Tanzania kuzidi kupaa, naishia kucheka kwa huzuni.

Mtu mmoja alikuwa akitibiwa India eti kila siku gharama za matibabu ni sh mil 150, huyu naye mlishindwa kumdhibiti kwa wizi mkubwa wa kishamba hivi?

INAENDELEA
TZ BADO IPO NA KAMPENI YA NYUMBA NI CHOO!😂😂😂😂 WACHA KAGAME ATUTAWALE KWA ULOFA WETU! think tank ya Jiwe😃😆😆
 
Back
Top Bottom