Part 3: TISS bado safari ngumu

Part 3: TISS bado safari ngumu

Mkuu My Son Drink Water, bado akilini mwangu siamini Kama waafrika ni binadamu kama binadamu wengine Duniani. Naamini sisi Akili zetu Si za kibinadamu!
Wao Wanaenda Kufia India, Singapore UK na kwingineko na Si Afrika, wakati siye twafia Zahati za Namtumbo kwa kukosa dawa.

Mkuu umenikumbusha yule senator alieshambuliwa ujerumani kwa ajili ya matibabu
Bado tuna safari ndefu sana
 
Sikushangaa kumwona waziri mkuu wetu akizindua Gereza, kuzindua Gereza ni mkosi, ni balaa, ni nuksi, ni laana, ni futureless.
'Mchimba shimo huingia mwenyewe' Labda iwe mhenga aliyesema hivi wakati anasema alikuwa 'matingas'
 
Hata mm nashangaa mkuu.

Yaani TISS inachukuliwa kama mungu wa pili ni kosa sana hata nchi zilizoendelea kama marekani CIA kuna sehemu zina feli pia.

Pia Tiss sio private entity kwamba kuna robo, nusu au mwaka inatoa report kuonyesha walipofanikiwa au walipofeli ila wengi wetu humu tunafanya kuhisi na mihemko ya kukosoa TISS kana kwamba hawana mazuri zaidi ya mabaya tu mkuu.

Mkuu hata ww unaruhusiwa kusifia hayo mazuri.
 
Ukitaka kufanikiwa kimaisha, jifunze kwa watu waliofanikiwa, jenga urafiki na watu wenye mafanikio, jipendekeze kwao, jifanye mjinga siku ipite, kumbe lengo lako kuna kitu unachokitafuta.

Usijifanye mjuaji, kubali kukosolewa, pokea mawazo ya watu mbalimbali kisha uyachuje na kuchukua yale unayoona yanaweza kukusaidia, hiyo ndo siri ya mafanikio.

Idara yetu ya usalama wa taifa inatakiwa iige mafanikio ya idara zilizofanikiwa zaidi Duniani, MOSSAD, MI6,CIA,PSIA(Japan) huwezi kufanikiwa kwa kuendelea kuiga mifumo iliyoshindwa, na ndo maana kila kitu chetu hakiendi, tumebakia kuwa watu wa kulia lia kila siku na umaskini usio koma.

Sikushangaa kumwona waziri mkuu wetu akizindua Gereza, kuzindua Gereza ni mkosi, ni balaa, ni nuksi, ni laana, ni futureless.

Duniani pote ktk ufuatiliaji wangu wa habari za mataifa mbalimbali sijawahi kuona kiongozi mkuu wa serikali kwa level ya waziri mkuu akizindua Gereza, bali huwa nawaona wakizindua viwanda.

Kuzindua Gereza ni ishara ya kukata tamaa, unazindua ili nani akalale humo?

Wakati Uholanzi wanafunga magereza sisi tunazidi kuyajenga, 95% ya uhalifu inasababishwa na hali mbovu ya uchumi na si vinginevyo.

Ni idara ya usalama wa taifa pekee ndo yenye uwezo mkubwa wa kutengeneza mazingira ya utawala bora yanayopelekea uchumi imara kwa watu wake, hili Japan na Israel wamefanikiwa sana.

Kwa sasa Israel ina kiwango cha maisha bora mno kwa watu wake kuliko nchi nyingi tu za Ulaya.

Israel ni nchi ya 20 Duniani kwa kuwa na uchumi bora, na ni nchi ya pili Duniani baada ya Marekani kuwa na makampuni makubwa ya Technology na kampuni zingine kubwa kuzidi kuwekeza Israel na siyo China ambayo wengi wanaisifia, huu ni utundu uliotukuka wa vijana wa MOSSAD.

Mossad wanatumika kuhakikisha Israel iko salama kwa kitu, haki, Demokrasia, utu, uzalendo vimetamalaki Israel.

Sasa unawezaje kuwaiga Rwanda hao choka mbaya badala ya kutamani kuwa Kama Japan au Israel?

Binafsi huwa natamani kuwa na pesa nyingi na mafanikio Kama MO Dewji, sitamani kuwa maskini.

Huwa natamani sana kuiona Tanzania ikifanikiwa kiuchumi Kama Australia, ukiwa ktk nchi hii huhitaji maneno ya magazeti ya kisiasa kuwa eti nchi uchumi umekua, mandhali ya nchi na watu wake pekee yatosha kukujulisha kwamba hii ni nchi yenye uchumi mzuri.

Naporudi nyumbani Tanzania huwa nakaribishwa na mandhali iliyopauka kimaskini na nyuso za watu waliokata tamaa kwa ugumu wa maisha, Halafu nikienda kwenye kibanda cha magazeti nakutana na habari ya uchumi wa Tanzania kuzidi kupaa, naishia kucheka kwa huzuni.

Mtu mmoja alikuwa akitibiwa India eti kila siku gharama za matibabu ni sh mil 150, huyu naye mlishindwa kumdhibiti kwa wizi mkubwa wa kishamba hivi?

INAENDELEA
Ndugu taifa limejaa wajinga sana kila kona unacho preach ni ngumu kufanyiwa kazi na yoyote yule

Bado watanzania hawajui wanataka nini na ndio maana wanaona sawa tuuu hata wanavyoburuzwa na wajinga na kuendeshwa kwa matamko

Mfano mdogo tuu ni bwana bashite au yule jamaa wa mbeya

Ingekuwa taifa jingine yule hakupaswa hata kurudi ofisini alipomaliza mkutano wake pale
 
Kuna msemo mmoja unasema "KUMKOSOA MWENYE DIGRII UNATAKIWA KUWA NA DIGRII AU MASTAZ"

Kukosoa taasisi nyeti kama TISS inabidi ujue mfumo ambao unatumuka katika recruitment, utendaji, level za reporting, mipaka, nk.

Na kuyajua yote hayo ni kwa yule mwajiriwa tu na si wa cheo vha kawaida bali mtu mwenye cheo.

Vinginevyo ni porojo na upotoshaji uliotukuka.
 
Mkuu kila kinachotokea kinaakisi malezi na makuzi ya watu wa jamii husika.
Nimekaa mahali katika shughuli inayonipa fursa ya kushuhudia vizazi tofauti katika nchi yetu jinsi vilivyo kitabia,perceptions,matumizi ya akili,etc.Amini ndugu zangu kama tutaendelea hivi,ipo shida kubwa inakuja mbele.
Kizazi cha watu wanaojua kuwaza,kuamua na kutenda kwa usahihi kilirithiwa na kizazi cha watu wanaowaza,kuamua na kutenda bila kutathmini kama ni sahihi au la,nacho sasa kinarithiwa na kizazi cha watu wasiowaza,wasioamua wala wasiotenda,no guts at all.
Tujiulize,tumefikaje hapo?
Sasa usije ukawalaumu Tiss ilhali wanaruhusiwa kurecruit maafisa toka jamii isiyofikiri wala isiyotaka responsibilities kabisa,na bado ndani ya jamii hiyo hiyo,kutokana na corruption na undugulization,tiss inarecruit mbegu mbovu zaidi ktk jamii mbovu!
10 years ago nilikuwa nainteract na vijana ambao ukimwambia kesho njoo ofisini twende mahali sikuhitaji kumfundisha dressing code,leo hii nainteract na vijana ambao hata chupi yake tu anaionyesha nje,sasa mtu huyu ambaye chupi tu kuificha ni shida,unategemea aingie tiss na kuwa na siri hata akilewa pombe?
Wapo vijana wa tiss nawajua,yaani hadi najiuliza where are we going as a nation?!Tunakosea wapi,the problem is so deep rooted.
Katika situation ya hivi,tiss ilipaswa kuwa makini sana ili kupata wenye unafuu toka jamii hii iliyochoka kichwani.Ilihitaji sana mkono wa wazee wetu kutumia busara zao kongwe kuandaa kizazi kipya kwa njia sahihi.You just trigger it,na wanaendeleza mengine wenyewe.
Wazee hawawezi kwenda na sayansi ya sasa,ila hawashindwi kuandaa kizazi chenye maadili ya kupambana na changamoto za sasa.
Zamani tulikuwa tunatumia nguvu nyingi kuelekeza vitu vidogo kwa watoto wadogo ndani ya nyumba,sasa hivi tunatumia nguvu kubwa kuelekeza vitu vidogo hata kwa vijana wakubwa wa chuo kikuu,tunakoelekea tujiandae kutumia nguvu kubwa kutiisha jamii hata katika level za wafanyabiashara,askari,hakimu etc.Tatizo linazidi kupanda kichwani and who knows,maybe kuna siku tutalazimika kumtiisha hadi Rais na makamu wake ikulu,huku watu wa kufanya hivyo wakiwa hawapo,maana jamii itajaa watu wasiowaza na kutenda!Sijui nani atatukomboa.
 
Hiyo Australia inaikuta Tanzania kwa uzuri?
Weee Tz yangu naipenda sana ila ina viongozi ambao huwezi kuwatofautisha na watoto, sasa huwezi linganisha mtoto na mtu mzima alienda shule hiyo Australia ni kitu kingine mkuu
 
Huwa natamani sana kuiona Tanzania ikifanikiwa kiuchumi Kama Australia, ukiwa ktk nchi hii huhitaji maneno ya magazeti ya kisiasa kuwa eti nchi uchumi umekua, mandhali ya nchi na watu wake pekee yatosha kukujulisha kwamba hii ni nchi yenye uchumi mzuri.
mbona uchumi wetu unapaa !, huoni mafly over , stigla , mameli , laki tano tano kwa wahanga wa moto , rada mpya , kama huoni yote haya basi wewe utakuwa beberu tu 😆😆😆😆
 
Ndugu taifa limejaa wajinga sana kila kona unacho preach ni ngumu kufanyiwa kazi na yoyote yule

Bado watanzania hawajui wanataka nini na ndio maana wanaona sawa tuuu hata wanavyoburuzwa na wajinga na kuendeshwa kwa matamko

Mfano mdogo tuu ni bwana bashite au yule jamaa wa mbeya

Ingekuwa taifa jingine yule hakupaswa hata kurudi ofisini alipomaliza mkutano wake pale
Hua napenda kuangalia taarifa za habari za CNN BBC, niangalia taarifa moja mtembea kwa miguu uingereza amemsimamisha Prime minister, anamuhoji kwamba anazunguka tu kwenye mitaa na wakati alitakiwa awepo kwenye mkutano muhimu huko Brussels,
You can look mindset za wenzetu zinavyotaka mtu au kiongozi mkubwa katika nchi awajibike ipasavyo kwa position aliyopo kwenye Jamii au nchi,
 
mbona uchumi wetu unapaa !, huoni mafly over , sigla , mameli , laki tano tano kwa wahanga wa moto , rada mpya , kama huoni yote haya basi wewe utakuwa beberu tu 😆😆😆😆
Yaan umeandika kinafiki mkuu hadi wee mwenyewe ukajicheka
 
Mtu mmoja alikuwa akitibiwa India eti kila siku gharama za matibabu ni sh mil 150, huyu naye mlishindwa kumdhibiti kwa wizi mkubwa wa kishamba hivi?
 
Sikushangaa kumwona waziri mkuu wetu akizindua Gereza, kuzindua Gereza ni mkosi, ni balaa, ni nuksi, ni laana, ni futureless.
 
ORODHA YA WAKURUGENZI WAKUU WA 'TISS' TANGU UHURU.

Idara ya usalama wa Taifa (TISS) imeundwa kwa sheria ya bunge namba 15 ya mwaka 1996 (Tanzania Intelligence and Security Service act No. 15 of 1996) iliyosainiwa na Rais Benjamin Mkapa tarehe 20 mwezi Januari mwaka 1997. Sheria hiyo ndio inayoipa mamlaka Idara hiyo kufanya kazi zake ndani na nje ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Pamoja na idara hii kusajiliwa kisheria mwaka 1996, lakini ilkuwepo tangu wakati wa utawala wa kikoloni chini ya ofisi ya Gavana wa Tanganyika. Baada ya Uhuru mwaka 1961 ilihamishiwa ofisi ya Rais.

Tangu idara hii kuanzishwa hadi sasa imeongozwa na Wakurugenzi 9 akiwemo Diwani Athumani Msuya aliyeapishwa jana.

Wa kwanza ni mzee Emilio Mzena, huyu aliongoza mwaka 1961 hadi mwaka 1975. Ndiye Mkurugenzi wa TISS aliyeongoza idara hii kwa miaka mingi zaidi kuliko wengine (miaka 14). Aliaminiwa na Mwalimu Nyerere baada ya idara yake kuzima majaribio kadhaa ya kumpindua.

Wa pili ni Dr.Lawrence Gama (PhD). Huyu alipokea kijiti kutoka kwa Mzena. Aliongoza kwa miaka mitatu tangu mwaka 1975 hadi mwaka 1978, kabla ya Mwalimu Nyerere kumuondoa katika nafasi hiyo na kumteua kuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma.

Wa tatu ni Dr.Hassy Kitine (PhD) ambaye aliongoza idara hii kwa miaka miwili toka mwaka 1978 hadi 1980. Kitine alichaguliwa kuongoza idara hiyo nyeti akiwa kijana wa miaka 36 tu. Anakumbukwa kwa jinsi alivyoiwezesha TISS kushirikiana na Idara ya Usalama na Utambuzi Jeshini (MI) Chini ya Meja Jenerali Tumainieli Kiwelu, kuiteka nyara ndege ya makomandoo kutoka Libya iliyokuja kumsaidia Idd Amin katika vita ya Kagera.

Mwaka 1980 Mwalimu Nyerere alimteua kijana mwingine mwenye miaka 35 Dr.Agustine Mahiga (PhD) - ambaye ni waziri wa sheria kwa sasa - kuwa Mkurugenzi mkuu wa 4 wa TISS. Aliongoza idara hiyo hadi mwaka 1983, alipomuondoa na kumpeleka kuwa Kaimu Balozi wa Tanzania (Minister Plenipotentiary) nchini Canada.

5. Baada ya Mahiga kwenda Canada, Mwalimu Nyerere alimteua Luteni Jenerali Imrani Kombe kuwa Mkurugenzi mkuu wa 5 wa TISS mwaka 1983. Nyerere alipong'atuka alimuacha kombe kwenye idara hiyo na alidumu hadi mwaka 1995.

June 30 mwaka 1996 Jenerali Kombe aliuawa na Jeshi la polisi kwa madai kuwa walifananisha gari lake (Nissan Patrol) na gari iliyokua imeibiwa na mtuhumiwa Ernest Mushi maarufu kama "White".

Alimininiwa risasi 4 kifuani licha ya kushuka kwenye gari na kunyoosha mikono juu kama ishara ya kusurrender. Askari waliohusika na mauaji hayo walihukumiwa kunyongwa lakini Rais Kikwete aliwapunguzia adhabu mwaka 2011. Bado kifo cha Jenerali Kombe kina maswali mengi kuliko majibu.

Mwaka 1995 Rais Mkapa alimteua Kanali Apson Mwang'onda kuwa Mkurugenzi Mkuu wa 6 wa TISS ambaye aliongoza idara hiyo hadi mwaka 2005 alipostaafu.

Mwaka 2005 Rais Jakaya Kikwete alimteua Othman Rashid kuongoza idara hiyo hadi mwaka 2016 alipostaafu. Othmna Rashid alikuwa Mkurugenzi wa 7 wa idara hiyo.

August 24 mwaka 2016 Rais John Magufuli alimteua Mchungaji Dr.Modestus Kipilimba (PhD) wa Kanisa la City Harvest Church la jijini Dar es Salaam kuwa Mkurugenzi Mkuu wa 7 wa TISS. Kabla ya uteuzi huo Kipilimba alikua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya taifa (NIDA).

Mchungaji Dr.Kipilimba amedumu katika nafasi hiyo hadi September 12 mwaka huu alipotenguliwa uteuzi wake na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna wa Polisi CP Diwani Athumani Msuya.!

By Malisa

Back
Top Bottom