Nakubaliana kwamba mleta uzi katumia MOYO badala ya UBONGO sawa sawa.
Binafsi mleta post angeleta tafiti kujua MAFANIKIO, KUFELI na USHAURI kipi kifanyike ili Tiss ifanye vizuri zaidi ningemuelewa lakini anapondea mwanzo mwisho kana kwamba hawana MAFANIKIO
Napenda kukujibu kama ifuatavyo:-
1.MAFANIKIO:-
Yapo, ingawaje mafanikio yenyewe ni "Hasi" KWA umma ( i.e. Negative Achievements), instead of Positive Achievements.
NB: Kutokana na Sheria na Kanuni zilizopo zinazosimamia TISS hivi sasa, ni vigumu sana kupata "Mafanikio Chanya" ambayo yataridhiwa na umma mpana zaidi wa wananchi wa Tz.Mafanikio yanayopatikana hayaweezi yakahesabiwa kuwa ni faida machoni pa wananchi wengi, ingawaje KWA mujibu wa Sheria na Kanuni za TISS inahesabika kuwa ni mafanikio.
Kumbuka ya kwamba, hata kuwaangamiza Watu RAIA wema ambao ni wakosoaji wa Rais au Serikali kwa nia njema, pia ni mafanikio KWA TISS, kulingana na natakwa ya Sheria mbalimbali, Kanuni NA Miongozo inayotumika ktk uendeshaji wa shughuli za TISS.
2. KUFELI:-
Kutokana na Sheria na Kanuni zilizopo zinazosimamia TISS, suala LA kufeli au kushindwa kupata Mafanikio Chanya yenye tija kwa maslahi mapana ya umma linakuwa ni jambo LA kawaida lisiloweza kuepukika.
Kufeli au kushindwa KWA TISS kunatokana NA kuwepo kwa Sheria, Kanuni NA Miongozo mibaya, iliyopitwa na wakati ambayo inatumika ktk kusimamia uendeshaji wa shughuli za kila siku za taasisi hii ya TISS. Kamwe Haramu haiwezi kuzaa Halali, haitatokea hata siku moja.
3.USHAURI:-
Njia pekee ya kuifanya TISS iwe Taasisi yenye manufaa kwa maslahi mapana ya umma wa wananchi wa Tz, kwanza kabisa ni:-
( i ) Kubadilisha Sheria, Kanuni, na Miongozo mbalimbali inayotumika ktk uendeshaji wa Kazi za kila siku za Taasisi hii nyeti, bila kusahau kuirekebisha Katiba ya nchi, ili ziendane NA mahitaji NA mazingira ya sasa ya Uchumi shindani KWA nguvu ya Soko, Maendeleo ya Sayansi NA Teknolojia, Utandawazi, etc.
( ii ) Kufanya Mapinduzi ya Fikra kupitia "ELIMU BORA"
ELIMU BORA ndio silaha nzito zaidi ya kuwezesha maendeleo endelevu mahali popote pale duniani.
Bila ya Elimu bora hakuna maendeleo wala mabadiliko Chanya yanayowezekana kutokea,
Mapinduzi ya fikra kupitia Elimu ni suala LA lazima KWA kila MTU ili kuleta maendeleo ya kweli.
ELIMU (Intelligence) ndio nyenzo kuu kabisa ktk kufanikisha utekelezaji WA majukumu yake yote ya Taasisi za UJASUSI mahali popote pale duniani, ndio maana zinaitwa "INTELLIGENCE SECURITY AGENCY"