Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 17,582
- 28,562
Mkuu unakosea tena.Ukitaka kufanikiwa kimaisha, jifunze kwa watu waliofanikiwa, jenga urafiki na watu wenye mafanikio, jipendekeze kwao, jifanye mjinga siku ipite, kumbe lengo lako kuna kitu unachokitafuta.
Usijifanye mjuaji, kubali kukosolewa, pokea mawazo ya watu mbalimbali kisha uyachuje na kuchukua yale unayoona yanaweza kukusaidia, hiyo ndo siri ya mafanikio.
Idara yetu ya usalama wa taifa inatakiwa iige mafanikio ya idara zilizofanikiwa zaidi Duniani, MOSSAD, MI6,CIA,PSIA(Japan) huwezi kufanikiwa kwa kuendelea kuiga mifumo iliyoshindwa, na ndo maana kila kitu chetu hakiendi, tumebakia kuwa watu wa kulia lia kila siku na umaskini usio koma.
Sikushangaa kumwona waziri mkuu wetu akizindua Gereza, kuzindua Gereza ni mkosi, ni balaa, ni nuksi, ni laana, ni futureless.
Duniani pote ktk ufuatiliaji wangu wa habari za mataifa mbalimbali sijawahi kuona kiongozi mkuu wa serikali kwa level ya waziri mkuu akizindua Gereza, bali huwa nawaona wakizindua viwanda.
Kuzindua Gereza ni ishara ya kukata tamaa, unazindua ili nani akalale humo?
Wakati Uholanzi wanafunga magereza sisi tunazidi kuyajenga, 95% ya uhalifu inasababishwa na hali mbovu ya uchumi na si vinginevyo.
Ni idara ya usalama wa taifa pekee ndo yenye uwezo mkubwa wa kutengeneza mazingira ya utawala bora yanayopelekea uchumi imara kwa watu wake, hili Japan na Israel wamefanikiwa sana.
Kwa sasa Israel ina kiwango cha maisha bora mno kwa watu wake kuliko nchi nyingi tu za Ulaya.
Israel ni nchi ya 20 Duniani kwa kuwa na uchumi bora, na ni nchi ya pili Duniani baada ya Marekani kuwa na makampuni makubwa ya Technology na kampuni zingine kubwa kuzidi kuwekeza Israel na siyo China ambayo wengi wanaisifia, huu ni utundu uliotukuka wa vijana wa MOSSAD.
Mossad wanatumika kuhakikisha Israel iko salama kwa kitu, haki, Demokrasia, utu, uzalendo vimetamalaki Israel.
Sasa unawezaje kuwaiga Rwanda hao choka mbaya badala ya kutamani kuwa Kama Japan au Israel?
Binafsi huwa natamani kuwa na pesa nyingi na mafanikio Kama MO Dewji, sitamani kuwa maskini.
Huwa natamani sana kuiona Tanzania ikifanikiwa kiuchumi Kama Australia, ukiwa ktk nchi hii huhitaji maneno ya magazeti ya kisiasa kuwa eti nchi uchumi umekua, mandhali ya nchi na watu wake pekee yatosha kukujulisha kwamba hii ni nchi yenye uchumi mzuri.
Naporudi nyumbani Tanzania huwa nakaribishwa na mandhali iliyopauka kimaskini na nyuso za watu waliokata tamaa kwa ugumu wa maisha, Halafu nikienda kwenye kibanda cha magazeti nakutana na habari ya uchumi wa Tanzania kuzidi kupaa, naishia kucheka kwa huzuni.
Mtu mmoja alikuwa akitibiwa India eti kila siku gharama za matibabu ni sh mil 150, huyu naye mlishindwa kumdhibiti kwa wizi mkubwa wa kishamba hivi?
INAENDELEA
Hakuna mahala idara za usslsma zikawa Think Tanks za maendeleo ya kiuchumi.
Pengine nikufungue macho....
"An intelligence agency is a government agency responsible for the collection, analysis, and exploitation of information in support of law enforcement, national security, military, and foreign policy objectives. ...Intelligence agencies can provide the following services for their national governments.
-Give early warning of impending crises;
-Serve national and international crisis management by helping to discern the intentions of current or potential opponents;
-Inform national defense planning and military operations (military intelligence);
-Protect sensitive information secrets, both of their own sources and activities, and those of other state agencies;
-Covertly influence the outcome of events in favor of national interests, or influence international security; and Defense against the efforts of other national intelligence agencies (counter-intelligence).
Ref: Wikipedia
Kifupi Tiss ni kulinda mafanikio na kuimarisha usalama wa nchi.