Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,667
- 25,700
Wiki hii TISS imetrend, boss mpya, wa zamani etc
Kwani TISS ina kazi gani hasa na nini tofauti yake na polisi na wanajeshi wanaolinda usalama wetu raia.
Ushauri ni kwamba sheria inayounda TISS ipitiwe upya na ikiwezekana kuwe na sheria mpya kabisa ya kuundwa kwa idara hii na vitengo vingine ndani yake vitakavyokuwa na majukumu tofauti ya TISS.
Yaani: TISS ni Usalama wa taiifa chini ya mkurugenzi wake mkuu na mitandao yake yote nchi nzima.
Mkurugenzi wake mkuu ateuliwe na raisi lakini aidhinishwe na Bunge kwa sababu katika nchi zingine huyu bosi ana level moja na waziri yoyote yule yaani anakaa kwenye kikao cha BLM.
Akiidhinishwa Bunge anakuwa amepitia chujio.
Huyu DG anakuwa kama inavyojulikana anatoa PDB (taarifa za kila siku) kwa raisi kila usubuhi na hii PDB huwa inatoka kwenye idara zote nchi nzima na hata nje.
Hivyo DG wa TISS anaiongoza na kuielekeza TISS kwenye masuala na mpango mzima wa Usalama wa Taifa na pia ni mshauri wa raisi kama nilivyosema hapo juu kuhusu PDB.
Itaendelea, ntaongelea mapendekezo ya TISS mpya na vitengo vyake kikiwemo kitengo cha ujasusi wa nje ya Tanzania , maana suala la kuzuiwa ndege yetu ya ATCL kule Afrika Kusini limetutia aibu sana.
Pia ntaongelea tofauti yake na polisi lakini uwiano wake wa kazi na JWTZ.
Pia ntaongelea nini maana ya jumuiya ya wanausalama na umuhimu kwake kwa taifa la Tanzania linaloelekea kwenye hatua ya kila mwananchi kupata maziwa na asali.