Part 1: TISS bado safari ngumu

Part 1: TISS bado safari ngumu

Msilamu awamu ya tano kwa tatizo lolote lile kwani uozo Rais wa nchi ameukuta kama alivyokuta hapakuwa na nidhamu makazini, ufisidi wa viwanda na mashirika yote ya umma alituachia Baba wa Taifa, viongozi walikuwa wanapishana angani kama mbayumbayu kwenda nchi za nje, Nchi ilipouzwa kwa Oman/China 2014/2015 kwa miaka zaidi ya 100, kumbuka Mjeruma alitawala Tanganyika kwa miaka 30, Mwengereza(UK) miaka 40 lakini pwani yote ya Tz makao makuu yao yakiwa Bandari ya Bagamoyo, TISS ilikuwa wapi, uzalendo wa viongozi ulikuwa wapi? Kama siyo Rais Dr Magufuli kufutilia mbali mikataba ya “KIBEBERU” yaan viongozi wa Tz wakiwa ndo Mabeberu na siyo Wachina wala Wa Oman nchi ingekuwa chini ya himaya ya Oman kwa zaidi ya miaka 100!!!!!!!!
Kweli JPM alikuta Tiss imeoza, ila lilimsaidia yeye, ingekua TISS inafanya kazi kweli kweli kama KBG mossad CIA nk, JPM asingekua Raisi wa nchi hi chakushangaza hawakua na file ya siri ya huyu mtu, wangekua nao nakumjua vizri kwa masilahi pana ya taifa wasingeruhusi CCM kumpa uraisi
 
Huo ndio ukweli wenyewe, kundi litalinda maslahi yake na Taifa litalinda maslahi ya Taifa.

Hivyo ikiwa na mfumo unaolinda kundi, chama fulani cha siasi, n.k. usitegemee kutoboa kama Taifa zaidi ya kulinda kikundi hicho!.
Kabisa, Kwahiyo tutaendelea kufanya siasa na si maendeleo.
 
Tangu waninyime hii nafas ya kipilimba ambayo waliniahidi nimewasusia toka jana yani sijawabrief any current intelligence info kutoka ukanda huu wa Skendinevia. Nataka sasa hivi wanirudishe nyumbani kijitonyama nimechoka kubeba boksi
😆😆😆😆
 
Yani ukisoma humu michango ya watu wanaweza fikiri kila mtu humu ni TIS maana kila jambo wanajua na wao wako sahihi kabisa kwa kila jambo ..[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Idara nyeti inapaswa kuwa na watu ambao brains zao zinacharge kweli kweli
Watu wenye upeo mkubwa kiakili na kinidhamu.

Idara inapaswa iwe na cream of the cream ya nchi

Siyo unachukua watu kwa milengo ya kisiasa matokeo yake hata analysis simple tu za mambo yanayojiri nchini hawawezi na hawana inputs zozote za maana!

Siyo lazima wachukue wenye madigrii tu bali wachukue watu bright kisha wawaendeleze, maana kuna watu hawakwenda shule za madarasani lakini wana akili kishenzi!

Kiukweli mambo yaliyokuwa yakifanyika nchini ndani ya miaka minne iliyopita utadhani yanapangwa na kufanywa na amateurs, kuanzia scripts za matukio feki ambazo raia siku hizi wanacheka tu!

Wewe imagine mtu anapiga picha kijijini kakaa na Jiwe anajifanya eti na yeye ni mmoja wa wazee masikini wa huko Chato kumbe ni.mmoja wa waambata wa Jiwe kwenye matukio mengine na picha zake zipo!

Eti mwanamama yuko hospitali anajifanya kumuomba raisi hela ya kukomboa maiti, halafu eti yuko peke yake na hakuwa cleared njiani anapopita rais, umewahi kuona wapi hii zaidi ya script?

Eti mtu anaenda bandarini na kisha kuokota vichwa vya treni

Vijana kufuatiliwa facebook kwa comment za maoni yao tu ya kisiasa na kupewa msoto mkali!

Unaenda kuandaa script ya maandamano kwenye ubalozi wa nchi nyingine kinyume cha protokali za Kidiplomasia duniani eti kushinikiza nchi iingilie mchakato wa madai yaliyoko mahakamani

Mambo gani haya ya ajabu kabisa!

TUNATAKA IDARA SMART, SHARP, JUST na YENYE KULINDA USALAMA WA NCHI KWANZA SIYO POLITICAL ambitions za MTU

Mimi ile picha ya CCTV Sirro alosema ni ya gari ilomteka Mo ndo iliniacha hoi kabisa.....yaani picha HD kabisa![emoji23]
 
Kweli JPM alikuta Tiss imeoza, ila lilimsaidia yeye, ingekua TISS inafanya kazi kweli kweli kama KBG mossad CIA nk, JPM asingekua Raisi wa nchi hi chakushangaza hawakua na file ya siri ya huyu mtu, wangekua nao nakumjua vizri kwa masilahi pana ya taifa wasingeruhusi CCM kumpa uraisi

Inasemekana file lipo na hao wanaopanguliwa ni wana madhara
 
Tiss imekuwa kama polisi wa uchunguzi, wanalewa na kujisifu, UVCCM inatia aibu, kila mtu anajua 90% ni UVCCM aibu tupu
Tatizo kila mtu mjuaji. Mfano kama 90% unatuambia ni UVCCM inamaana tukikuuliza kwa jumla yao wako wangapi utatupa jibu?
 
Hivi kati ya TISS na TANU (CCM) kipi kilianza kwanza?
 
Nauliza tu hakuna mpinzani aliyeko kwenye makaratasi ya malipo ya TISS? Maana hapo juu umesema haiwezi kuajiri wapinzani
Wapo wengi tu, ingawa inawezekana mwanzisha uzi halijui hilo. Usajili wa tiss haufanywi kwa kuangalia kadi za vyama! Mtoa mada nadhani ana uchungu kwa kuwa mzee wake wa kanisa amepigwa chini.
Lakini, nakubaliana naye kwamba kuna mambo ambayo tiss inatakiwa kuimprove ili kurejesha hadhi ya ilivyokuwa wakati wa mwalimu.
 
Kuna kitu sensitive nilkua nimeandika lkn kwa upumbavu wa watu waliopo huko nimamua kufuta. Maana hawachelewi kupiga hodi kwa Melo kuomba faili.
 
Back
Top Bottom