TISS ina matatizo makubwa sana tofauti na watu wengi wanavyofikiri.
Tatizo kubwa kabisa linaloifanya TISS kuonekana kuwa ni taasisi ya hovyo, isiyofaa NA kuonekana kuwa ni taasisi ambayo ni adui mkubwa wa umma wa Tz ni kutokana na Sheria anzilishi ya Taasisi hii, pamoja na Sheria zingine, kanuni, na Miongozo inayotumika ktk kuendesha shughuli za kila siku za taasisi yenyewe.
Sheria na Kanuni zinazosimamia TISS ni mbaya, zimepitwa NA wakati, hazilengi ktk kuikomboa nchi hii na wananchi wake wote KWA ujumla kutokana na vitisho mbalimbali vya kiusalama pamoja na kuikomboa nchi na watu wake kutoka kwenye janga kubwa LA umaskini KWA kufanya UJASUSI wa Kiuchumi.
Kutokana na Sheria na Kanuni zilizopo, TISS inalazimika kuwa ni taasisi ya Kumlinda Rais, Urais, Viongozi wa Serikali, hasa wa nyadhifa za juu tu pamoja Serikali yenyewe, pamoja na Chama Tawala kilichopo Madarakani, basi.Hivyo basi, hata akiajiriwa nani ndani ya taasisi hii ya TISS anajikuta analazimika kutii kwa lazima matwaka haya ya Sheria ya Kulinda NA kutetea maslahi ya Viongozi wa Serikali tu na ya Chama Tawala kilichopo madarakani badala ya Kulinda NA Kuitetea Maslahi Mapana ya Umma wa wananchi wa Tz.