Part 1: TISS bado safari ngumu

Part 1: TISS bado safari ngumu

boss wa TISS ni rais wa TANZANIA ambae ni mwenyekiti wa CCM.
 
Usalama wa Taifa wa Tz huwa wanaviloja mkuu, kuna mmoja nlikutana nae hospital ni pale Posta mtaa wa mtendeni kwa Dr. Hassanali. Jamaa kaja hospital kakuta foleni, kaona dah muda unaenda ntachelewa. Mwanawe ndo alikuwa anaumwa, basi jamaa likaamua kukunja sura likaenda mpaka pale mapokezi likajitambulisha kwa yule mdada kwa cheo chake cha usalama wa taifa. Yule msita akawa anamnyenyekea na watu tukaanza kumchora huyu bwana kumbe ni big huko majuu, lenyewe likaona sifa na upara wake
Hizi kweli ni stori za Vijiweni
1. Afisa wa TISS huwa hajitanbulishi popote hata kwa mwenza wake wala wanawe. Katika mazingira yoyote Yale hawezi kujitamulisha kwa cheo wala kazi yake bali kazi mbadala
2. Huwa wana marafiki katika sehemu mbalimbali za huduma ambako hawafahamiki kama TISS hivyo anaweza kufanikisha matibabu kwa mwanae bila foleni wala kubembeleza mapokezi.
3. Kama Ulikuwa kwenye foleni naye akapitilisha kwenda mapokezi, sio rahisi utambue alivyojitambulisha
 
UKIONA IDARA KAMA HII IMEKUMBATIA CHAMA JUA TUNA SAFARI NDEFU.
MIMI KWA MAWAZO YANGU YA KIJINGA HAWA WALITAKIWA KUWA WASHAURI WA VYAMA NA TAASISI MBALIMBALI JUU YA MUSTAKABAL WA MAMBO YAO.
MFANO WALITAKIWA KUWAPITIA WAGOMBEA WOTE NA KUVISHAURI VYAMA JUU YA WALE WENYE MIENENDO MIBOVU ILI TAIFA LIPATE VIONGOZI WAZURI.
 
Tangu waninyime hii nafas ya kipilimba ambayo waliniahidi nimewasusia toka jana yani sijawabrief any current intelligence info kutoka ukanda huu wa Skendinevia. Nataka sasa hivi wanirudishe nyumbani kijitonyama nimechoka kubeba boksi
HahahHa
 
Hizi kweli ni stori za Vijiweni
1. Afisa wa TISS huwa hajitanbulishi popote hata kwa mwenza wake wala wanawe. Katika mazingira yoyote Yale hawezi kujitamulisha kwa cheo wala kazi yake bali kazi mbadala
2. Huwa wana marafiki katika sehemu mbalimbali za huduma ambako hawafahamiki kama TISS hivyo anaweza kufanikisha matibabu kwa mwanae bila foleni wala kubembeleza mapokezi.
3. Kama Ulikuwa kwenye foleni naye akapitilisha kwenda mapokezi, sio rahisi utambue alivyojitambulisha
Hapo namba moja: hata raisi mwenyewe alimtambulisha kuwa yeye ni TISS Diwani wkt anampa ukurugenzi wa PCCCB sasa wewe unategemea nini...????
 
TISS ina matatizo makubwa sana tofauti na watu wengi wanavyofikiri.

Tatizo kubwa kabisa linaloifanya TISS kuonekana kuwa ni taasisi ya hovyo, isiyofaa NA kuonekana kuwa ni taasisi ambayo ni adui mkubwa wa umma wa Tz ni kutokana na Sheria anzilishi ya Taasisi hii, pamoja na Sheria zingine, kanuni, na Miongozo inayotumika ktk kuendesha shughuli za kila siku za taasisi yenyewe.

Sheria na Kanuni zinazosimamia TISS ni mbaya, zimepitwa NA wakati, hazilengi ktk kuikomboa nchi hii na wananchi wake wote KWA ujumla kutokana na vitisho mbalimbali vya kiusalama pamoja na kuikomboa nchi na watu wake kutoka kwenye janga kubwa LA umaskini KWA kufanya UJASUSI wa Kiuchumi.

Kutokana na Sheria na Kanuni zilizopo, TISS inalazimika kuwa ni taasisi ya Kumlinda Rais, Urais, Viongozi wa Serikali, hasa wa nyadhifa za juu tu pamoja Serikali yenyewe, pamoja na Chama Tawala kilichopo Madarakani, basi.Hivyo basi, hata akiajiriwa nani ndani ya taasisi hii ya TISS anajikuta analazimika kutii kwa lazima matwaka haya ya Sheria ya Kulinda NA kutetea maslahi ya Viongozi wa Serikali tu na ya Chama Tawala kilichopo madarakani badala ya Kulinda NA Kuitetea Maslahi Mapana ya Umma wa wananchi wa Tz.
Sasa mkuu ni kwa nini miaka ya nyuma ilikuwa na heshima ukilinganisha na Sasa hivi Kama unasema sheria zake ni zile zile za zamani?
 
Nauliza tu hakuna mpinzani aliyeko kwenye makaratasi ya malipo ya TISS? Maana hapo juu umesema haiwezi kuajiri wapinzani
Hata Kama ukiona mpinzani yupo kule ujue sio mpinzani wa kweli bali anataka kuwaingiza chaka na kuwavuruga wenzake.
 
Natamani TISS iwe independent institution, ideology ibadirike..TISS isiwe kwa ajili ya chama TAWALA na kuhakikisha kinakaa madarakani pali TISS iwe kwa ajili ya usalama wa Watanzania wote...wa vyama vyote.....TISS iwe kama baba mzazi..
unaweza kuwa na watoto tofauti tofauti..wengine wakorifi, wahuni..etc lkn still ni wanao unaenda nao hivohivo
 
Hata Kama ukiona mpinzani yupo kule ujue sio mpinzani wa kweli bali anataka kuwaingiza chaka na kuwavuruga wenzake.
Ndio kazi za interejensia hizo. Na hapo ndipo chama kinabidi kitumie interejensia yake kubaini hilo. Sio makapi yote yanayo hamia chamani inaitwa kubadili gia angani kumbe kukiua chama
 
Kuna watu wanadhani kuondoka kwa mzee wangu wa Kanisa,TISS ndugu Kipilimba basi mambo yanaenda kubadilika na kuifanya idara hiyo ifanye kazi nzuri la hasha.

TISS bado ina safari ndefu mno ili iwe idara bora Kama zingine, recruitment ya TISS imejaa viroja na maajabu, tofauti na mashirika mengi ya kijasusi Duniani.

TISS imejaa kina "kamlete ",yaani watu wanaopewa ajira na ndugu zao kwa sababu ya ugumu wa maisha ya Bongo, hakuna usahili wa uhakika, madhara yake kumejaa ma agent ambao wakiona post Kama hii wanatamani wamkamate mtoa mada na kumpoteza.
Haina watu wazalendo kwa Taifa lao bali wazalendo wa chama tawala cha CCM chenye ndoto za kutawala Tanzania milele.

TISS haiwezi kumwajiri mwanachama wa CHADEMA au mpinzani yoyote bali Lazima awe mfia CCM na siyo mfia Tanzania.

Kazi kubwa za idara za kijasusi ni kuhakikisha nchi iko salama wakati wote na kuhakikisha hakuna umaskini ktk nchi kwa gharama yoyote ile.

Hongera zenu CIA, MI6, MOSSAD nyie ndo mnaipeleka Dunia puta kwa maslahi ya mataifa yenu, hamna muda na siasa.

Kazi ya idara ya usalama wa taifa ni kuwa loyal kwa nchi na si kwa wanasiasa...

INAENDELEA
USALAMA WA CCM.
 
Nauliza tu hakuna mpinzani aliyeko kwenye makaratasi ya malipo ya TISS? Maana hapo juu umesema haiwezi kuajiri wapinzani
Huyo kaanza vizuri, kaandika hadi kapitiliza.

Hajui hata hao waanzilishi wa upinzani walitoka jikoni?

Anyways waganga wa kupiga ramri kulingana na mtukio hawajaisha duniani.
 
Hapa ndipo unaonyesha wazi kuwa umeparamia mambo ya TISS wakati kichwa chako cheupeee .Umejaa ujuaji hewa.TISS wasipoajiri wanachama wa vyama vya upinzani nani atawaletee taarifa za kiinteligencia za ndani ya Chadema na hivyo vyama vingine vya Upinzani? Naona unaandika story za vijiweni.Kichwani uko mweupeeee.Wewe kijiweni ndie wanakuona expert wa mambo ya TISS vijiweni !!!!!!!
Naishi Australia, hapa hakuna vijiwe wala vilinge kila mtu yupo busy, ni bora ungekaa kimya kuliko kuonyesha ujinga wako humu, TISS kupeleka Majasusi upinzani wapate Taarifa za CHADEMA kuna faida gani kwa nchi? Kwa nini wasipeleke spies Japan wakaibe technology za kutengeneza magari ili nchi ipae kiuchumi, habari za Siri za CHADEMA zina maslahi gani kwa nchi?
Wewe ni zero brain kabisa, kwanza mada yangu hujaielewa, mtu mjinga Kama ulivyo wewe eti unakuta ni agent wa TISS, pathetic kabisa.
 
Umejihangaisha kumjibu bure, kwenye majukumu ya TISS hilo la kuvifanyia surveillance vyama vya upinzani haimo.

Huyo ndo Kati yao, Lumumba buku7
Naishi Australia, hapa hakuna vijiwe wala vilinge kila mtu yupo busy, ni bora ungekaa kimya kuliko kuonyesha ujinga wako humu, TISS kupeleka Majasusi upinzani wapate Taarifa za CHADEMA kuna faida gani kwa nchi? Kwa nini wasipeleke spies Japan wakaibe technology za kutengeneza magari ili nchi ipae kiuchumi, habari za Siri za CHADEMA zina maslahi gani kwa nchi?
Wewe ni zero brain kabisa, kwanza mada yangu hujaielewa, mtu mjinga Kama ulivyo wewe eti unakuta ni agent wa TISS, pathetic kabisa.
 
Huyo kaanza vizuri, kaandika hadi kapitiliza.

Hajui hata hao waanzilishi wa upinzani walitoka jikoni?

Anyways waganga wa kupiga ramri kulingana na mtukio hawajaisha duniani.
Usilolijua ni usiku wa Giza, Hujui hata nilichokiandika, umesoma juu juu tu, soma between the lines utaelewa mada vizuri.
TISS haina msaada wowote kwa taifa.
Kawafanya kina Mbatia na Mabere Marando kuwa wapinzani hewa Kuna faida gani kwa nchi?
Hujaelewa lolote kwenye mada yangu.
 
Kuna muda nawaza ili hii nchi uendelee inabidi watu wote million 55 tutolewe tuwekwe sayari nyingine,....ianze afresh!!!!

Unless otherwise kuisha kwa haya matatizo,migongano, ubinafsi na unafiki ni ngumu Sana Kama sio ndoto.

Naamini creams of the creams wapo lakini ni ngumu kufanya kazi ikiwa impurities ndo zimeshika hatamu
We have a thousand miles way to go.🙎
 
Mambo yamebadilika sana yaani watu tunajadili masuala ya TISS rahisi rahisi tu .
Miaka ile ya akina mzee Apson unaweza kukaa hata mwaka mzima na usikutane na habari ya TISS.
Walau miaka ya mzee wangu mzanzibar Othuman na msaidizi Balozi Jack Zoka tulikuwa tunasikia habari za idara walau Mara mbili kwa mwaka lakini miaka hii kila siku tunajadili TISS.
Sisemi kuwa ni jambo baya lakini kwa asili ya idara yenyewe na mambo yanayojadiliwa nadhani aidha idara imekuwa wazi sana au wasiotakiwa kujua masuala ya TISS basi wamejua habari nyingi kupitiliza.
Ufanisi wa idara hizi popote duniani umejengwa kwenye "usiri wa kutotabirika" kwenye mipango yake na mfumo wake wa kiutendaji.
Sasa mkuu kwa uelewa wako unaona kuna kipi hapa kinachojadiliwa ambacho ni nyeti sana toka huko idarani?
Mimi naona ni ngonjera zisizo na maana
 
Kuna kimama kilikuja school wakati tuna jiandaa na necta form six..yani kinavyo ongea na kilivyo tu maswali yake unajua kabsa uyu ni usalama wa Taifa .. shenzi zao...
 
Vijana wa tiss wanatakiwa wapunguze ulevi kwanza, wao ni kishinda bar mchana kutwa
 
Viongozi wa nchi hii ndio wanaongoza kupeleka watoto wao kuajiriwa huko tiss itakuaje bora
 
Back
Top Bottom