Parking Dar: Kingunge na familia yake ni wasanii?

Kwenye magazeti ya leo familia ya Kingunge wamejitetea kuwa wanapata hasara siku ambazo madaraja huzunjika kwa mvua na kusababisha mabasi kutosafiri.My take: hii ni 'very weak excuse' na hutokea mara 1 kila baada ya miaka hata 5 na kwa njia 1 tu ya arusha/moshi au singida/mwanza.
 
...kingunge mbona ana matatizo kiasi hiki! Huyu si ndio anaendesha pia ile parking system? Ndio maana anachukia watu wanaopinga mafisadi,ni fisadi namba moja, na tatizo kuwa busara kwake kwake zinapungua badala ya kuongezeka kama tunavyodhani wazee wana busara,lakini kwa huyu ni tofauti. Kwanza ana ushauri mbovu kwa jk, pili anatetea ufisadi (rejea alivyopinga kuwepo kwa ufisadi bot), nadhani pia ndio mzee wa fitina ccm (rejea alivyowapinga akina warioba na bujiku). Naomba mwenye mazuri yake ayaweke hapa, so far record yake haionyeshi!

swadaktaaaa!
 
Rekodi za mapato yao yote tangu walipokabidhiwa rasmi kuendesha kituo hicho zipitiwe na wakaguzi na warudishe mapato ambayo yanastahili kwa halmashauri ya jiji ambayo ni lazima yatakuwa zaidi ya shilingi milioni 1 kwa siku.

Jiji halina fedha za kufanya mambo mbali ya kuboresha huduma mbalimbali za jiji, wakati huo huo kuna watu wanapewa mikataba ya kifisadi.

Mkuu Bubu salam,
Katika habari ambazo nimesoma kwa MSHANGAO MKUBWA nihizi; ati serekali ya JIJI ua iwe ya mji au ya mitaa itoe ZABUNI kwa KABEPARI au KAFISADI FULANI hivi kakusanye MAPATO hiyo SEREKALI yenyewe ina kazi gani kama hiyo ya kuhakikisha na kudhibiti kila aina na namna ya njia za uingizaji kipato zinakua chini yao.wanatoa ZABUNI pale tu wanapokuwa wamezidiwa au hawana TAALUMA na hiyo shughuli husika. Hapa sidhni kama hiyo ndio KESI ilivyo ni wazi LINE ilichongwa hiyo Kampuni ifaidike kirahisi I DONT CARE KAMA NI FAMILIA KINGUNGE or SH...T!!!! THIS KIND OF UPUUZI,UJINGA na USHENZI should stop and STOP NOW. Mama mia; ati Jiji linashindwa kukusnya mapato? linaajiri KIJAMAA cha mitaanni kiwafanyie hiyo kazi sijui hao WAKURUGENZI wa Jiji na MAMENEJA walipita shule gani? Na ikiwa TENDA hiyo iliuwa Crieted kwa makusudi na kuna Presha zozote bihind it pia tujulishwe.Sasa ni wakati wa kusema HATUVUMILII KUONEWA TENA,KUNYANYASWA,KUPUUZWA NA KUDHALILISHWA.
 
Kwenye magazeti ya leo familia ya Kingunge wamejitetea kuwa wanapata hasara siku ambazo madaraja huzunjika kwa mvua na kusababisha mabasi kutosafiri.My take: hii ni 'very weak excuse' na hutokea mara 1 kila baada ya miaka hata 5 na kwa njia 1 tu ya arusha/moshi au singida/mwanza.

Waonyeshe mahesabu yao basi ili hiyo hasara wanayopata kwa madaraja kuvunjika kila siku; na kwa barabara kama za Arusha na Mbeya tuyaone. Pia watueleze walipataje hiyo mikataba, na walitumia kigezo gani au fomula ipi kupata hiyo1.5m wanayolipa kila siku badala ya % ya mapato yanayokusanywa! Vinginevyo wakae kimya wasubiri hukumu yao, ambayo haiko mbali.
 
Hapa tunazinguana tu hakuna lolote litakalofanywa aidha yatakuja majibu hewa ili kila mmoja aridhike ,huyu PM kabakiza miezi tu ,sasa miaka yote imepita anakuja kukurupuka leo wakati uchaguzi umekaribia ,kama sikutaka kuwalaghai watu ni kitu gani ?
Halafu ikiwa hapo ameingia yeye PM(Waziri Mkuu ) Hawa wakuu wa mikoa wapo wapi ? Wakuu wa Wilaya wapo wapi ?

Bila ya shaka akina Mkuu wa Mkoa na wilaya wanaogopa watoto au jamaa wa vigogo kwa muondoko huo tatizo lipo mikoa yote ,kwa maana nyingine wakuu wa mikoa na wilaya wanashindwa kutekeleza kazi zao kwa kuogopa watayagusa magogo makubwa na hivyo kuhatarisha ajira zao ,kwa maana hiyo Utawala wa CCM na viongozi wake hawataweza kutekeleza kitu na huko ni kushindwa koutawala kwa sababu wanaogopana au wanalindana .Pinda ameamua ili kuikosha serikali yake kutokana na Uchaguzi Mkuu unaochungulia ,harakati hizi kama zingeanza mara tu baada ya Kikwete kuchukua madaraka leo tungelikuwa mbali ,lakini woga ndio umewakinza wafuasi wa Sultani CCM.
Wafuasi wa Sultani CCM hamna mtakachokifanya kwa leo kwani miaka 47 imeshatosha mlichokipanda itakuwa kiko njiani kukivuna , haya madoido ya kupigishana kura mchana ni aibu na kutafuta matatizo zaidi baina ya wananchi.Kama polisi na usalama wa Raia umeshindwa kuzuia basi wakuu wake wabwage manyanga.
 
Hivi Jiji Linashindwa kukusanya Mapato hadi Wawape Kampuni FEKI tender...wether tender sahihi au sio....Utaratibu huu wa Jiji kutoa Tender siouni kama una Manufaa kwa Jiji wala wananchi...

Mbona TRA hatutoi tender kampuni zije zikusanye Mapato? Huu ni Ubwege....Tender mnazotakiwa sio za Kukusanya mapato yenu....Hata USAFI HAMPASWI KUTOA TENDER....

Pinda Hana lolote...JK mwanzoni alipoingia Madarakani alipita Masoko yote, then baadae Shein nae akapita...Hawakuyaona Haya? ya soko la Tandale kuingiza Million 1 kwa mwezi? CCM na Serikali yake isitufanye wapumbavu...they know pesa zinakwenda wapi...yeye Pinda Kakaa kwa Waziri MKUU Muda wa maisha yake yote..HAYAJUI HAYA...?.....PINDA huwezi pata credits kwa mchezo....You have to work more~~
 
hiki kibabu kimeanza kuiba tangu kijana mpaka anazeeka bado ni mwizi tu,anafikiri hizo hela atazikwa nazo. Na kwanini JK anamuendekeza huyu mzee.Eti mbunge wa kuteuliwa, anamtakia nini? Hawa CCM wote ni wizi, kuanzia Raisi mpaka diwani. Mkapa hafungwi kwa wizi aliofanya kwasasababu na huyu kiwete anajua na yeye atafungwa akimaliza wakati wake.
 
Sometimes ukifikiria inachekesha... kajamaa kazee mpaka meno yameisha lakini kanatafuna kama kawa!!
 
pinda aumbua familia ya kingunge

2009-03-13 14:17:27
na restuta james​

waziri mkuu mizengo pinda ameshuhudia mkataba mbovu unaonukia ufisadi katika kituo kikuu cha mabasi cha ubungo (ubt), jijini dar es salaam.

ufisadi huo unafanywa kupitia mkataba uliofikiwa kati ya halmashauri ya jiji la dar es salaam na mkandarasi, kampuni binafsi ya smart holdings, inayomilikiwa na familia ya mbunge wa kuteuliwa na rais, kingunge ngombale-mwiru.

katika taarifa yake, izumbe alisema kwa mujibu wa mkataba, mkandarasi huyo hutoa sh. Milioni 1.5 kwa halmashauri ya jiji kwa siku, taarifa iliyomshangaza pinda na kumfanya ahoji: ``hata kama anakusanya sh. Bilioni 1 anatoa sh. Milioni 1.5? Na kwa nini mkataba utamke shilingi badala ya asilimia?`` [/b]


kutokana na hali hiyo, pinda aliiagiza halmashauri ya jiji na halmashauri ya manispaa ya kinondoni kuupitia upya mkataba huo ili kuondoa maswali yasiyokuwa na majibu.


Source: Nipashe [/color]



naunga mkono hoja hiiiiii jamani kwani hakuna watu wengine wanaoweza kuboresha parking system tz?
 
Sahihisha hapo,
anawatoto wawili wakiume, mwingine ni nyumba ndogo mamake alikuwa pale ubungo National housing!
Huyo mama hana aibu na wala hatosheki ! Huyo mzee ameshakua mtu mzima, haongei wala hafurukuti mbele ya mkewe. "National Parking solutions" wanakusanya pesa mpaka vichochoro vya kariakoo, mpaka mbele ya nyumba za watu, ardhi yote ya DAR imekuwa shamba lake, utafikiri ametoka nayo BK ! isitoshe, ana mtoto mmoja tuu, na yeye kazeeka, hizo hela zote atazipeleka wapi ??????????????? TAMAA GANI HIYO !!!!!!!!!!!!!!
 
kale kazee nadhani kana miaka zaidi ya mia, sasa hakana tena jipya. ila aliona kuwa wengi wape. alikuwa upande wa nyerere lakini akazidiwa nguvu na mafisadi so akaamua kujiunga nao ili kutimiza ule usemi usemao, if you cant fight us, join us
 
Naanza kupata picha kuwa Kingunge yuko nyuma ya kila ufisadi ndani ya nchi hii. The old man is so crooked!!
 
Pinda kufa na mkataba kampuni ya familia ya Kingunge Ubungo

2009-03-16 10:29:35
Na Mashaka Mgeta


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameagiza Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), kukagua hesabu za makusanyo ya fedha katika kituo kikuu cha mabasi kilichopo Ubungo jijini Dar es Salaam.

Makusanyo ya fedha hizo, yanafanywa na kampuni ya Smart Holdings inayomilikiwa na familia ya Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Kingunge Ngombale-Mwiru.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana, alipokuwa akizungumza katika kikao cha majumuisho, baada ya ziara yake ya siku tatu jijini Dar es Salaam.

Alisema bila kujali mmiliki halali wa kampuni hiyo, ukaguzi wa hesabu hizo unapaswa kufanyika kwa maslahi ya umma, kabla ya kuchukua hatua kwa mujibu wa mapendekezo yatakayotolewa na CAG.

``Mimi sijui ni nani anayemiliki ile kampuni, lakini hapa ninachokizungumzia kinahusu maslahi ya umma. Tuone hicho kinachofanyika huko ni kwa maslahi ya nani,`` alisema Pinda katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Pinda, alisema inashangaza kuona licha ya kuwepo mazingira yanayothibitisha kupatikana kwa kiasi kikubwa cha fedha, serikali inaambulia Sh. milioni 1.5 pekee kwa siku.

Katika hali iliyoonyesha kuchukizwa na hali hiyo, Pinda alisema ukaguzi huo unapaswa kufanyika haraka, ili kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kisizidi kupotea.

``Tusijidanganye kwamba mkataba bado una muda wake kabla ya kuisha, (mkataba) utaendeleaje kuwepo wakati tunazidi kupoteza... CAG afanye kazi yake na ushauri atakaotupatia ndio tutakaoufanyia kazi,`` alisema.

Pinda alisema ukaguzi huo unapaswa kufanyika hadi katika vibanda vilivyomo ndani ya kituo hicho, ili kubaini ikiwa kuna baadhi visivyolipa mapato serikalini.

Alisema kituo cha Ubungo ni miongoni mwa vyanzo vikubwa vya mapato ikiwa usimamizi wake ungefanyika kwa ufanisi zaidi.

Aidha, Waziri Mkuu, alisema licha ya kituo hicho, CAG atafanya ukaguzi kama huo katika Soko la Kariakoo, ambalo uongozi wake unadhihirisha kutokuwa na uwezo wa kusimamia uendeshaji wake.

Siku moja baada ya ziara ya Waziri Mkuu kituoni hapo, kampuni ya Smart Holdings ilisema madai yaliyotolewa dhidi yake hayana ukweli wowote.

Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo, Hassan Khan alisema kilichodhihirika ni kwamba, viongozi wa Jiji waliokuwapo kwenye ziara hiyo, hawajui lolote kuhusu mkataba huo na ndio maana wakashindwa kumueleza Waziri Mkuu ukweli kuhusu suala hilo.

Khan alisema katika mkataba huo, walikubaliana na Halmashauri ya Jiji kwamba, watakuwa wakiilipa asilimia 75, lakini akashangaza kusema kwamba asilimia hiyo ni Sh. milioni 1.5 na kwamba watakuwa wanalipa kiasi hicho kwa kila siku bila kujali hali ya mapato itakayokuwa kituoni hapo.

Khan alisema siku za wikiendi na wakati madaraja yanapokatika, kampuni yao hupata hasara.

Katika hatua nyingine, Pinda, alizitaka halmashauri za manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni, kuweka utaratibu wa kuboresha mazingira ya masoko na kuondoa uchafu uliokithiri kwenye maeneo kadhaa jijini.

Waziri Mkuu aliwaambia watendaji na viongozi kuwa masoko mengi ya jijini hayapo katika hali nzuri, hivyo kutowapa wafanyabiashara fursa nzuri za kunufaika kiuchumi.

Pia alisema uchafu umekithiri kwenye maeneo mengi, hivyo kutaka ongezeko la kasi ya kuondokana na hali hiyo.

Kuhusu kero ya usafiri wa wanafunzi katika Jiji la Dar es Salaam, Waziri Mkuu aliutaka uongozi wa manispaa hizo kubuni mbinu mbadala, ikiwemo matumizi ya mabasi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA).

Alisema kwa kuwa tatizo hilo ni kubwa linalotegemea utekelezaji wa mradi wa mabasi yanayokwenda kwa kasi kuwa sehemu ya suluhu yake, mabasi ya UDA yanaweza kutumika kwa kipindi cha kabla ya kuanza kwa mradi huo.

Waziri Mkuu Pinda alisema kuna dalili za kuwepo vitendo vya rushwa kwa watendaji wa halmashauri ya Jiji na Manispaa ya Ilala katika ugawaji wa mabanda ya biashara katika soko la Mchikichini.

Alisema baadhi ya wafanyabiashara walielezea kuwepo mabanda yasiyokuwa na watu kutokana na watendaji wasiokuwa waaminifu na wanaosimamia soko hilo, kutaka hongo kutoka kwao (wafanyabiashara).

``Hatuwezi kwenda hivyo, hebu gavana (Mkuu wa Mkoa) ingilieni kati suala hili, mtangaze ili vibanda vile vipate watu,`` aliagiza.

SOURCE: Nipashe
 
Jamani hizo fedha za parking sio za CCM wala nini za Kingunge - mke wake anapita akisupervise na akikuta hawa vijana/wadada wa parking wamekaa tu (eti lazima wasimame siku nzima) anawafukuza kazi - imagine MMOJA AMENISIMULIA AMEFANYA KAZI 4 YEARS AKIMKUTA NA KOSA ANAMFUKUZA - HIVI ANALIPA KODI KWELI? JE ANAWAWEKEA NSSF HAWA WATANZANIA? NI UKATILI TU UNAOFANYIKA - achilia mbali fedha wanazokusanya - ni mradi binafsi na kama Jiji labda analipa percentage kidogo tu - unapark gari hata uchochoroni unatakiwa kulipia - AFADHALI WALE WA BREAKDOWN HAWAPO SIKU HIZI - LA SIVYO NAO WANAVUTA GARI - HALAFU UNALIPIA 85,000/= ETI UMEPARK VIBAYA - KWANINI JIJI LISITENGENEZE PARKINGS WATU WAKAPARK KISTAARABU? UNAPARK GARI - MAHALI PACHAFU - YET YOU PAY THEM - THIS IS TOO MUCH - NCHI HII HAINA HAKI HATA KIDOGO - NA HIYO FAMILIA YA KINA KINJE HIZO HELA ZITAWATOKEA PUANI - KWANI NI HELA ZA MASKINI - AFADHALI ZINGEINGIA NA KUSAIDIA WATOTO YATIMA
 
Rekodi za mapato yao yote tangu walipokabidhiwa rasmi kuendesha kituo hicho zipitiwe na wakaguzi na warudishe mapato ambayo yanastahili kwa halmashauri ya jiji ambayo ni lazima yatakuwa zaidi ya shilingi milioni 1 kwa siku.

Jiji halina fedha za kufanya mambo mbali ya kuboresha huduma mbalimbali za jiji, wakati huo huo kuna watu wanapewa mikataba ya kifisadi.



2009-03-16 08:16:00

Pinda : Audit bus terminal performance
By Beatus Kagashe
THE CITIZEN

Prime Minister Mizengo Pinda has ordered the Controller and Auditor General (CAG) to do a performance management audit at the Ubungo Bus Terminal (UBT) and the Kariakoo market to establish the truth about revenues collected and their contracts.

Speaking yesterday at a meeting to wind his tour of Dar es Salaam Region, Mr Pinda said the report would provide a solution to the problem as there were many unanswered questions regarding the loopholes in the two areas.

Mr Pinda said the bus terminals and the major markets would be good sources of income if well managed. Smart Holding Co Ltd has been contracted to collect revenue at UBT since 2004 and they are paying Sh1.5 million per day.

The Premier said it was amazing that the number of buses using the terminal has been increasing but the revenue remained the same.

"We cannot tolerate such investors� such contracts are unbearable and can�t be entertained any more, let�s be serious so that we don't loose revenues in the hands of few individuals," said Mr Pinda.

He said the government would wait for recommendations from the CAG to make the required changes immediately. He blamed the municipality for leaving the terminal to be managed without a board or even a committee.

"Let us be firm when things go wrong, there is neither board nor committee to advice the management which cause them to do whatever they want," he said.

During the tour at the Kariakoo market the traders blamed the leaders for charging them hiked fees while providing poor services.

The Premier called the three municipalities of Kinondoni, Ilala and Temeke to ensure they improve the standards of the markets in their areas.

"Most of the markets have no important services like water and electricity, how can we expect traders to pay more?" he said. He also asked the three municipalities to conduct environmental impact assessments before allocating land for major investments.

"Many of the land problems happens because we have given land to investors without considering the impact of their business to the people," said Mr Pinda referring to authorities' decision to suspend operations at KTM Industry in Mbagala.

The factory has been closed pending rectification of sewerage infrastructure.

"It's unfortunate some leaders are granting permission for investors to build their industries in residential areas without taking into consideration of lives of those people," he said.
 
Hizi hela zinazotokana na parking hata kama si zote basi ni muhimu sehemu ya hiyo itumike kuboresha parking. sehemu kama pale stesheni karibu na uhamiaji kuna uwazi mkubwa. wangeweza jenga parking structure kubwa ya magari mengi tuu kupunguza kero. tatizo mamlaka zetu si wabunifu na hawako kimaendeleo.
hayo ya kufukuza wafanyakazi na kutowalipia NSSF na vingine ni muhimu kufuatiliwa maana wanatengeneza mabilioni na kunyanyasa wazawa.
 
"We cannot tolerate such investors� such contracts are unbearable and can�t be entertained any more, let�s be serious so that we don't loose revenues in the hands of few individuals," said Mr Pinda.



Inaonyesha unayajua madudu yanayofanyika, but is this all you can say or do?
 
Hii miradi inayosimamiwa na kingunge iangaliwa upwa kwani inakosesha serikali mapato.Waziri Mkuu alishuhudia ya UBT na Kariakoo,pia iangaliwe parking mjini.Huyu jamaa(Kingunge)aliwahi kupata tenda ya kukarabati kiwanda cha korosho cha Kibaha lakini alichofanya ni usanii tu wa kupiga rangi tena ya kupaka kwa brashi kama nyumba basi na akajichukulia mamilioni yake,hivyo usanii alianza zamani baada tu ya kifo cha Baba wa Taifa 1999.
 
Back
Top Bottom