Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,317
- 11,181
Chuo kikuu kikongwe zaidi duniani ambacho kinaendelea kutoa elimu ni kile kilichopo barani Afrika, nchini Morocco na ambacho kilianza msikitini(masjid) na kuendeshwa kwa mfumo wa madrasa.
Chuo kikuu hicho kilijengwa na bi Fatma kikiambatana na msikiti wakati wa ukhalifa wa Abbasiya ambao ulitawala mashariki ya kati, Ulaya na Afrika. Ukhalifa huo na watangulizi wao walitilia umuhimu mkubwa masuala ya elimu na hivyo kurithisha fikra hizo kwa kila watu wa eneo fulani.
Miongoni mwa wanafunzi wa chuo hicho ni papa Sylevester (2).Somo lililomvutia zaidi ni hesabu wakati huo Ulaya ikiwa haijui hata kuhesabu machungwa.
Mfumo wa kuhesabu hasa kwa kutumia kifaa cha Abacus alichojifunzo kutoka walimu wa chuo cha Alqarawiyen ulimfanya aonekane kama ni mchawi na hiyo ikawa ndiyo sababu ya Ulaya nzima kujifunzo na kuanza kuhesabu kutoka kanisani kwake.
Mahesabu mengine magumu na elimu ya astronomy alichukua kutoka dola ya kiislamu ya Andalasia.