Etaro Sekondari Yadhamiria kuwa na High School ya Somo la Kompyuta - Jimbo la Musoma Vijijini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

ETARO SEKONDARI YADHAMIRIA KUWA NA "HIGH SCHOOL" YA SOMO LA KOMPYUTA - HARAMBEE JUMAMOSI, 23.12.2023

Tarehe ya Harambee:
Jumamosi, 23.12.2023
Saa 3 asubuhi

Mahali:
Etaro Sekondari
Kijijini Etaro

Akaunti ya Shule:
Benki: NMB Musoma
Akaunti Na: 30301200341
Jina la Akaunti: Etaro Sekondari

Maabara zilizoko Etaro Sekondari:
(i) Maabara ya Bailojia
*Ilishajengwa na tayari inatumiwa

(ii) Maabara ya Kemia
*Serikali imetoa Tsh milioni 30 (Tsh 30m) kwa ujenzi wa maabara hii ambayo itakamilika kabla ya tarehe 15.1.2024. Tunaishukuru sana Serikali yetu kwa mchango huu.

(iii) Maabara ya Kompyuta
*Kompyuta 25 zimefungwa kwa msaada ya fedha kutoka Chuo Kikuu cha Northern Illnois, USA. Tunakishukuru sana Chuo hiki kwa mchango huu.

*Mafunzo ya Kompyuta yameanza kutolewa wiki hii hapo shuleni kwa kutumia Wahadhiri wa DIT ambao ndio wamepewe jukumu la kujenga Maabara ya Kompyuta shuleni hapo.

Headmaster Jacob Joseph Chagavalye na walimu wenzake wanapongezwa sana kwa ubunifu wao na udumishaji mzuri wa urafiki wao na Northern Illnois University - mfadhili wa computer lab ya Etaro Sekondari.

(iv) Maabara ya Fizikia
*Harambee ya Mbunge wa Jimbo itachangia ujenzi wa maabara hii ambayo imepangwa ikamilike kabla ya tarehe 1.3. 2024

"High School" ya Somo la Kompyuta:
Etaro Sekondari inajitayarisha (mwakani, Julai 2024) kuwa na Form V yenye mchepuo wa Physics, Mathematics & Computer Science na michepuo mingine ya masomo ya sayansi.

Taarifa nyingine za Etaro Sekondari:
Sekondari ya Etaro ilifunguliwa Mwaka 2006. Sekondari hii inahudumia vijiji vinne vya Kata ya Etaro. Vijiji hivyo ni: Busamba, Etaro, Mmahare na Rukuba (Kisiwa).

Etaro Sekondari ina wanafunzi 897. Wanafunzi wa Kidato cha nne (Form IV) wanaosoma somo la Fizikia ni 20 kati ya 146 (13.7%), na wale wanaosoma somo la Kemia ni 41 kati ya 146 (28.1%)

HARAMBEE & MCHANGO WAKO:
*Unakaribishwa sana kwenye Harambee yetu ya Jumamosi, 23.12.2023.

*Iwapo utashindwa kuhudhuria Harambee hiyo, tafadhali sana MCHANGO wako utume moja kwa moja kwenye Akaunti ya Etaro Sekondari.

Picha zilizoambatanishwa hapa
*Baadhi ya majengo ya Etaro Sekondari
*Shamba la shule: wanafunzi wanapata chakula shuleni hapo kutoka kwenye mavuno ya shamba lao

TUWEKE MIUNDOMBINU YA ELIMU YA SAYANSI KWENYE SHULE ZETU - tutawashawishi na kuwavutia wanafunzi wengi kuwa wanasayansi.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 20.12.2023
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-12-20 at 21.50.47.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-20 at 21.50.47.jpeg
    94.1 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-12-20 at 21.50.47(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-20 at 21.50.47(1).jpeg
    129.7 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-12-20 at 21.50.48.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-20 at 21.50.48.jpeg
    131.3 KB · Views: 3
Back
Top Bottom