Papa Francis ataka sala ya Baba Yetu ifanyiwe marekebisho

Papa Francis ataka sala ya Baba Yetu ifanyiwe marekebisho

Huyu bwana ana controversies nyingi sana,nadhani there is something behind the curtain.Lakini sishangai sana kwa kuwa ni Jesuit.Hata hivyo there are many important issues within the Catholic faith to consider which are not in order,this is very petty.
Naomba nikuelewe vizuri....eti..umesema..??
 
Mtabadilishiwa neno moja baada ya neno kwa lugha ya kidiplomasia ivyo hivyo hadi mwisho mtajikuta hamna Bible tena bali kitabu cha kishenzi sana.

Onaona, atabadili hilo neno la kwenye sala ya Baba Yetu, na ushoga na usagaji yuko njiani anakuja kuleta tafsiri nyingine ya neno la watu wanaofunga ndoa.

Maana ameisha wapigia kwenye neno usitutie katika vishawishi.

Na amewa-beep kwenye neno "wapenzi wa jinsia moja", nadhani mwaka 2019 atawapigia kabisa kuwa mapenzi ya jinsia moja kuwa ni ruksa.

Hizi dini ni foolish kabisa...
Wenye akili hujibu hoja kwa kuleta hoja kwenye jambo husika sio kuleta vioja
 
Wenye akili hujibu hoja kwa kuleta hoja kwenye jambo husika sio kuleta vioja

Socratic ,

Mkuu, kama hujaona hoja kwenye hiyo comment yangu uliyo quote hapo juu basi endelea vivyo hivyo mara paaaaapu, Papa anafuta dini yenu kabisa ndiyo utaelewa nilichoandika hapo juu kuwa ni hoja ama siyo.

Asante kwa kunitusi.
 
Kwa nini abadilishe leo hii? Je wenzake miaka yote hawakuliona hilo kosa?
Tafsiri,kesha kujuza ilitafsiriwa vibaya,
Nikujuze kitu ambacho unaweza usiamini lkn ni kweli,
Hivi unajua hata neno takatifu YAWEH lilitafsiriwa vibaya na haliitwi hivyo,lafudhi za mtafsir ndo zilifasiri hivi,hivo so sahihi kusema Yaweh,
Hili ni jina takatifu la Mungu ambalo waisraeli ilikuwa marufuku kulitamka hovyo,kuhani ndo alikuwa akilitamka lkn halikuwa jina km tunavyoliita sasa Bali zilikuwa ni herufu tatu za kiebrania na zilitamkwa kinyume,
 
Kwa Wakatoliki, hilo linawezekana kabisa. Maana ktk imani yao Papa anamamlaka ya kubadili amri za Mungu🙁🙁 Uprotestant ulianza ili kuondoa nadharia hii ya Mwanadamu kujibandika Mamlaka ya Mungu. Cha ajabu miaka mia tano (500) baada ya Martin Luther, Waprotestant wanaungana na ukatoliki🙁🙁🙁🙁🙁 Hakuna mwanadamu mwenye mamlaka ya kubadili chochote kilichoandikwa kwenye Biblia. Ufunuo 22:19 "Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki".
Mmeumbwa na kufundishwa kulichukia kanisa mama ndo maana kila wafanyacho mnawaponda,huku mkisahau kuwa nguvu yao ndo imefanya hata nyie Leo muwepo,
Yapo mambo meeengi tafsiri ilikosewa japo maana yake inabaki pale pale hasa unapotumia lugha asilia,
 
Hiyo sala imeandikwa kwenye bible anataka aibadilishe.
Hahaha ndo maana hua nasema dini nuksi tu, wote mnachezeshewa story za the avengers, black panther ndiyo starring. Huyu anataka kubadilisha hiki, upande wa pili wao ni full kuchinjana ka kuku, upande wa tatu wazee wa depression hawana raha hata kidogo, hii amani iko wapi? mbona ni the total opposite? Inabidi wakati ufike watu mfungue akili, hakuna kifungo kikali ka cha dini, madawa ya kulevya ni rahisi mara mia kuacha kuliko mambo yaliyojazwa kuchwani toka utotoni.
Rudia upya kusoma utaelewa jambo
Ondoa mkurupuko unaosukumwa na upinzani
 
MTU yule atakayeondoa neno ktk biblia NAYE Mungu atamwondelea sehem yake.

Nayule atakayeongeza neno ktk maandiko matakatifu ,NAYE Mungu atamwongezea mapigo km alivyoyataja..

Duuuuuhhhhh hatujamaliza LA Israel ,,tumeshaletewa LA Papa ..ivi kweli neno LA Mungu linahojiwa au kujadiliwa ????????.


The end is near !!.
Mi nnadhani mnamatatizo ya kufikiri,
Umeambiwa tafsiri ilikosewa,siyo neno asili linaondolewa,
Ipo hivi,
Neno ktk lugha asili ya sala hiyo ni ile ile lkn aliyetafsiri kuileta sala hiyo kwa kilatini nk alilitafsiri vibaya ambapo ndo linatuletea kiswahili cha usitutie,
Acha tutafute lugha asili ya hii sala halafu tuliweke neno kwenye translator tuone nn kitatukia,
 
Naomba nikuelewe vizuri....eti..umesema..??
Nimesema nilichosema kwamba Pope Francis ni Jesuit,an underground society,kwa hiyo controversies zake hazinishangazi.Nimesema pia kwamba hili la sala ni dogo sana,yapo mambo mengi ya kiimani katika imani ya Kanisa Katoliki ambayo hayako sawa,aya-address hayo,hili la sala ni very petty.
 
Mimi ni MKATOLIK ,ILA HILI LIMENIFANYA MOYO WANGU KUSHIKWA NAGANZI.
Acha kuwa mkatoliki mbumbumbu,
Umeambiwa TAFSIR
Ilikosewa,inamaana asili ya neno kwa lugha yake asilia inatamkwa sahihi na inabaki vile vile,ila mtafsiri wa kulileta ktk kilatini na lugha tunazotumia alitafsiri kimakosa,
Hivi Mungu anamtia MTU ktk makosa ama anamuokoa MTU asipatwe kishawishi?
 
Ni tafsiri ndio ilikosewa lakini watu walishaiweka sawa toka karne ya kumi na nane.
Hata mimi siku zote nikiomba hii sala natumia neno "usituache tukaingia majaribuni"
Naaaam
Mkuu hivi unajua hata hili neno ambalo tunaliita km jina la MUNGU tafsiri ililikosea maana asili yake zilikuwa herufi ambazo kwa wayahudi hazikutamkika na walikiheshimu na hivyo kutolitamka isipokuwa kuhani mkuu alizitamka Mara moja tu kwa mwaka,sasa mtafsiri alipotaka kuzitamka hizo herufi TAKATIFU ikaskika Yahweh na ndo tunavyoziita mpaka Leo japo maana ni ile ile,jaribu kutafuta wataalamu watakujiza
 
Papa Francis ipo siku atataka kanisa liruhusu ushoga.
Kila Mara anataka kubandika vitu anavyoona yeye ni sahihi bila kujali athari zake.
Atabomoa misingi ya kanisa letu pendwa huyu babu
Atataka vipi wakati mlimvumishia tayari katambua?
 
Huenda wewe ni Msabato....labda...


Ila ngoja nikuulize! Je! Mungu anaweza mtega kiumbe chake na kukiacha kiingie dhambini..?
Mimi sio Msabato,ila soma Waebrania 12:5-12;Yakobo1:2-4 upate majibu ya maswali yako.
 
abadilishe tu maana yeye ndio mungu wa wakatoliki
Ulivyo mjinga unaongea kutafuta sifa na kuburudisha humu huku ukisahau kuwa kwa Mungu hata unachoongea humu kinakutia hatiani ama la,endelea kuropka maana hazina yako utaikuta juu,au unadhani wachina wameweka kiwambo cha kuzuia Mungu asiyaone makosa tunayotenda kwenye net,
 
Mimi si msomaji mzuri wa biblia lakini ninachofahamu katika kitabu cha Mathayo 6 msitari wa 7 Yesu alitoa agizo kwamba wakati wa kusali watu wasipayuke payuke kama watu wa mataifa na badala yake akafundisha hiyo sala ambayo ndani yake kuna huo mstari unaoomba Mungu asitutie majaribuni/katika vishawishi. Ina maana Yesu mwenyewe alikosea kutamka hivyo?
Umeisoma kutoka lugha gani,
Km unaisoma ktk lugha asilia alotumia Yesu sawa, lkn unaisoma ktk kiswahili na kiingereza na kilatini ambacho tafsiri ilikosewa kwa neno hilo
 
"Usitutie katika vishawishi" ni sawa na "usituache tuingie katika vishawishi" ? May be, may be not..
Usitutie ni usituingize
Haya ni tofauti na usituache tukaingia ktk kishawishi,
Na maana inajieleza kabisa km haujafungwa na uhasama,Mungu hamtii MTU majaribuni/kishawishi
Ila Mungu anatusaidia kutoingia kishawishini
 
Back
Top Bottom