Papa Francis ataka sala ya Baba Yetu ifanyiwe marekebisho

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,610
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameomba maombi maarufu ya Kikristo ya Baba Yetu yafanyiwe marekebisho.

Anataka sehemu ambayo huzungumzia vishawishi ilitafsiriwa vibaya.

Asema tafsiri kwamba "Usitutie katika vishawishi (majaribu/majaribuni)" iangaziwe upya akisema tafsiri iliyofanywa si sahihi kwa sababu Mungu huwa hawaongozi binadamu kutenda dhambi.

Papa amependekeza watu watumie "usituache tukaingia katika vishawishi (majaribu/majaribuni)" badala yake.

Alitoa pendekezo hilo akizungumza katika runinga ya Italia Jumatano usiku.

Ombi la Baba Yetu ndilo linalofahamika vyema zaidi miongoni mwa maombi ya Kikristo.

Papa Francis amesema Kanisa Katoliki nchini Ufaransa sasa linatumia tafsiri hiyo ya "usituache tukaingia katika vishawishi" kama mbadala, na kwamba jambo kama hilo linafaa kufanywa kote duniani.

"Usiniache nikaingia kwenye vishawishi kwa sababu ni mimi nitakayeanguka, si Mungu anayetutia katika vishawishi na kisha kutazama nilivyoanguka," aliambia runinga ya TV2000, runinga ya kanisa Katoliki Italia.

"Baba hawezi kufanya hivyo, baba hukusaidia huinuke upesi."

Ni tafsiri kutoka kwa tafsiri ya biblia ya Kilatini ya karne ya nne ambayo iliidhinishwa rasmi na kanisa Katoliki karne ya 16, ambayo ilitafsiriwa kutoka kwa maandiko ya kale ya Kigiriki, Kiebrania na Kiaramaic.

Tangu kuanza kuhudumu kama Papa, Papa Francis hajasita kugusia masuala tata na amekabiliana na baadhi ya mambo moja kwa moja, wachanganuzi wa mambo ya Vatican wanasema.

Alikuwa awali amesema kwamba Kanisa Katoliki linafaa kuwaomba radhi wapenzi wa jinsia moja kutoka na vile ambavyo limewatazama na yale limewatendea kwa miaka mingi.

Aidha, alilinganisha vituo vya kuwazuilia wahamiaji Ulaya na vituo vilivyotumiwa na Wanazi kuwazuilia na kuwaua Wayahudi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Chanzo: BBC
 
Kabadili maana au kabadili neno? Kwanza hilo neno usitutie kwenye kishawishi haiko hivyo dunia nzima bali imekuwa hivyo kutokana na afsiri ya kiswahili. Mfano hata kwa kiswahili neno usitutie kinaweza kuwa usitupitishe ,usituweke, utuepushe nk maneno tofauti maana moja. Mfano mtu akisema dunia na mwengine akasema ulimwengu kwahiyo hapa issue ni maana wala siyo neno
 
Kwa nini abadilishe leo hii? Je wenzake miaka yote hawakuliona hilo kosa?
 
Kwa Wakatoliki, hilo linawezekana kabisa. Maana ktk imani yao Papa anamamlaka ya kubadili amri za Mungu🙁🙁 Uprotestant ulianza ili kuondoa nadharia hii ya Mwanadamu kujibandika Mamlaka ya Mungu. Cha ajabu miaka mia tano (500) baada ya Martin Luther, Waprotestant wanaungana na ukatoliki🙁🙁🙁🙁🙁 Hakuna mwanadamu mwenye mamlaka ya kubadili chochote kilichoandikwa kwenye Biblia. Ufunuo 22:19 "Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki".
 
Ufunuo 22:19 mwandishi hazungumzii biblia kwakua hakukua na hicho kitabu wakati huo, anazungumzia kitabu chake cha "ufunuo". Wakati huo kila kitabu, kilikua kivyake na kulikua na mamia ya vitabu. Ni kundi tu la watu kama wewe na mimi wakaamua kivichuja na kuviunganisha vile walivyoona vinafaa kuunda biblia.
 
Sidhani kama nia ni kubadilisha amri za Mungu...!!nia kuiweka katika maana sahihi...!!!
 
Hiyo sala imeandikwa kwenye bible anataka aibadilishe.
Hahaha ndo maana hua nasema dini nuksi tu, wote mnachezeshewa story za the avengers, black panther ndiyo starring. Huyu anataka kubadilisha hiki, upande wa pili wao ni full kuchinjana ka kuku, upande wa tatu wazee wa depression hawana raha hata kidogo, hii amani iko wapi? mbona ni the total opposite? Inabidi wakati ufike watu mfungue akili, hakuna kifungo kikali ka cha dini, madawa ya kulevya ni rahisi mara mia kuacha kuliko mambo yaliyojazwa kuchwani toka utotoni.
 
MTU yule atakayeondoa neno ktk biblia NAYE Mungu atamwondelea sehem yake.

Nayule atakayeongeza neno ktk maandiko matakatifu ,NAYE Mungu atamwongezea mapigo km alivyoyataja..

Duuuuuhhhhh hatujamaliza LA Israel ,,tumeshaletewa LA Papa ..ivi kweli neno LA Mungu linahojiwa au kujadiliwa ????????.

The end is near !!.
 
Kwa Wakatoliki, hilo linawezekana kabisa. Maana ktk imani yao Papa anamamlaka ya kubadili amri za Mungu🙁🙁 Uprotestant ulianza ili kuondoa nadharia hii ya Mwanadamu kujibandika Mamlaka ya Mungu. Cha ajabu miaka mia tano (500) baada ya Martin Luther, Waprotestant wanaungana na ukatoliki🙁🙁🙁🙁🙁 Hakuna mwanadamu mwenye mamlaka ya kubadili chochote kilichoandikwa kwenye Biblia. Ufunuo 22:19 "Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki".
Umemaliza mkuuu!.
 
Mimi ni MKATOLIK ,ILA HILI LIMENIFANYA MOYO WANGU KUSHIKWA NAGANZI.
 
Ufunuo 22:19 mwandishi hazungumzii biblia kwakua hakukua na hicho kitabu wakati huo, anazungumzia kitabu chake cha "ufunuo". Wakati huo kila kitabu, kilikua kivyake na kulikua na mamia ya vitabu. Ni kundi tu la watu kama wewe na mimi wakaamua kivichuja na kuviunganisha vile walivyoona vinafaa kuunda biblia.
Safi kabisa uko vizuri
 
Papa Francis ipo siku atataka kanisa liruhusu ushoga.
Kila Mara anataka kubandika vitu anavyoona yeye ni sahihi bila kujali athari zake.
Atabomoa misingi ya kanisa letu pendwa huyu babu
 
Kabadili maana au kabadili neno? Kwanza hilo neno usitutie kwenye kishawishi haiko hivyo dunia nzima bali imekuwa hivyo kutokana na afsiri ya kiswahili. Mfano hata kwa kiswahili neno usitutie kinaweza kuwa usitupitishe ,usituweke, utuepushe nk maneno tofauti maana moja. Mfano mtu akisema dunia na mwengine akasema ulimwengu kwahiyo hapa issue ni maana wala siyo neno
====
DUNIA ni earth, Ulimwengu ni universe
 
Back
Top Bottom