ZEE LA HEKIMA
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 1,422
- 1,851
NIV (yaani New International Version) Bible inasema:...lead us not into temptation. KJV (yaani King James Version) Bible inasema:..lead us not into temptation. Amplified Bible inasema:....lead (bring) us not into temptation. Biblia ya Kiswahili inasema:...usitutie majaribuni. Biblia zote zilizotafsiriwa toka lugha mbalimbali zinasema USITUTIE MAJARIBUNI. Mt 4:1 inasema..Yesu ALIPANDISHWA NA ROHO (yaani Roho Mtakatifu) nyikani ILI AKAJARIBIWE NA IBILISI. Yaani ni Mungu Baba mwenyewe alimtia Yesu majaribuni. Ni kanuni ya Mungu kumjaribu mtu kwa kumwacha kwenye majaribu (lakini SIO MUNGU KUMJARIBU YEYE). Kwa hivyo Biblia inaposema usitutie majaribuni IKO SAWA KABISA. MUNGU HAKUJARIBU YEYE lakini anakupeleka utakapojaribiwa. Anafanya hivyo ili kukupima kama unampenda kiasi kwamba unakataa kutenda dhambi (kama Yusufu alivyokataa kulala na mke wa Potifa). Ni mtihani wa kutaka kujua umefika wapi kiimani. Na wote mkumbuke kwamba Yesu hakuanzisha dhehebu. Alikuja kuhubiri tu habari njema za ufalme wa Mungu. Wewe unayetetea dhehebu lako hujui.uliko. Kiongozi wa dhehebu LAZIMA abadili mambo 'kidogo' ili dhehebu lake liwe tofauti na mengine. Dhehebu halimpeleki mtu mbinguni bali 'kuishi neno' (yaani kuishi sawasawa na neno la Mungu) ndiko kunampeleka mtu mbinguni