FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 40,921
- 47,014
"Usitutie katika vishawishi" ni sawa na "usituache tuingie katika vishawishi" ? May be, may be not..
Mkuu kumbuka yeye mpaka kwa kiitaliano kaona maana si nzuri, na wala hajui kiswahili linatamkaje, kwahyo ni kweli kaona kuna changamoto.Kabadili maana au kabadili neno? Kwanza hilo neno usitutie kwenye kishawishi haiko hivyo dunia nzima bali imekuwa hivyo kutokana na afsiri ya kiswahili. Mfano hata kwa kiswahili neno usitutie kinaweza kuwa usitupitishe ,usituweke, utuepushe nk maneno tofauti maana moja. Mfano mtu akisema dunia na mwengine akasema ulimwengu kwahiyo hapa issue ni maana wala siyo neno
Kumbuka Yesu hakuisema kwa kiswahili, alisema kwa lugha yake then watu wakatafsiri kwa lugha tofauti tofauti. Na sifa ya lugha hua haijitoshelezi huwezi kupata maana ya kila neno kwa lugha yako, ndio maana hata kiswahili kina baadhi ya maneno ya kiingereza.Mimi si msomaji mzuri wa biblia lakini ninachofahamu katika kitabu cha Mathayo 6 msitari wa 7 Yesu alitoa agizo kwamba wakati wa kusali watu wasipayuke payuke kama watu wa mataifa na badala yake akafundisha hiyo sala ambayo ndani yake kuna huo mstari unaoomba Mungu asitutie majaribuni/katika vishawishi. Ina maana Yesu mwenyewe alikosea kutamka hivyo?
Wenyekili zetu tulishaitupilia mbali maigizo hayaKiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameomba maombi maarufu ya Kikristo ya Baba Yetu yafanyiwe marekebisho.
Anataka sehemu ambayo huzungumzia vishawishi ilitafsiriwa vibaya.
Asema tafsiri kwamba "Usitutie katika vishawishi (majaribu/majaribuni)" iangaziwe upya akisema tafsiri iliyofanywa si sahihi kwa sababu Mungu huwa hawaongozi binadamu kutenda dhambi.
Papa amependekeza watu watumie "usituache tukaingia katika vishawishi (majaribu/majaribuni)" badala yake.
Alitoa pendekezo hilo akizungumza katika runinga ya Italia Jumatano usiku.
Ombi la Baba Yetu ndilo linalofahamika vyema zaidi miongoni mwa maombi ya Kikristo.
Papa Francis amesema Kanisa Katoliki nchini Ufaransa sasa linatumia tafsiri hiyo ya "usituache tukaingia katika vishawishi" kama mbadala, na kwamba jambo kama hilo linafaa kufanywa kote duniani.
"Usiniache nikaingia kwenye vishawishi kwa sababu ni mimi nitakayeanguka, si Mungu anayetutia katika vishawishi na kisha kutazama nilivyoanguka," aliambia runinga ya TV2000, runinga ya kanisa Katoliki Italia.
"Baba hawezi kufanya hivyo, baba hukusaidia huinuke upesi."
Ni tafsiri kutoka kwa tafsiri ya biblia ya Kilatini ya karne ya nne ambayo iliidhinishwa rasmi na kanisa Katoliki karne ya 16, ambayo ilitafsiriwa kutoka kwa maandiko ya kale ya Kigiriki, Kiebrania na Kiaramaic.
Tangu kuanza kuhudumu kama Papa, Papa Francis hajasita kugusia masuala tata na amekabiliana na baadhi ya mambo moja kwa moja, wachanganuzi wa mambo ya Vatican wanasema.
Alikuwa awali amesema kwamba Kanisa Katoliki linafaa kuwaomba radhi wapenzi wa jinsia moja kutoka na vile ambavyo limewatazama na yale limewatendea kwa miaka mingi.
Aidha, alilinganisha vituo vya kuwazuilia wahamiaji Ulaya na vituo vilivyotumiwa na Wanazi kuwazuilia na kuwaua Wayahudi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Chanzo: BBC
Vipi kuhusu"Utusamehe kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea" Nani mwenye kutoa msamaha zaidi kati Mungu na sie Wanadamu? Manake sie ndiyo tunatakiwa tusamehe kama yeye anavyotusameheKiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameomba maombi maarufu ya Kikristo ya Baba Yetu yafanyiwe marekebisho.
Anataka sehemu ambayo huzungumzia vishawishi ilitafsiriwa vibaya.
Asema tafsiri kwamba "Usitutie katika vishawishi (majaribu/majaribuni)" iangaziwe upya akisema tafsiri iliyofanywa si sahihi kwa sababu Mungu huwa hawaongozi binadamu kutenda dhambi.
Papa amependekeza watu watumie "usituache tukaingia katika vishawishi (majaribu/majaribuni)" badala yake.
Alitoa pendekezo hilo akizungumza katika runinga ya Italia Jumatano usiku.
Ombi la Baba Yetu ndilo linalofahamika vyema zaidi miongoni mwa maombi ya Kikristo.
Papa Francis amesema Kanisa Katoliki nchini Ufaransa sasa linatumia tafsiri hiyo ya "usituache tukaingia katika vishawishi" kama mbadala, na kwamba jambo kama hilo linafaa kufanywa kote duniani.
"Usiniache nikaingia kwenye vishawishi kwa sababu ni mimi nitakayeanguka, si Mungu anayetutia katika vishawishi na kisha kutazama nilivyoanguka," aliambia runinga ya TV2000, runinga ya kanisa Katoliki Italia.
"Baba hawezi kufanya hivyo, baba hukusaidia huinuke upesi."
Ni tafsiri kutoka kwa tafsiri ya biblia ya Kilatini ya karne ya nne ambayo iliidhinishwa rasmi na kanisa Katoliki karne ya 16, ambayo ilitafsiriwa kutoka kwa maandiko ya kale ya Kigiriki, Kiebrania na Kiaramaic.
Tangu kuanza kuhudumu kama Papa, Papa Francis hajasita kugusia masuala tata na amekabiliana na baadhi ya mambo moja kwa moja, wachanganuzi wa mambo ya Vatican wanasema.
Alikuwa awali amesema kwamba Kanisa Katoliki linafaa kuwaomba radhi wapenzi wa jinsia moja kutoka na vile ambavyo limewatazama na yale limewatendea kwa miaka mingi.
Aidha, alilinganisha vituo vya kuwazuilia wahamiaji Ulaya na vituo vilivyotumiwa na Wanazi kuwazuilia na kuwaua Wayahudi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Chanzo: BBC
Kisichobadilika ni "neno" la Mungu sio lugha za wanadamu, lugha zetu hubadilika kutoka muda kwenda muda na kwa sbb ya mabadiliko hayo baadhi ya maana za lugha za kale huanza kupotea au kupotoshwa.Kwa Wakatoliki, hilo linawezekana kabisa. Maana ktk imani yao Papa anamamlaka ya kubadili amri za Mungu🙁🙁 Uprotestant ulianza ili kuondoa nadharia hii ya Mwanadamu kujibandika Mamlaka ya Mungu. Cha ajabu miaka mia tano (500) baada ya Martin Luther, Waprotestant wanaungana na ukatoliki🙁🙁🙁🙁🙁 Hakuna mwanadamu mwenye mamlaka ya kubadili chochote kilichoandikwa kwenye Biblia. Ufunuo 22:19 "Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki".
Hivi ni vitu viwili tofauti kabisa!====
DUNIA ni earth, Ulimwengu ni universe
Eti Mungu mwenye upendo wote anaweza kukuingiza majaribuni...?? Hebu nijibuHuyu jamaa sasa hv atabadili sehemu yenye jina.la Yesu awekwe Yeye
Kwa akili yako ukadhani anarekebisha kiswahili..??Kwanza anatanatafsiri kutoka lugha ipi kwenda lugha ipi? Maana "usitutie katika vishawishi" ni kiswahili, sasa original yake ni ipi na ni lugha gani
Haswa. naona jamaa anadhani ni kitu kimoja.Hivi ni vitu viwili tofauti kabisa!
Hata km ni kiyunani, hiyo lugha co km anaijua PAPA peke yake, na unavyozungumzia tafsir unakuwa unahusisha lugha. Bible imetafsiriwa kwa lugha nyingi. Na huwezi tafsiri maana, huyo anahangaika na maneno tu, km ni maana watu walisha maanisha hivyo kitambo hakuwa wanamsubiri PAPA.Kwa akili yako ukadhani anarekebisha kiswahili..??
Ndio, why not??Eti Mungu mwenye upendo wote anaweza kukuingiza majaribuni...?? Hebu nijibu