Papa Francis ataka sala ya Baba Yetu ifanyiwe marekebisho

Papa Francis ataka sala ya Baba Yetu ifanyiwe marekebisho

Implication ya mabadiliko haya ni kwamba pale mtu akipatwa na majanga au akitenda dhambi ni kwamba ameachwa na mungu afanye hivyo. Na kwakua amekuacha ufanye hivyo itatafsiliwa amekubaliana na shetani kutekeleza dhamira yake ovu. Inaondoa weakness na freedom ya nafsi na haki ya kuadhibu kwani kama amekuacha na ulimuomba asikuache why akulaumu tena?

semantically nadhani anahitaji kutoa somo la maana au kukubali debate katika hayo mabadiliko....
 
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameomba maombi maarufu ya Kikristo ya Baba Yetu yafanyiwe marekebisho.

Anataka sehemu ambayo huzungumzia vishawishi ilitafsiriwa vibaya.

Asema tafsiri kwamba "Usitutie katika vishawishi (majaribu/majaribuni)" iangaziwe upya akisema tafsiri iliyofanywa si sahihi kwa sababu Mungu huwa hawaongozi binadamu kutenda dhambi.

Papa amependekeza watu watumie "usituache tukaingia katika vishawishi (majaribu/majaribuni)" badala yake.

Alitoa pendekezo hilo akizungumza katika runinga ya Italia Jumatano usiku.

Ombi la Baba Yetu ndilo linalofahamika vyema zaidi miongoni mwa maombi ya Kikristo.

Papa Francis amesema Kanisa Katoliki nchini Ufaransa sasa linatumia tafsiri hiyo ya "usituache tukaingia katika vishawishi" kama mbadala, na kwamba jambo kama hilo linafaa kufanywa kote duniani.

"Usiniache nikaingia kwenye vishawishi kwa sababu ni mimi nitakayeanguka, si Mungu anayetutia katika vishawishi na kisha kutazama nilivyoanguka," aliambia runinga ya TV2000, runinga ya kanisa Katoliki Italia.

"Baba hawezi kufanya hivyo, baba hukusaidia huinuke upesi."

Ni tafsiri kutoka kwa tafsiri ya biblia ya Kilatini ya karne ya nne ambayo iliidhinishwa rasmi na kanisa Katoliki karne ya 16, ambayo ilitafsiriwa kutoka kwa maandiko ya kale ya Kigiriki, Kiebrania na Kiaramaic.

Tangu kuanza kuhudumu kama Papa, Papa Francis hajasita kugusia masuala tata na amekabiliana na baadhi ya mambo moja kwa moja, wachanganuzi wa mambo ya Vatican wanasema.

Alikuwa awali amesema kwamba Kanisa Katoliki linafaa kuwaomba radhi wapenzi wa jinsia moja kutoka na vile ambavyo limewatazama na yale limewatendea kwa miaka mingi.

Aidha, alilinganisha vituo vya kuwazuilia wahamiaji Ulaya na vituo vilivyotumiwa na Wanazi kuwazuilia na kuwaua Wayahudi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Chanzo: BBC
Tukisema ni mpinga Kristo mnabisha. Mwanzilishi wa Sala kuu ni Yesu Kristo. Lakini hili Pagani la kilatini linampinga Na kumkosoa Yesu Kristo
 
Papa Francis ipo siku atataka kanisa liruhusu ushoga.
Kila Mara anataka kubandika vitu anavyoona yeye ni sahihi bila kujali athari zake.
Atabomoa misingi ya kanisa letu pendwa huyu babu
Kwa akili yako unadhani "kakurupuka" yeye kama yeye?
 
Kwa akili yako unadhani "kakurupuka" yeye kama yeye?
Rudi ukasome thread vizuri.
Hata kama hajakurupuka yeye anaushawishi Mkubwa zaidi kwa kanisa kuliko mtu mwingine yeyote.
Aache kubadili misingi ya kanisa kama channel za radio tu
 
Kwa Wakatoliki, hilo linawezekana kabisa. Maana ktk imani yao Papa anamamlaka ya kubadili amri za Mungu🙁🙁 Uprotestant ulianza ili kuondoa nadharia hii ya Mwanadamu kujibandika Mamlaka ya Mungu. Cha ajabu miaka mia tano (500) baada ya Martin Luther, Waprotestant wanaungana na ukatoliki🙁🙁🙁🙁🙁 Hakuna mwanadamu mwenye mamlaka ya kubadili chochote kilichoandikwa kwenye Biblia. Ufunuo 22:19 "Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki".
Kuna tofauti kati ya KUBADILI na KUTAFSIRI
 
Kwa Wakatoliki, hilo linawezekana kabisa. Maana ktk imani yao Papa anamamlaka ya kubadili amri za Mungu🙁🙁 Uprotestant ulianza ili kuondoa nadharia hii ya Mwanadamu kujibandika Mamlaka ya Mungu. Cha ajabu miaka mia tano (500) baada ya Martin Luther, Waprotestant wanaungana na ukatoliki🙁🙁🙁🙁🙁 Hakuna mwanadamu mwenye mamlaka ya kubadili chochote kilichoandikwa kwenye Biblia. Ufunuo 22:19 "Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki".
Acha kusoma biblia fikra ndogo mkuu, hiyo nukuu haimaanishi kubadili meneno bali maana. Kubadilika kwa maneno katika lugha ni kulingana na ukuaji wa lugha husika. Mfano zamani tz kulikuwa na neno washika dau kwa lugha ya kiswahili ( partners) leo tuna nano wadau ( partners). Juzi tulikuwa na makanikia leo tuna mashobo, hata ni mabadiliko ya maneno tu ila maana ni ile ile. Mfano kwa maelezo ya pope kwamba kusema 'usitutie katika kishawishi ni tafsiri mbaya kwasababu Mungu hawezi kumtia mtu kwenye kishawishi bali tafsiri nzuri iwe usituache tukaingia kwenye ushawishi' kimbuka maandiko yanasema Mungu hamjaribu mtu bali hujaribiwa na tamaa zake mwenyewe, na tamaa ikichukua mimba huzaa dhambi na dhambi ikishakomaa huzaa mauti. Kwa taarifa yako pia hii biblia tuliyonayo ni matokeo ya tafsiri kwahiyo kinachotakiwa kibaki katika uhalisia ni maana wala siyo maneno
 
MTU yule atakayeondoa neno ktk biblia NAYE Mungu atamwondelea sehem yake.

Nayule atakayeongeza neno ktk maandiko matakatifu ,NAYE Mungu atamwongezea mapigo km alivyoyataja..

Duuuuuhhhhh hatujamaliza LA Israel ,,tumeshaletewa LA Papa ..ivi kweli neno LA Mungu linahojiwa au kujadiliwa ????????.


The end is near !!.
Una uelewa finyu sana kwenye maandiko na historia ya ukristo mkuu. Kubadili kunakomaanishwa na biblia ni kusema usiue wewe ukasema ua au ukairemba remba kwamba usiue lakini ukichokozwa waweza kuua . Kumbuka biblia ilitafsiriwa na watu tena kwa lugha ambazo kwasasa zimebadilika sana maana kwahiyo unaweza kukuta kitu kinakosa maana.
 
HAPA MADA INGEKUWA JE NI KWELI MUNGU ANATUTIA KWENYE VISHAWISHI? KAMA JIBU NI NDIYO BASI NENO USITUTIE KATIKA MAJARIBU / VISHAWISHI IKO SAWA

LAKINI KAMA MUNGU HATUWEKI KWENYE MAJARIBU BASI TAFSIRI ASITUACHE TUKAINGIA MAJARIBUNI IKO SAHIHI. MAANA KUMBE TUNAINGIA WENYEWE PALE MUNGU ANAPOTUACHA
 
hivi mpaka leo biblia imeshabadilishwa mara ngapi? huu ni utani
 
Mimi si msomaji mzuri wa biblia lakini ninachofahamu katika kitabu cha Mathayo 6 msitari wa 7 Yesu alitoa agizo kwamba wakati wa kusali watu wasipayuke payuke kama watu wa mataifa na badala yake akafundisha hiyo sala ambayo ndani yake kuna huo mstari unaoomba Mungu asitutie majaribuni/katika vishawishi. Ina maana Yesu mwenyewe alikosea kutamka hivyo?
 
hivi mpaka leo biblia imeshabadilishwa mara ngapi? huu ni utani
Kijana biblia haibadilishwi ila biblia inaweza kufanyiwa tafsiri sahihi kulingana na ukuaji wa lugha. Mfano kuna neno linasema ' yesu akasema ni vigumu tajiri kuingia mbinguni kuliko ngamia kuingia kwenye tundu la sindano' sasa kwa akili na uelewa wako unadhani Yesu alikuwa anaongelea sindano ipi ya chereheni au. Hii ndiyo maana biblia inahitaji masomo ili ueweze kuelewa maana iliyotakiwa wasomaji wapate na mazingira ya wakati hayo yanaandikwa. Mfano neno hilo la tajiri linataka tu watu waone jinsi gani ilivyo ngumu kwa matajiri kuingia kwenye ufalme wa Mungu kutokana na wao kuweka tumaini lao katika mali. Kwahiyo hata kama mtu atasema ni vigumu kwa tajiri kuingia kwenye ufalme wa mbinguni kuliko Ng'ombe kuingia kwenye tundu la sindano bado maana inabaki ile ile ya ugumu wa jambo husika. Kwahiyo cha msingi ni kutunza maana siyo kukariri maneno.
 
Wafuasi mna kazi bora niendelee kuwa mpagani
 
Back
Top Bottom