Papa Francis ataka sala ya Baba Yetu ifanyiwe marekebisho

Papa Francis ataka sala ya Baba Yetu ifanyiwe marekebisho

Kwenye biblia mbona kuna watu Mungu aliwatia katika vishawishi? Watu wote waliojaribiwa na shetani walipata idhini ya Mungu tena kwa majadiliano. Aliruhusu watiwe vishawishini lakini akaomba shetani asiangamize roho zao.
Hilo ndo chimbuko la hilo neno kwenye sala ya bwana au baba yetu
 
Kabadili maana au kabadili neno? Kwanza hilo neno usitutie kwenye kishawishi haiko hivyo dunia nzima bali imekuwa hivyo kutokana na afsiri ya kiswahili. Mfano hata kwa kiswahili neno usitutie kinaweza kuwa usitupitishe ,usituweke, utuepushe nk maneno tofauti maana moja. Mfano mtu akisema dunia na mwengine akasema ulimwengu kwahiyo hapa issue ni maana wala siyo neno
Kuna haja ya kurudi shule na kusoma upya, kwanzia kiswahili mpaka biblia inakuchanga
 
Duh hii dini hii kila siku ammendment inafanywa na wanaadamu tena katika point muhimu ya sala
 
Kumbuka Yesu hakuisema kwa kiswahili, alisema kwa lugha yake then watu wakatafsiri kwa lugha tofauti tofauti. Na sifa ya lugha hua haijitoshelezi huwezi kupata maana ya kila neno kwa lugha yako, ndio maana hata kiswahili kina baadhi ya maneno ya kiingereza.
Ukisoma biblia ya kiingereza na ya kiswahili kuna maneno yanatogautiana kabisa kimaana
Kama ndivyo basi kuna uwezekano mkubwa kwamba yapo mengi kwenye biblia ambayo yametafsiriwa ndivyo sivyo.
 
Kama ndivyo basi kuna uwezekano mkubwa kwamba yapo mengi kwenye biblia ambayo yametafsiriwa ndivyo sivyo.
Ndio maana yake, kwa mfano ukisoma biblia ya kiingereza king James version jina la Mungu ambalo ni Jehova wenyewe wameliondoa nakutumia Lord, Lord maana yake ni Bwana na si Jehova.
Yapo maneno mengi ambayo baada ya kutafsiriwa yamebadikisha maana
 
Ndio maana yake, kwa mfano ukisoma biblia ya kiingereza king James version jina la Mungu ambalo ni Jehova wenyewe wameliondoa nakutumia Lord, Lord maana yake ni Bwana na si Jehova.
Yapo maneno mengi ambayo baada ya kutafsiriwa yamebadikisha maana
Ahsante kwa ufafanuzi. Sisi waswahili kumwita Jehova kwa jina la Mungu sijui hilo neno Mungu lilikuwa na maana gani?!
 
Ahsante kwa ufafanuzi. Sisi waswahili kumwita Jehova kwa jina la Mungu sijui hilo neno Mungu lilikuwa na maana gani?!
Neno Mungu ni cheo tu, na wapo Mungu wengi tu huku ulimwenguni. Ndio maana hata yeye alisema usiwe na miungu mingine ila yeye. Miungu ni wingi wa mungu.
Pia akaonya usilitaje jina lake bure, hakumaanisha jina mungu bali jina lake
 
Km nakumbuka vizur baadhi ya maneno, ni kwmb Bwana Yesu Kristoaliwafundisha wanafunzi wake kwa kuwaambia kuwa..."msalipo salini hivi......", kwa hyo kwa ufaham wng ni kwmb papa anampinga Bwana Yesu Kristo
 
Kwa Wakatoliki, hilo linawezekana kabisa. Maana ktk imani yao Papa anamamlaka ya kubadili amri za Mungu🙁🙁 Uprotestant ulianza ili kuondoa nadharia hii ya Mwanadamu kujibandika Mamlaka ya Mungu. Cha ajabu miaka mia tano (500) baada ya Martin Luther, Waprotestant wanaungana na ukatoliki🙁🙁🙁🙁🙁 Hakuna mwanadamu mwenye mamlaka ya kubadili chochote kilichoandikwa kwenye Biblia. Ufunuo 22:19 "Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki".
Martin Luther alijiondoa ukatolikini baada ya kuyabaini mapungufu zaidi ya 95 katolikini. Unapoona waliojitenga na uozo wanaurudia uozo tena (kuungana) ujue ni unabii unatimia ule wa yule mnyama 666. NEW WORLD ORDER is on the way.

Wewe ULIYEOKOKA jikamate na Yesu sana usimwache, tunaishi nyakati za hatari sana!
 
Acha unafiki....
hayo ni maoni yake binafsi sasa unafiki wake uko wapi? usijione kama umebeba imani ya wakatolik wote after all dini yako nailinganisha na punda aliyembeba Yesu kwenda yerusalem ambapo punda yule hakuingia hekaluni lakini yesu aliingia hekaluni. dini ni sawa na punda itakupeleka hadimahala fulani lakini mbinguni hutaingia na dini yako iliyochakachuliwa na wanadamu
 
Hiyo sala imeandikwa kwenye bible anataka aibadilishe.
Hahaha ndo maana hua nasema dini nuksi tu, wote mnachezeshewa story za the avengers, black panther ndiyo starring. Huyu anataka kubadilisha hiki, upande wa pili wao ni full kuchinjana ka kuku, upande wa tatu wazee wa depression hawana raha hata kidogo, hii amani iko wapi? mbona ni the total opposite? Inabidi wakati ufike watu mfungue akili, hakuna kifungo kikali ka cha dini, madawa ya kulevya ni rahisi mara mia kuacha kuliko mambo yaliyojazwa kuchwani toka utotoni.
Kingereza kingiiiii unaona ww ndio unajua kila kitu......Subiri siku yako ya kutolewa roho ndio utajua kama Kuna Dini au hakuna Maana unajiona kama umezuka tu Duniani.
 
Nafikiri waliotutafsiria bible kutoka lugha za awali walishindwa kutupa neno zuri hapo nafikiri yuko sahihi kabisa kwani maandiko yanatuambia Mungu hampitishi mtu katika majaribu bali kwa tamaa zake yeye mwenyewe
 
HAPA MADA INGEKUWA JE NI KWELI MUNGU ANATUTIA KWENYE VISHAWISHI? KAMA JIBU NI NDIYO BASI NENO USITUTIE KATIKA MAJARIBU / VISHAWISHI IKO SAWA

LAKINI KAMA MUNGU HATUWEKI KWENYE MAJARIBU BASI TAFSIRI ASITUACHE TUKAINGIA MAJARIBUNI IKO SAHIHI. MAANA KUMBE TUNAINGIA WENYEWE PALE MUNGU ANAPOTUACHA
Nafikiri Mungu hatuweki katika majaribu bali tunaingia wenyewe mkuu
 
Mimi si msomaji mzuri wa biblia lakini ninachofahamu katika kitabu cha Mathayo 6 msitari wa 7 Yesu alitoa agizo kwamba wakati wa kusali watu wasipayuke payuke kama watu wa mataifa na badala yake akafundisha hiyo sala ambayo ndani yake kuna huo mstari unaoomba Mungu asitutie majaribuni/katika vishawishi. Ina maana Yesu mwenyewe alikosea kutamka hivyo?
Inawezekana hata Yesu alilishwa maneno tu kwa sababu tafsiri hapa ndio ilikosewa kumbuka maandiko yametafsiriwa kutoka lugha za kale za kiebrania na kiamaraic na kigiriki so hapa kuna kosa katika tafsiri
Ukisema Mungu anakutia majaribuni sio kweli Mungu hamtii mtu majaribuni bali kwa tamaa zake mwenyewe
So hapo amenyoosha tafsiri inayofaa zaidi kuliko hii ya usitutie katika kishawishi
 
Kwani Papa anafikiri Mungu hawezi kuamua mtu wake kuingia majaribuni (kumtia majaribuni). Basi abadilishe na kitabu cha Ayubu kisiwepo kwenye biblia kwa maana Mungu mwenyewe aliruhusu Ayubu aingie majaribuni.
Mungu hakumtia majaribuni ayubu bali shetani ndio alimjaribu ayubu ili kuona kama anaigiza kumjua Mungu au ni kweli ni mtu wa Mungu
Ndio maana Mungu akamwambia shetani asimuue ayubu kama anafikiri mali alizonazo ndio zinamfanya ampende Mungu

Hapa huwezi sema Mungu alimtia majaribuni ayubu huko ni kutokuijua maandiko vizuri
 
Back
Top Bottom