Eyce
JF-Expert Member
- Mar 16, 2016
- 7,816
- 26,676
Mimi ni mkatoliki tena ni kiongozi wa jumuiya ila wakati mwingine huwa simuelewi Papa. Anakuwa kama anataka kuwaridhisha wanasiasa yaani kubalance siasa na dini. Mfano suala la ushoga kisiasa ni haki za binadamu, na si kidini. Kidini ushoga ni tabia na si asilia, na tabia ni roho.
Kumbe kuna haki za kidini au ndugu yangu mkuu wa jumuiya umesahau kuwa Yesu mwenyewe aliwaambia watu, kama kuna mkamilifu kati yao bhasi awe wa kwanza kutupa jiwe la kwanza kwa yule mwanamke mzinzi!!
Hicho ndicho Papa anakimaanisha daima ni kutowahukumu watu vile tunavyoona sisi inatupasa maana hiyo ni kazi ya Mungu maana kati yetu hakuna ambaye ana haki ya kurusha jiwe kwa binadamu mwenzake maana hakuna aliye mkamilifu
Tena kanuni ya kwanza kupewa ni upendo, upendo kwa Mungu na kwa jirani zetu na kwa zaidi wale waliotukosea au tunaowaona wamekosa haki mbele ya macho yetu
Kwa maana tukiwapenda wale walio wema kwetu au ndugu zetu tunakuwa tumefanya nini cha ziada kuliko wengine wasiomjua kristu.
Jivike roho ya upendo na msamaha kwa ndugu zenu kama vile baba wa mbinguni alivyo juu yenu...



