Papa amvua Upadri Padri Munyeshyaka kwa kukiri kuzaa mtoto wa Kiume

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,665
Padre Munyeshyaka raia wa Rwanda aliyekuwa akihudumu katika parokia ya Evreux kaskazini kwa Ufaransa amefukuzwa upadre na hakubaliwa kuhudumu popote duniani kwa kosa la kukiri kuwa na mtoto wa maika kumi.

195eef20-ea62-11ed-acc7-cf1ef9edf321.jpg

Padre Munyeshyaka pia anahitajika nchi Rwanda kwa makosa ya mauji ya kimbali nchini humu mwaka 1992 wakati akihudumu kama padre wa parokia moja mjini Kigari wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

====

Papa Francis amemvua upadri mzaliwa wa Rwanda ambaye amekuwa akihudumu kama kasisi kaskazini mwa Ufaransa kwa takriban miongo mitatu.

Taarifa inayosambazwa mtandaoni iliyotiwa saini na askofu wa Évreux inasema kwamba Wenceslas Munyeshyaka, 64, "anapoteza moja kwa moja haki za ukasisi" na "amezuiliwa" kutumikia "mahali popote" kama kasisi.

Ofisi ya Dayosisi ya Evreux imeithibitishia BBC uhalisi wa taarifa hiyo ambayo inasema kuwa inatokana na agizo la Papa la Machi.

Bw Munyeshyaka, ambaye alikimbilia Ufaransa baada ya mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994, hajazungumzia uamuzi huo.

Alisimamishwa kazi na Dayosisi ya Evreux mnamo Desemba 2021 baada ya kuibuka kuwa amekiri kisheria kuwa baba wa mvulana wa miaka 10.

Bw Munyeshyaka alitawazwa kuwa kasisi nchini Rwanda mwaka wa 1992 ambapo anatuhumiwa kuhusika katika mauaji ya mamia ya Watutsi waliokuwa wamekimbilia kanisani kwake katika mji mkuu wa Kigali wakati wa mauaji ya kimbari.

Mahakama nchini Ufaransa zimemuondolea mashtaka ya mauaji ya halaiki.

Chanzo: BBC Swahili

USSR
 
Kwa hiyo wameona kosa kubwa ni kuzaa na mwanamke bali siyo mauaji aliyosaidiya kuwauwa watu waliokimbilia kanisani kwake?Kweli Dini zingine zinaamriwa na mtu siyo na Mungu
 
Upumbavu mtupu kuwadanganya wapumbavu wenzie wakina miujiza heti padir ni mtakatifu anaweza kuishi maisha bila mke kama sio ukafiri nn?
 
Back
Top Bottom