Moshi: Kanisa Katoliki lamsimamisha Padri anayetuhumiwa kubaka Watoto

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Siku mbili baada ya Padri Sostenes Bahati Soka wa Jimbo la Moshi, mkoani Kilimanjaro, kushtakiwa kwa ubakaji wa watoto watatu, Kanisa Katoliki nchini limesema limemsimamisha kutoa huduma za kiroho hadi tuhuma zinazomkabili zitakapomalizika.

Padri huyo aliyekuwa paroko wa Parokia Teule ya Mtakatifu Deonis Aropagita, alifikishwa mbele ya mahakimu watatu tofauti wa mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi na ile Wilaya ya Moshi, akikabiliwa na kesi tatu za kubaka wanafunzi wenye umri wa miaka 12 na 13.

Wakati Padri huyo akifikishwa mahakamani Jumatatu hii, tovuti ya kanisa hilo Jimbo la Moshi pia imeondoa jina na picha yake kwenye orodha ya mapadri wazawa wa jimbo hilo.

Kabla ya kufikishwa mahakamani, jina lake ilikuwa pamoja na mapadri wenzake saba waliopata upadrisho mwaka 2012.

Jana, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima alilieleza Mwananchi kuwa kutokana na tuhuma hizo, Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi, Ludovick Minde amemsimamisha padri huyo kufanya kazi.

Padri Kitima alisema hayo wakati akijibu swali la gazeti hili, lililotaka kujua iwapo Padri Soka ataendelea kutoa huduma za kiroho kama kawaida.

“Kwa sasa Askofu amemsimamisha kutoa huduma za kipadri mpaka mahakama ifanye maamuzi yake. Baada ya hapo ndipo maamuzi mengine juu ya upadri yatafanyika,” alijibu Padri Kitima.

Kabla ya hapo, Padri Kitima alinukuliwa na mtandao wa BBC Swahili akisema kanisa hilo litatoa ushirikiano wa kutosha ili haki iweze kupatikana kwa pande zote katika kesi hiyo.

“Mkondo wa sheria utachukua utaratibu wake na kanisa litatoa ushirikiano ili kuhakikisha kwamba waliokosewa haki zao wametendewa haki,’’ alisema.

Padri Kitima alisema kwa ujumla Kanisa Katoliki linapingana na vitendo vya udhalilishaji kingono kwa watoto, kwa kuwa linatakiwa kuwa sehemu salama kwa watu wote.

“Tukiri hili ni tatizo ambalo ni tabia ya mtu husika, tuna mapadri zaidi ya 3,000 hapa nchini, lakini katika hao, unakuta hao wenye udhaifu na mapungufu ndiyo inakuwa hivyo,’’ alisema.

Padri Kitima alisema (kama kanisa) wanalichukulia suala hilo kama jambo baya kwa sababu linasababisha mashaka makubwa kwa wazazi na watoto.

Alisema watoto wanapokwenda kwenye shughuli za mafundisho wana matumaini kwamba wanapata mtu anayewalea kiroho, lakini wanapofanyiwa vitu kinyume na malengo “yanakuwa masikitiko makubwa”.

“Sisi kama kanisa tunasikitika kwa tabia mbaya za mtu mmojammoja, ambazo zinaenda kinyume na kile ambacho tunategemewa kukijenga -- kujenga mtu katika maadili mazuri,” alisema.

Mashtaka
Katika kesi ya kwanza, Padri Soka anatuhumiwa kumbaka mtoto wa miaka 12, kosa analotuhumiwa kulitenda Agosti 12, 2022 katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Dionis Aropagita, iliyopo barabara ya Kawawa ambapo alimwingilia mtoto huyo mwenye umri wa miaka 12.

Kwenye kesi hiyo, alitakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaojaza hati ya dhamana ya Sh10 milioni, masharti ambayo hayajatimia.

Katika kesi nyingine, Padri huyo anadaiwa kumbaka mtoto mwingine wa umri wa miaka 13 katika eneo hilo hilo la parokia. Mahakama pia ilisema dhamana iko wazi na kumtaka mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini dhamana ya Sh2.5 milioni na alitimiza sharti hilo.

Kuhusu kesi hiyo ya kwanza na ya pili, mahakama ilielezwa upelelezi umekamilika na ikaahirishwa hadi Oktoba 12, mwaka huu atakaposomewa maelezo ya awali.

Haya hapa mashtaka yanayomkabili Padri
Halikadhalika, katika kesi ya tatu, padri huyo anadaiwa kumbaka mtoto wa miaka 12 katika eneo hilohilo la Parokia. Alitimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili waliosaini hati ya Sh2 milioni. Upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na iliahirishwa hadi Oktoba 18, 2022.


Chanzo: Mwananchi
 
Mmh kachafua watoto na bado anapata dhamana daah dunia haina usawa.
 
Ujue za mwizi no 40, tunasuhiroli 40 ya waliobaki kwani ni wengi. Ila haya mambo yanafanywa kwa weledi wa hali ya juu.
 
Ujue za mwizi no 40, tunasuhiroli 40 ya waliobaki kwani ni wengi. Ila haya mambo yanafanywa kwa weledi wa hali ya juu.
Mkuu; usisubiri 40 ya waliobaki kwani ni wengi mno, tena mno - mno. Ukitambua kwamba hao ni watu(Binadamu kama mm na ww) ni wadhaifu (hata labda zaidi yetu mm na ww) hutaona shida au kushabikia kwani wamekosa/wamefanya makosa kama vile ambavyo hata mm na ww tungeliweza kufanya. Mimi sijaona cha ajabu hapo.
 
Mbona habari hizi kwa watumishi hawa zinavuma sana duniani? Kama wanaona aibu kuongoza wanawake si waende wakanunue papuchi kwenye madanguro?!
-Enhe! Kiongozi, hivi kununua papuchi kwenye madanguro ndo itakuwa sio dhambi/kosa eti?
-Wataonaje aibu wakati ndio kazi/shughuli au kama inavyosemwa ndo wito wao ili watoe Huduma shambani?
 
MCHINAJI huyu wala hajafanya jambo geni.
Katafuna kondoo wa bwana kwa raha zake manake huenda walikuwa na pepo sasa yeye ikabidi alitoe na kulikemea taratiiibu.

Dadadeki.

Oeni nyie kondoo. Mtabaka mpk the end
 
-Enhe! Kiongozi, hivi kununua papuchi kwenye madanguro ndo itakuwa sio dhambi/kosa eti?
-Wataonaje aibu wakati ndio kazi/shughuli au kama inavyosemwa ndo wito wao ili watoe Huduma shambani?
Wapendwa naona mnajaribu kuinclude watu wengi. Huyo nae atakuwa alipitiwa na Kama ni tabia ya mtu Ni ya MTU mmoja sio kuinclude mapadre wote
 
Back
Top Bottom