Papa Francis atangaza Mafinga kuwa Jimbo la Kanisa Katoliki!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
87,627
150,231
Hii Ndio habari mpya tunapoelekea Christmas

Papa Francis ametangaza Mafinga iliyo mkoa wa Iringa kuwa Jimbo la Kanisa Katoliki

===

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Fransisko ametangaza eneo la Mafinga mkoani Iringa kuwa Jimbo Jipya Katoliki na kumteua Padri Vincent Mwagala wa Jimbo Katoliki la Iringa kuwa askofu wa kwanza wa jimbo hilo jipya.

Kwa mujibu wa taarifa ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) iliyosainiwa na katibu wake mkuu, Padri Charles Kitima, leo Desemba 22, 2023, uteuzi huo unaanza leo huku jimbo hilo likipewa jina katika lugha ya kilatini ‘Mafingens’.

Askofu Mteule Mwagala amezaliwa Desemba 11, 1973 huko Makungu Wilaya ya Mufindi, Jimbo Katoliki la Iringa.

Baada ya masomo ya upadri, alipewa daraja takatifu la upadri Julai 11, 2007 jimboni Iringa na kuhudumu katika nafasi tofauti za utume nchini Italia na jimboni Iringa.

Mwananchi
 
Hii Ndio habari mpya tunapoelekea Christmas

Papa Francis ametangaza Mafinga iliyo mkoa wa Iringa kuwa Jimbo la Kanisa Katoliki
Kanisa hili linajiimarisha na kujizatiti zaidi kwa kusogeza huduma muhimu sana za kiroho kwa waamini wake wahitaji wanaoongezeka kwa wingi kila uchwao....
 
Back
Top Bottom