Mkuu jambo hili halitafanyika katika staili tu ya kubonyeza button na kila mtu kuanza kuoa. Kanisa Katoliki liko makini sana. Kujikatalia kuoa au kuolewa haikuzuka tu bali kulikuwa na sababu za msingi. Toka mwanzo wa Kanisa mapadri walikuwa wanaoa. Yako mazingira baadaye yalikuja kulazimisha watawa wasioe wala kuolewa. Hata hivyo sio jambo geni katika Kanisa. Wako Mapdri waliopokolewa toka Anglican Church wameendelea kuwa na ndoa zao.
Ninasubiria taarifa rasmi toka vyanzo vya Kanisa. Ninayo access ya matukio yote ya Papa Francis kila siku ila hii stori sijaiona! Hata siku ikitokea watawa kuruhusiwa kwa Kanisa zima kutakuwa na exceptions kadhaa na mahali kadhaa.
Kwa Afrika suala hilo linaweza kuua uinjilishaji kabisa. Waumini hawataweza kuhimili kugharimia mahitaji ya familia zitakazotokana na ndoa hizo. Moja ya sababu ni extended families. Lingine ni ukubwa Wa familia. Waafrika idadi ya watoto inaamuliwa na wanandoa na wala sio sheria. Tatu itabidi watawa walipwe mishahara ili wakae nje ya Parokia na ma-converts. Je,unafikiria mshahara gani utamtosha Padri au mtawa ili akidhi mahitaji ya maisha ya familia yake na wategemezi wake? Na vigezo gani vitatumika kumlipa Padri huyu mshahara ule au huu?
Je, pale Padri mmoja mmoja atakapohitaji kuishi na familia yake maisha fulani hivi ya juu zaidi kwa sababu ya shinikizo la mwanamke au watoto nani atagharimia hilo? Je, sio ndio chanzo cha kujiingiza kwenye biashara na mikopo ya pesa toka benki na kwa waumini? Je, ikitokea hivyo unaziona social problems zitakazoibuka?
Kwa hiyo ni jambo gumu kidogo na sio rahisi kihivyo.